Baada Ya 'Machinga' Kukiona cha Mtema Kuni..! Bodaboda Wa Mjini Kati Kaeni Chonjo

Baada Ya 'Machinga' Kukiona cha Mtema Kuni..! Bodaboda Wa Mjini Kati Kaeni Chonjo

kinje ketile

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Posts
5,089
Reaction score
9,664
Wahenga Wana msemo Wao... 'Mwenzio Akinyolewa Wewe chako Tia Maji'.

Tamko la Kuondolewa Machinga Likiendelea kwa Kasi huku Mabanda Sehemu Mbalimbali Yakiendelea Kuvunjwa Jijini Dar Kwa Mzee Amos Makalla.

Ni Vema Bodaboda wa mjini Kati Wajiandae Kisaikolojia maana Chochote Kinaweza Kutokea..!

Mambo yanaweza kurudi Kama Zamani Yaani boda mwisho ni huko nje Ya mji. ..! Ukikatiza tu basi mgambo Wa Jiji unao ..!!

Ila Yote kwa Yote kutesa Kwa Zamu , mkisikia uchaguzi unakuja fasta huwa Mnapanda Cheo mnakuwa nyinyi ndo Mabosi na msishangae Watoa Matamko wanawapigia Magoti.

...Kazi na Iendelee....!
 
huwa na jiuliza ccm inashinda kwa kura za kupigiwa kweli asilimia 100%.
 
Hata bajaji pale congo ziangaliwe upya au zipangiwe utaratibu mwingine.
 
Moja moja watarudi walikokua, wawaache maraia wengine wanaolipa mamilion ya shilingi kama kodi ili kuendesha shughuli za Serikali. Watakabaki wanafanya Biashara katikati ya Miji ni wale tu wenye leseni za biashara vinginevyo turudi minadani na katika magulio.
 
Wakitokea Tegeta mwisho Mwenge, ...We Kigamboni mwisho Kivukoni na Darajani.
 
Ila mji utapendeza.
Machinga warudi makwao waache kuchafua mji, shughuli ni za kufanya ni nyongi tu sio kazima uwe machinga wanajazana mjini bila sababu za msingi.
mtu ameshika tuboksi twa viberi au nyembe ati yupo mjini ana hustle.
 
Back
Top Bottom