Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

WAKUU TUNAKUMBUSHANA TUU,

Dereva kasema wenye nguo zinazobana msitupe mwez wa kumi zitatutosha December Tutamodoa
 
Sioni mtu wa kuongoza nchi kwenye upinzani , Mbowe ? Lissu ? Sugu ? Halima Mdee , Msigwa ? Waliomo Ukawa hata kiganja hawajai , mawaziri utachagua wapi ,
Shida akili yako imefungwa unaamini serikali lazma iundwe na wanasiasa..... kwahyo wale wabunge 120 wa UKAWA hamna hata mmoja anaweza kuwa waziri??? Basi tufanye hamna kweli enhee nani kasema hawawezo fanya mabadiliko ya mfumo wakaleta mawaziri wasiotokana na wabunge wa majimboni?? Je vp zile nafasi kumi za rais hawezi teua wataalam wote kumi na akawapa uwaziri??? Au wwe akili yako inaishi kwa kukariri mfumo!!!

Shame on u
 
Lowasa hagombei tena 2020?Na je bado ana nguvu kisiasa?Jibu ni fupi-Hapana hana nguvu tena za kuua Simba.Simba ni mkali...eeh eeh aliua baba eh eh eh akaua mama...eh eeh eeh.
Ni lini chadema wamerudia mgombea urais ???
 
Paskali samahani kama nitakukwaza. Zamani zile unahoji watu maaruf ktk kile kipindi kama sikosei DTV ulikuwa vizuri sana, au niseme mpaka leo uko vizuri. Nakumbuka Issa Shivji ktk mambo ya katiba mpya yalikuwa yanamwandama. Aluvunja ukimya pale Nkuruma na ktk Kigoda cha mwal Nyerere kuwa

" Haya mambo kila mtu anachagua upande"

Sasa nimekufatilia vizuri naona umechagua upande. Simaanishi kama sio haki yako. Ila huioni hatari iliyopo inayoweza kujengeka kuwa jamii fulani au kabila fulani wanateteana au wanabebana wakipewa nafasi ya uongozi . Yaani itafanya jamii ianze kuona kabila fulani halifai kwasababu tuu wao ni kabila fulani.

Nikutakie tafakari na kazi njema.
 
Yani huyo kilaza apewe nchi?alafu hatutaki kanda moja tu,ina maana kanda nyingine hazina mtu anaefaa?
Kwani urais unatolewa kwa kuangalia kanda mtu alikotoka au tunazingatia sifa na vigezo? .

Hata ikitokea ni wa dini fulani, wanaweza kufuatana hadi hao wa dini nyingine wakidhi sifa na vigezo. Mfano Nyerere alikuwa Mkatoliki ila sifa na vigezo vya urais sio ukatoliki wake. Alipoingia Mkapa naye aliingia kwa sifa na vigezo ila pia ika just happen naye ni Mkatoliki. Sasa tunaye JPM ambaye nae amechaguliwa kwa sifa na vigezo ila pia amejust happen to be Mkatoliki. Anayefuatia pia anaweza kuwa Mkatoliki na Mkatoliki na Mkatoliki hadi na hao wengine wakidhi vigezo.

Hivyo rais ajaye baada ya JPM, anaweza kutoka Kanda ya Ziwa na kufuatiwa na Kanda ya Ziwa na kufuatiwa na Kanda ya Ziwa hadi kanda nyingine nazo zikidhi vigezo!.

Kama ilivyo kwa Bara na Zanzibar, baada ya Nyerere, aliingia Mwinyi kwa vigezo ila aka happen kuwa ni Mzanzibara. Baada ya Mwinyi hajatokea tena Mzanzibara au Mzanzibari mwenye kukidhi vigezo hivyo rais ataendelea kutoka bara na kutoka bara na kutoka bara hadi Zanzibar wakidhi vigezo.

Vivyo hivyo kwenye dini alianza Mkristu, akafuata Muislamu, kisha Mkristu tena, akafuata Muislamu, sasa ni Mkristu. Dini sio kigezo, baada ya Mkristu anaweza akafuata Mkristu, na Mkristu tena na tena au Waislamu wakafuatana.

Kinachoangaliwa hapa ni vigezo tuu. Kwenye bandiko hili nimewawekea vigezo .

Paskali
 
Kaka @pascalmaya wataka watu wavunje keyboards au kuvunja vioo vya simu zao! Kwa kweli sina mbavu, na hapo hapo nimeipenda article, ofcourse Makonda bomba, si umeona alivyojieleza kwa taadhima na kwa umakini, kajibu maswali yote bila kuhepa wala nini..Kazi kwa @cloudsfm wapeleke vithibiti na vielelezo kesi ingurume...Kama vipi washtakiwe wao @cloudsfm kwa kumchafua Makonda wetu..
Tumfagilie achukuwe nchi kwa kweli..
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za Magufuli.

2025 atatufaa sana. Kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule mama pale, au akampumzishe Musukuma na kumshikisha adabu. Atashinda na kupewa moja ya portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushika nchi, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi. Baada ya Magufuli aje Makonda, na baada ya hapo kule kule mpaka na wengine wawe ni walio wengi! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.



!
!
Waandishi wengine bwana khaaa. Tangu asubuhi Ni kusifu na kujipendekezapendekeza tu Mara hivi Mara Makonda vile
 
Paskali kuna kitu kingine anamaanisha kwenye huu uzi...i dont want to believe naively that the guy has changed so abruptly all over the sudden! Kwa tuliozoea nyuzi zake za nyuma there is something this guy tries to insinuate...sarcasm? Or a metaphorical post of its kind?? ...muda utaongea.
 
Paskali kuna kitu kingine anamaanisha kwenye huu uzi...i dont want to believe naively that the guy has changed so abruptly all over the sudden! Kwa tuliozoea nyuzi zake za nyuma there is something this guy tries to insinuate...sarcasm? Or a metaphorical post of its kind?? ...muda utaongea.
Hapana this time umepotea. He is from there and from there shall he tirelessly defend.
 
Teh teh teh! Dah aisee nchii kwa kweli kuna vioja ila tusijilazimishe kumdhihaki Mungu wa kweli jamani nchi tunaitia laana sisi wenyewe
Kweli kabisa, maana kufikia mwaka huo watu,watakuwa wamebakia wenye IQ kuanzia 10-15, hivyo mambo yatakuwa raha mstarehe
 
kina dada wa kitaa husema "ushoga ni kushikama kwa shida na raha, shoga wa kweli hamwachi shoga yake kwenye shida"
 
Makonda labda anakufaa ww mleta mada kwamaana nimeona wote akili zenu zipo sawa.
 
hii post ni ya mwezi wa pili na mwandishi ni mayalla sidhan kama hadi sasa kashikilia msimamo wake
 
Back
Top Bottom