Majok majok
JF-Expert Member
- Aug 3, 2023
- 783
- 2,057
Kiufupi labda nikwambie tu yanga watashinda na wanashinda mechi zao kwa mipango mathubuti ya kiufundi, kikosi Bora, benchi Bora la ufundi, na uongozi Bora chini ya Eng.Hersi, yanga aishindi mechi kwa utabiri wa mtu au ndoto za mtu, au mawazo ya mtu, yanga inaamini kwenye maandalizi Bora ndio uleta matokeo Bora awawezi kuingia mkenge wa kusema watamfunga Aly ahly nje ndani kwakuwa gentamycin kaliona Hilo ndotoni akiwa amelala na mke wake! Hapana soka aliko ivyo wanajipanga na watajipanga vizuri kuakikisha wanatimiza malengo yao ndani ya uwanja! Aly ahly ni wakubwa na watachezewa mpira wa kikubwa ili waje wawasimulie na wajukuu wao kwamba Kuna timu Tanzania ni habari nyingine kwenye soka la kiufundi kwa sasa!Na kwa Kujiamini kabisa na leo tena narudia kusema ( najua wana Simba SC Wenzangu mtaumia ) kuwa kwa Al Ahly FC hii hii niliyoiona ikicheza hovyo dhidi ya Simba SC hapa Dar na Cairo na ilivyocheza leo na Mamelodi Sundown FC huku Kiwango chao Kikipungua itaenda Kufungwa na Yanga SC ambayo kwa sasa iko katika Fomu na inacheza Mpira wa Kiushindi, Uhakika na wa Malengo bila kusahau wa Kimkakati pia.
Huyu Kocha Mkuu wa Al Ahly FC akimaliza Wiki ijayo kama hajafukuzwa basi nitaogelea ( nitapiga Mbizi ) kutoka Magogoni Feri hadi Kigamboni.