Baada ya makongamano na shughuli za ibada Tanganyika Peaks–Kawe, nani anawajibika kwa usafi wa mazingira?

Baada ya makongamano na shughuli za ibada Tanganyika Peaks–Kawe, nani anawajibika kwa usafi wa mazingira?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
photo_2026-08-04_08-35-08.jpg
Katika kipindi cha hivi karibuni, eneo la Tanganyika Peaks–Kawe limekuwa likihudumia shughuli mbalimbali kutokana na kufanyika kwa makongamano ya kidini, hususan ibada zinazoratibiwa na Kanisa la Arise and Shine (maarufu kama kanisa la Mwamposa).

Viwanja hivyo vimeendelea kuwa na shughuli mbili za kiuchumi na kijamii Hata hivyo licha ya changamoto za usafi zinazolikumba eneo hilo, ikiwemo harufu kali ya mikojo, kuna tatizo jingine kubwa linalohitaji uwajibikaji wa haraka ili kulinda mazingira.

Nimeshuhudia taka nyingi za mifuko ya plastiki zikiwa zimetapakaa katika eneo lote bila kuokotwa. Eneo hilo limegeuka kuwa kama dampo la mifuko ya plastiki. Baada ya kufika eneo hilo kufuatia shughuli ya kiroho iliyohusisha mkesha, nilikuta mazingira yakiwa yamejaa uchafu, ikiwemo pampasi za watoto, huku kukiwa hakuna dalili za juhudi za kusafisha wala anayejali hali hiyo.

Viwanja hivyo vya wazi hubaki katika hali mbaya baada ya matukio makubwa kumalizika, jambo linaloharibu taswira na mandhari ya eneo hilo. Aidha, mifuko hiyo ya plastiki inaweza kusababisha athari kubwa kwa mazingira, ikiwemo kupelekwa baharini kutokana na ukaribu wa eneo hilo na Bahari ya Hindi.

Nimezungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya jirani, ambao wamedai kuwa hakuna uwajibikaji wa wazi kutoka kwa viongozi wa ngazi za chini kuhusu usafi wa eneo hilo. Wanasema pia wana hofu ya kulizungumzia kwa nguvu suala hili kwa sababu matukio hayo yanaratibiwa na watu wenye ushawishi mkubwa.

Wito wangu kwa Serikali, hususan Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, NEMC pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ni kufuatilia suala hili kwa karibu na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya yeyote anayeshindwa kutimiza wajibu wa kulinda mazingira.
photo_2026-08-04_08-35-09.jpg
photo_2026-08-04_08-34-57.jpg
Vilevile, natoa wito kwa waandaaji wote wa shughuli zinazofanyika katika eneo hilo, ikiwemo Kanisa la Arise and Shine, kuwajibika katika utunzaji wa mazingira kwa kuweka miundombinu ya kutosha ya kuhifadhi taka, kuhakikisha maeneo yanasafishwa mara baada ya shughuli kumalizika, na kuendelea kuwaelimisha waumini wao kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.
 
Boni najua unasoma huu ujumbe, zingatia usafi wa mazingira maana hapo ushapafanya ofisini kwako.

Linda afya ya watumishi na wateja zako usiishie tu kula hesabu za maji na wese.

#Hallelujah!!!
 
Back
Top Bottom