Mradi wa Kituo cha Mabasi cha Green Park, ambao hapo awali ulipigiwa debe kuwa ungebadilisha hali na kupunguza msongamano CBD, unadaiwa kusimamiwa na kuendeshwa na watu wenye uhusiano na viongozi wa ngazi za juu katika serikali ya kaunti.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti la Daily Nation, kituo hicho, kilichogharimu walipa kodi Sh milioni 250 wakati wa utawala wa iliyokuwa Huduma ya Jiji la Nairobi (NMS), kinadhibitiwa na vijana wenye uhusiano wa karibu na viongozi wakuu wa kaunti.
“Watu hao wanajulikana katika maeneo ya City Hall. Wanafanyia kazi baadhi ya watu kwa kusimamia kituo hicho na kukusanya fedha kutoka kwa mabasi na magari yanayokuja kuegeshwa humo,” afisa mmoja wa City Hall aliliambia gazeti la Daily Nation.
Wakati wa uchunguzi huo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wakikusanya fedha hizo hawakuwa wahudumu rasmi wa Serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi wanaosimamia maegesho jijini. Aidha, walikubali kiasi chochote cha fedha kutoka kwa madereva iwapo wangekataa kulipa ada ya maegesho ya Sh300.
“Lipa bwana, huwezi kutoka hivyo. Tumekuchungia gari kuanzia asubuhi,” alisema mmoja wa vijana wanaodhibiti eneo hilo.
Kila dereva ambaye gari lake linapita katika lango la kuingilia analazimika kuwapa fedha vijana hao wa maegesho. Kila siku, kituo hicho hujaa magari hadi kufikia kiwango cha juu kabisa. Madereva wa magari ya masafa marefu, pamoja na matatu zinazofanya kazi ndani ya kaunti, hutumia mwanya wa mfumo huo usiofanya kazi ipasavyo kuegesha magari yao wakati wa mchana huku wakisubiri saa ambazo kuna abiria wengi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari katika City Hall, vijana wanaosimamia kituo hicho wanajulikana vyema na huwazuia wahudumu rasmi wa maegesho kuingia katika eneo hilo.
“Mapato hayo hayaingii katika hazina ya kaunti. Vijana hao ndio wanaoyadhibiti na wanajulikana na viongozi,” kilisema chanzo hicho kilichoomba kutotajwa jina. Kiliongeza kuwa walihofia kwamba kufichua utambulisho wao kungewafanya wapoteze kazi au kuchafuliwa jina na wakubwa wao.
Ikiwa kituo kilichojengwa kwa fedha za walipa kodi kimevamiwa na wahalifu wanaodaiwa kufanya biashara ya hofu, wananchi wanaweza kuwa na imani gani kwamba maeneo mengine ya umma yako salama kutokana na mtandao wa ulaghai na uhalifu?