TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,786
- 2,095
Mchumba angu alisafiri wiki 2 zilizo pita kwenda Loliondo kunywa kikombe kwa babu. Nilivyo muuliza gonjwa gani sugu linalo kupeleka huko kwa babu akasema Kisukari huwa kinamsumbua mara kwa mara nikamwambia mbona hujawahi niambia akasema ndo hivyo. Basi nikampa baraka zote aende akapige kikombe kwa babu. Toka arudi Loliondo amebadilika sana yaani hakuna mawasiliano kabisa imefikia kipindi namuuliza kulikoni mama anasema kwaresima dah yaani kwaresima ndo inafanya hata kujuliana hali iwe ngumu. Nisadieni huyu mchumba angu nifanyaje au ndo baada ya kupiga kikombe basi ameamua kunipotezea? Msaada jamani hata usingizi sipati na kila nikumsms hajibu nikipiga anapokea anapo taka. Naona kama dalili za mawingu. Hizi naona ni dalili za kupigwa kibuti.