Baada ya maridhiano kuna haja kuendele kususa na kuzira? Njooni mezani, tukae pamoja, tuwe wamoja, twende pamoja!

Baada ya maridhiano kuna haja kuendele kususa na kuzira? Njooni mezani, tukae pamoja, tuwe wamoja, twende pamoja!

Wanabodi
Nimeona taarifa ya Mkutano huu humu Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa tarehe 3 na 4 Januari, 2024 View attachment 2855370

Mkuu Venus Star , asante sana kwa taarifa, hii sio ya kukosa!,

Ila to be honest, nina wasiwasi na baadhi promo za Mkutano huu, kama baadhi ya washiriki hawa
View attachment 2855372View attachment 2855373View attachment 2855374
View attachment 2855375kama kweli watashiriki mkutano huu this time, na kama walishirikishwa na kuridhia picha zao zitumike kuupromote huu mkutano, kwasababu huko nyuma, walisusaga na kuzira!.

Hawa jamaa, hawanaga mchezo mchezo, maana hawachelewi kuita press conference na kutangaza bado wamesusa, bado wamezira, na hawatashiriki!.

Swali ni licha ya maridhiano na kukubaliana kugawana nusu mkate! baada ya maridhiano na CCM, na kukubaliana kugawana Nusu Mkate, bado kuna haja ya wao kuendelea kususa na kuzira mikutano na vyama vingine?.

Baada ya kuususa ule Mkutano wa kwanza wa Dodoma, nikawaomba msisuse, Chadema, P'se, Msisusie Mkutano wa Vyama, Wasilisheni Hoja Zenu Mezani, Zitamfikia Samia, Ana Nia Njema na Nchi Hii, Mpeni Ushirikiano!.

Ila kususa kule kukawa na faida kwenu, kukazaa matunda ya maridhiano ambayo mmekubaliana kugawana nusu mkate, lakini Mkutano wa pili wa JNICC Dar es Salaam, mlisusa tena na kuzira!,

Nawaombeni sana, msiendelee kususa na kuzira, Please, hata kama mna hoja, njooni mezani, zileteni mezani, tukae pamoja, tuzijadili pamoja, tukiwa wamoja, ili twende pamoja!. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu, kuna vitu, ili ufanikiwe, vinahitaji a team spirit na team work, hivyo you have to be a team player and it's only if you are together, you can!.

Nawatakia Mkutano Mwema!.
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
Kuna baadhi ya vitu tunaviandika humu jf, kwenye baadhi ya hoja, tunaonekana kama tunajiandikia tuu for nothing, it's a wastage of time, money and resources, but believe it or not, it's not nothing, it's something na mfano hai ni bandiko hili, angalia nilishauri nini na angalia matokeo Mkutano Maalum wa Baraza la vyama vya siasa na wadau wa Demokrasia, January 3, 2024

Hivyo tuendelee kuandika na kushauri, baadhi ya hoja zetu humu zinasaidia.

Jf lets keep up.
Paskali
 
Nje ya Mada.....
20231228_004816_0000-png-jpg.2855372

Picha hiyo juu ya unaweza dhania Mbowe anatoa maoni yake ya Mkutano huu, ila badala yake, anaelezea jinsi alivyodondoka kwenye ngazi(alidondoshwa😁) halafu akaambiwa asimulie alifikia ngazi ya ngapi kwenda juu. Ona mkono.

Halafu picha hii, Presidential material! Yani Unaona Halima Mdee ameulizwa ana maoni gani kuhusu Mkutano huu, naye akajieleza kwa Ufasaha.

20231228_005908_0000-png-jpg.2855375
 
Na kwa mila za kiafrika, hairuhusiwi kuongea ongea wakati wa kula, tena mbele ya wazee.
 
Back
Top Bottom