Baada ya kuwakemea wachungaji, mitume na manabii wa kihuni, sasa zamu yenu Masheikh na Maustadhi wahuni

Baada ya kuwakemea wachungaji, mitume na manabii wa kihuni, sasa zamu yenu Masheikh na Maustadhi wahuni

Mimi ni muislam na nakubaliana nawe, kuna watu wanaiharibu dini kisa tu mali.. Huu uganga sijuk kuandika tarasimu, hawa wanaojiita kina sheikh sharifu majini na wengine wa jamii hiyo wanafanya saana shiriki.. Nakatika dhambi kubwa kabisa allah anaichukia ni hii shiriki, wengine sio kwamba hawajui wanafanya kwa kibri tu.
 
Unachotafuta utakipata

"Wilaya niliyotoka kila kijana aliye soma Quran akirudi nyumbani hugeuka mganga.
Acheni uhuni."
Akipate nini na anaongea ukweli, tusiwe wadini kiasi hatuoni makosa, kisa tu aliyekosea ni dini yetu.. Mimi muislam na ninakiri hao waduwanzi wapo, sio hao, ndani ya dini yetu kuna waduwanzi wengi tu, kuna wale wanapigana jihad haram wapo, kuna hao wanatumia elimu vibaya n.k
 
Wewe huwa unapenda kuongea vitu usivyovielewa, hivi mafuta ya mtoto mchanga unayajua bei yake na kazi zake?
Ndo hizo za giza wanauziwa tone tu kisha wanamix na mafuta ya kula,
 
Mafuta ya upako ni ushirikina, Yesu ni kamili anajitosheleza mwenyewe wala haitaji kukamilishwa na mafuta wala maji ya upako.
 
Wote hao wanafanya white magic, wanafanya uchawi makanisani kupitia jina la Yesu. Mchawi, mshirikina aathiriki kwa kulitaja jina la Yesu wanayo namna ya kumfanya kabla ya kulitamka. Kuzimu imeingia makanisani siku hizi.
 
Siku hiz wanasema mgonjwa ana damu chafu, Kuna kadudu kamoja kako Nkuhungu wenyewe wanakasifia kweli kila anayekwenda pale jibu ni damu chafu yaani, sielewi kwa Nini hawaendi kwenye hospitali na zahanati za serikali wao hawanashida ya kumdanganya mgonjwa maana mwisho wa mwezi wana mshahara kutoka serikali, sio hospitali binafsi ni lazima wadanganye ili walipe/walipwe mshahara kupitia mgonjwa.
Kila siku kwenye vituo vya afya vya serikali unaambiwa kipimo kimeharibika na wanakuelekeza kwa kwenda kupata kipimo Bora hukooo mtaani. Ajabu Sana, serikali Haina vipimo lakini watu binafsi Wana vipimo vyote. Bima za afya watu wanakata madawa kwenye maduka ya binafsi, utafika wakati madaktari na manesi watafanya kazi serikalini, lakini mishahara watalipwa na watu binafsi. Hovyo Sana. Nisameheni bure jamani.
 
Back
Top Bottom