Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!




Mkuu hii kasi destination haionekani kwa kweli japo Mimi sio nabii naona kama by 2025 tutakuwa level moja kiuchumi na
Somalia
Liberia
Haiti
North Korea
Afghanistan
South Sudan
 
Vijana wanaofaaa kuwa warith natamani wawe
John Mnyika
Zitto kabwe(kama ataacha uzandiki
David kufulila

Huwezi muweka makonda afikiriwe nafasi kama hiyo Makonda hafai kuwa hata karani
Mtu alimpiga waziri mkuu na makamu wa rais mstaafu(warioba)
Americans waziri mkuu mstaafu(Lowasa)
Bmakonda kalaaaniwa duniani na Mbinguni
 
 

Haya ni mawazo hatari sana, hayana tofauti na ile ideology ya "Hutu Power". Unatupeleka pabaya Pascal Mayalla
 
Paskali naona umeshakata tamaa na upinzani. Mzee wako Lowasa atakulilia na kusema Paskali paskali Paskali mbona umeniacha????
 
Paskali naona umeshakata tamaa na upinzani. Mzee wako Lowasa atakulilia na kusema Paskali paskali Paskali mbona umeniacha????
Mkuu Mbase, sijakata tamaa na upinzani kwa sababu sijawahi kuwepo upinzani, hivyo mimi sii mpinzani bali ni mkereketwa wa mabadiliko tuliwategemea wapinzani ila kwa bahati mbaya sana, they have never been serious, they are not serious and they will never be serious labda kizazi kijacho.

CHADEMA Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na hamtajipanga!-2015 ni CCM tena!

Paskali
 
Nimekuelewa mtani wangu, ndicho hua nakisema hapa kila siku,unakumbuka mwaka ule tulipokuwa na mkutano pale Diamond Jubilee? kama ulikuwepo lengo la kikao kile kilikuwa kuandaa jukwaa la kudai katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu wa vyama vingi, na pia kuomba serikali ya mpito kuelekea katika mfumo wa vyama vingi wakati tunaandikia katiba mpya na ndipo NCCR ikaanzishwa. Lakini jamaa tuliowaamini wakaibadilisha NCCR kutoka jukwaa la kudai katiba mpya mpaka chama cha siasa. Hapo ndiyo hasira yangu inapokuja kwa hawa wapinzani maana walichokifanya ni kukimbilia Ikulu. Waliponikatisha tamaa NCCR nikaanza kuwa mfuasi wa Mtikilia nikiamini kama ataungwa mkono na wanasiasa wenzake wa upinzani katika kesi alizozifungua za kikatiba. Lakini leo siamini macho yangu hawa wapinzani wanaposema wameibiwa kura najiuliza nani kawaibia? Tangu lini Tanzania iliachana na chama kimoja? hawakujua kama katiba iliyopo ilikua ya chama kimoja na hivyo tume ya uchaguzi haiwezekani kuwa huru??? Hapa JF nilitegemea kua kuna ma GT kama tunavyotaka kuaminishwa lakini naona kuna wengi ama ni mbumbumbu kwa maana hawajui mageuzi yalianzaje ama vichwani ni weupe kwa maana hawatumii akili zao walizopewa na Mungu.

Watu kama kina Sumaye, Lowasa, Ulimwengu, Kingunge, Seif, Duni hawa wote ni mazao ya chuo cha siasa kivukoni. Hiki chuo kazi yake moja ilikua kuwaandaa makada wa CCM, Leo hii hawa makada ndiyo wanaitwa makamanda wa UKAWA. Hawa makada wa CCM wanasema tumerudi nyuma miaka 50, halafu hatuwaulizi nani ameturudisha huko nyuma na walikua wapi kuona hizo juhudi za kuturudisha nyuma??

Vijana wa kizazi kipya ndiyo kina Sugu, Nape, Lissu, Zitto, Kibajaji, na wengine wengi je Mayalla unaona kama kuna yeyote hapo ana hata 50% ya uwezo wa Mapalala ama Fundikira walioshindana na mtu muelevu kuliko hawa tulionao leo Mwl Nyerere?? Hawa vijana wamejawa na unafiki na mambo yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo ya ZIDUMU FIKRA AMA ZA MAGUFULI, SEIF, LIPUMBA AU MBOWE. Safari ni ndefu sana kama wananchi tuna akili hizi ninazozisoma humu JF. Nilijiunga kwa mara ya kwanza na JF ilipoanzishwa lakini nikachana nayo maana majadiliano yetu huwa partisan zaidi badala ya kuwa bipartisan.
 
Asanteni wakuu zangu Mbase1970 na paskal mayalla majadiliano yetu yamenifanya nifikiri upya juu ya siasa za Tz.
 
[emoji33] [emoji33] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Asanteni wakuu zangu Mbase1970 na paskal mayalla majadiliano yetu yamenifanya nifikiri upya juu ya siasa za Tz.
Asante sana mkuu, ndiyo lengo la kina Max kuanzisha hili jukwaa. Hakuna anayejua kila kitu ila katika kujadiliana kwa heshima ndiyo tunafahamishana. Tukijadiliana kama wa Tanzania tukaweka nje itikadi basi tutafika muafaka mzuri na tutawaonyesha wanasiasa kuwa sisi tuna akili zetu na hatutegemei wao kutuendeshea akili zetu. Mijadala ya maana na kueleweshana mara nyingi ni mizuri kwetu kama wananchi. Pale penye tija kwa Taifa basi tujadiliane kwa nguvu za hoja na siyo hoja za nguvu. Kama tunaowaita wapinzani wakileta sera za maana na manufaa kwa Taifa letu basi sisi kama wananchi tuzijadili kwa bipartisan na siyo partisan. Tukabaliane kutokubaliana bila kutukanana hapo peke yake tutaweza kuwafanya hao tuliowapa amana ya kutuongoza waelewe kuwa tuna msimamo. Pale tunapouunga mkono kila pumba iwe za Magufuli ama za Mbowe ati sababu si wa chama chetu basi ujue huo ni mtego kwetu kutoka kwa hao wanasiasa kwasababu tunatakiwa kujua kusambaratika kwetu ni furaha ya wanasiasa na watu waliopo serikalini.

Imani yangu ni kubwa sana kwamba hata kama siyo wakati wangu lakini kuna muda utafika tukifunguka macho na kuacha kufanya ushabiki wa kisiasa bila kujua manufaa yake ni nini tutafika pale tunapotaka kufika. Mifano ni mingi sana Blaise Compaore alitumia malmuki kumuua rafiki yake wa karibu aliyekuwa mwanamageuzi wa kweli kule Upper Volta ama Burkinafaso hayati Thomas Sankara kwa kutumiwa na watu wasilipenda Taifa la Burkinafaso lakini yupo wapi Compaore??? Hakupinduliwa na Jeshi bali wananchi walimpindua na kwanini walishinda yale mapinduzi sababu kubwa ilikuwa hakukuwa na makundi kama haya kwetu. Watu wanajidanganya humu kuunga mkono kila mbiu mara HAPA KAZI TU ama UKUTA, KATA FUNUA, bila hata kufuatilia ni nini hizo kauli mbinu maana yake. Maneno yenyewe ya kihuni lakini tunadandia meri tu.

Mimi ni mfuasi wa mageuzi kama nilivyosema huko nyuma bila kujali chama gani kitaleta mageuzi lakini sijaona watu serious wa kutuletea hayo mageuzi. Nilikuwa na tegemeo kidogo na huyu mkuu wetu lakini mambo yanavyoendelea naona bado sana unabii wa mwalimu Nyerere wa kusema mabadiliko yataletwa na mtu wa CCM kutokea. Magufuli katika hotuba yake bungeni mwaka jana ilinipatia matumaini kidogo lakini matumaini yalianza kupotea alipoanza kula matapishi yake mwenyewe. Sasa kairudisha serikali ya awamu ya Nne kwa mlango wa nyuma. Ukiona mtu anaongea sana mniombee kila kukicha ujue ni tapeli. najua kina Lizabon watanipinga lakini ukweli hakuna cha maana atakachokileta huyu Mtukufu.

Vijana ni wakati wenu kuchukua nchi, undeni mikakati ya maana na mchague watu wasiyo wanafiki kama kina Zitto, maana sisi kizazi chetu kimechemsha tuliowaamini kina Marando, Lamwai, Mbowe, Seif, Duni wote walikua ma agent wa CCM. Marando ni mmoja wa waasisi wa Mageuzi lakini ndiye wa kwanza kuyasambaratisha akisaidiana na mwanasheria mwenzake Lamwai. Sina imani kabisa na wanasiasa wetu wa sasa wawe wa CCM ama upinzani ninaomba sana wanithibitishe uongo.
 
Mshauri kwanza mheshimiwa akarudie kurisiti pepa la necta ili apate gamba.... sidhani kama katiba inaruhusu raisi ambaye hajamaliza fom four
 
Amekosa mamlaka ya kimaadili - moral authority! Aweke mezani vyeti vyake kwanza!
 
Wasukuma Bwana... Hivi ni Pascal au Paskali? Kama umeamua kuwa mtumwa kubali sio unabadili Jina la Malikia kuwa la kanda ya ziwa...Basi tumia hilo Mayala linatosha
 
Elimu yake nishida afadhali Magu ana elimu lkn kingine mkuu ukabila utakumaliza umeshindwa kuandika makala yako kwaueledi umebaki kushabikia udikteta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…