Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

Hatu taki rahisi mwene njaa kwasasa na masikini asije kutufyaa kama hao walio pita sasa ivi ukitaka uraisi wa tanzania tunakupima kwa utajiri wako kama ni masikini utufai kabisa kwasasa lowasa ndo raisi wetu
 
Ngoja nipige magoti kumshukuru mungu na hao wachungaji kwa busara zao. Hakika mungu anaendelea kujibu sala zangu. Hongera mashekhe hongera wachungaji.
 
Go Lowassa go tukutane October ndio utatujuwa waTZ na Dr Slaa ni nani.

Maccm hayana mgombea zaid ya Lowassa

Tuheshimiane ndugu yangu POMPO
 

Attachments

  • 1427105672399.jpg
    73.3 KB · Views: 388
Nasubiri Mapdre nao waseme wameenda kumuomba Lowassa agombee, hakika Siku hiyo ntahasi kanisa katoliki Tanzania.
 
Makamba kaonge kweli tupu. Kwa hali ilivyo sasa ya watu kuusaka urais kwa njia mbali mbali zikiwa ni pamoja na kuwalipa watu ili waje kujifanya wanakuomba kugombea urais si ajabu tukaanza kuona misafara ya vyangu doa, mateja na mashoga wakilipwa ili kwenda kwa wagombea kuuaminisha umma ili uone kuwa wao wanafaa kuliko wenzao. Naomba siku ifike hao wote wanaowekeza urais kwa pesa na michezo michafu na ya kijinga kama hii waje kushikwa na mshangao kwa kuachwa hewani tuone hayo makundi kama yatawafuata tena. Kweli masikini hawana uhuru! Mimi naona makundi yote yanayokwenda kwa wagombea kwa kuandaliwa na kulipwa ni sawa na mazezeta waliojishushia utu na heshima yao. Walaaniwe wao na wagombea wao
 
Mi nikimwona mchungaji wangu humo kashika bango nahama kanisa
 
Poor wachungaji! Wamenena kwa lugha?
 
hakuna kitu kinachoiaumbua tz kama uji.nga wetu.
nikikumbuka ya kikwete 2005 na sasa lowasa nawaapia akipita tuna miaka mingine ya maumivu.
 
Kuna kitu hakiko sawa,yamkini kuna mambo hayako sawa. Ndugu EL na wengineo wameonekana wakiwa na shauku kubwa ya kuutaka urais. Hili halipingiki, na kwa kuwa Urais ni kazi ya kiasiasa michezo ya kisiasa lazima iwe sehemu ya njia ya kuupata. Kisichosawa ni kutumia ujinga,umaskini wa wananchi kuweza kutimiza haja ya moyo wako. Nahisi washauri wa kisiasa wa EL wamepotoka. Ni dhahiri shahiri kwa mtu mwenye common sense kuelewa sinema inayoendelea ni mchezo unaochezwa na Edo mwenyewe. Kwa lipi and kwa kipi makundi mbali mbali yakaji organise kumwomba mtu agombee wakati mtu huyo anautaka Urais kwa hali na mali.

Nafikiri inabidi Watanzania tuamke usingizini, hawa jamaa wanatumia udhaifu wa wengi katika fikra na umaskini kuweza kutimiza ndoto zao. Sinema inayoendelea sasa ni ileile iliyotumika 2005 na kutufikisha hapa tulipo sasa. Kama nchi tunahitaji mtu asie na mtandao, Mtandoa wake uwe ni watanzania maskini, Wakulima wasio na Pembejeo wala masoko ya uhakika. Wafanyakazi wasiokuwa na makazi wala kipato cha kutosha, Wanafunzi wasiokuwa na waalimu, vitabu wala majengo /madawati ya kutosha. Wanachuo wanaosoma kwa mazingira magumu,Elimu ya nadharia, Kukosa ajira kwa wahitimu n.k

Tukiruhusu watu wenye mtandao wakatawala tena Tanzania itafikia katika hali ya umaskini wa kutisha.
Tusilete siasa kwene maisha ya watu, hata kama EL alikuwa anfaa machoni pangu siku chache zilizopita, kwa nguvu anayotumia sasa nina mashaka makubwa na nia yake ya kuwatumikia watanzania. Kusema ukweli nimefuta kila aina ya ushawishi niliokuwa nikiuona, He's a complete Joke.

Alie na macho na akili na atambue sasa. Hii ni vita kati ya maskini na tajiri,walioshiba dhidi ya wenye njaa. Wanyonge dhidi ya wenye nguvu na waadilifu dhidi ya wahalifu.
 
Nakubaliana na wanaosema huyu lowassa hafai kuwa Rais. Ni mroho na mlafi wakila kitu. Iweje anunue nchi hii. Maana kama ameweza kutapeli wasomi, mashekhe, wachungaji na wanafunzi wa elimu ya juu munazani wakulima na wafugaji watawezaje kumpinga? Mbaya zaidi hata machinga waokota makopo na bodaboda nao wameshikiwa akili na huyu fisadi.
 

Hapa ndio pa kujiuliza maswali??
Kama ingelikuwa Chadema,Cuf au chama chochote wamejikusanya,wameandamana ivyo, marungu na mabomu ya machozi yangetanda kila kona.Polisi Lowassa na Maccm yao wangesema hawana vibali. Nakumbuka akina mama wa Chadema waliandamana kwenda Ikulu tena waliomba kibali wakakataliwa matokeo yake wakapigwa virungu, mabomu za machozi. Unawapiga akina mama ambao hawana hata fimbo mkononi.
Leo hii tunashuhudia tangu wiki iliyopita watu wanaandamana bila kibali, na kuzuia baadhi ya mawaziri, wabunge kutoka kwenye Makazi yao. Polisi Ccm na Lowassa wao wako kimya, mahema yamejengwa watu wanakunywa na kucheza uku polisi wako kimya.
Hii kama sio kampeni ni nini??
Tamko la Waislam, Wakristo tumezisikia kutoka kwa viongozi wao waonaotambulika kisheria.

Lowassa anafanya kampeni waziwazi kwa kugawa pesa kwa watu wake na kukusanya watu, Chama chake,Polisi wako kimya.
Hapa wanaleta mazingira ya fujo, Lowassa anafikiri wenzake ndani ya ccm nao hawana wafuasi wa kuwafanyia maandamano.
Kazi ipo ndani ya ccm,
NAWAAMBIA MACCM ZITTO KAENDA KWENYE CHAMA CHAKE (ACT) ATAKAYEMFUATA NI LOWASSA KAMA ATATEMWA KUTOKUGOMBEA URAIS.

Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.
WATANZANIA AMKENI ACHANENI NA PROPAGANDA,HASA VIJANA KOMBOENI NCHI YENU ACHENI KUWA WATUMWA NDANI YA NCHI YENU.MSIKUBALI KUONGWA NA VIJISENTI YA SIKU MBILI BAADAE UNASOTA KWA MIAKA MITANO. AMKA SASA,USINGOJE KESHO.
 
Anayeamini kuwa hawa ni viongozi wa DINI anyoshe mkono juu!:doh:
 
Halahala sitaki kuwepo kwenye "walimu" watakaoenda kwa lowasa, maana nadhani kesho itakuwa zamu ya walimu, mimi najitoa mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…