Elections 2015 Baada ya Masheikh wa Bagamoyo, Wachungaji wamzamia Edward Lowassa kumuomba kugombea Urais

Hawa wachungaji mbuzi ndiyo waliosema kikwete ni chaguo la Mungu, hawa akili zao hawatofautiani sana na Pengo sema mavazi tu.
 
Hawa baadae ndo wanakuja kutusumbua waumin hali ikiwa mbaya ya kiuchumi ooh hamtoi sadaka kumbe tatzo wanalianzsha wao

Safari hii dini zimeingilia. Hakika naamini sasa hawa wanaojiita watumishi ni Ushetani mtupu umewajaa. Hawana hata haya kukomaa na mambo ya siasa. Halafu wamepiga rushwa.
 
lowassa ni mafuriko,hayazuiliki kwa kiganja cha mkono......ndio chaguo letu milele,sio Jk wala NEC au CC inayoweza kumzuia,sisi wanachama hai wa ccm ndio tumeamua kumshawishi agombee urais
 
Hivi kweli tumefikia hatua hii kama Taifa.......mpk viongozi wetu wa dini nao wameingia kwenye huo mkumbo?
MUNGU ATUSAIDIE.

sifongo ndugu yangu kuna dini kweli. Lakini kuna watu siku hizi kila kukicha wanaanzisha kanisa. Sasa haooooo ndiyo haoooooo wanaofanya hayooo. Njaa mbaya watoto wanamsubiri baba mchungaji alete mboga mshahara kiduchu, mama mchungaji nae anataka aishi maisha ya juu, inabidi baba ajitose kwenye kujiuza kisiasa apate chochote kitu.
 

Upepo wa nchi hii unakoelekea ni kubaya ,ikiwa masheikh na wachunga kondoo wa bwana wameingia katika mtego huu nani tena wa kumtumaini kukemea maovu? Nilidhani watu kama hawa wangekuwa neutral ili wawe waamuzi wa haki kwa yale yanayoendelea nchini. Lakini haya yote ni matokeao ya harambee zilizokuwa zikiendeshwa na Lowassa misikitini na makanisani, sasa ni zamu yao kulipa fadhila.
 
Kazu butu Lowassa tupo nyuma yako baba, na tunakusubiri October ambapo hapatakuwa na wachungaji, wanafunzi wala mashekh. Furaha yetu tunataka uikate ccm vipandevipande. Kaza butu fisadi wetu, mpaka ccm ikujue kuwa wewe siyo joka la makengeza bali joka lenye macho kama paka mwitu.
 
Hofu ya Mungu hakuna tena, watu wanaangalia matumbo yao tu,
 

Kama tatizo la MB 8 limemshinda tukimpa nchi si ndio atatuuza huyu mwehu.
 
1. Hivi huyu Lowasa ndiye yule mshirika mkuu wa Kikwete aliyeingusha nchi kiaisi hiki?

2. Hivi huyu Lowasa ndiye mshiraka mkuu wa Rostam azizi aliyeshirikiana na Lowasa katika mpango mzito wa WIZI WA EPA uliotumika kumuingiza JK madarakani?

3. Je, huyu Lowasa ndiye yule aliyesema ukipata fursa ya kukwapua, we kwapua tu. Ndiye aliyekwapua ranchi mbalimbali za serikali na kijimilikisha n.k, n.k?

Wananchi wa Tanzania tumekuwa vipofu wa namna gani?

Hii ni ngoma gani tunayoicheza? Ni kweli kuwa tuko tayari kuingiza kundi lilelile lililotufikisha hapa tulipo?

Sianamini, hii naona kama vile inawezekana Tanzania tu!

Ama kweli, tuzidi kuomba ili shida ziongezeke
 
Hana maadili ni msanii tu urais hauombwi huyo ni muigizaji tu
 
Hakuna namna nyingine ni Lowasa tu!! Hata wewe unalijua hilo sema maslahi ndio yanakufanya uwe mnafki hapa.
 

Labda nikuulize mheshimiwa makamba! makundi hayo yooote yangeandamana kukusihi wewe uchukue form ya kugombea urais 2015 ungetoa hilo tamko!!???
 
Mwalimu aliwahi kusema kuwa ccm dhaifu itayumbisha nchi!
ni nani ameidhoofisha ccm kiasii hiki!?
 

Haya sasa masheikh walikua wa Bagamoyo na wachungaji ni wa wapi? Ila msiniambie ni wa sehemu tofauti tofauti kama mabango yanavoonesha kama ni hivo nani aliwaoganize mmoja katoka Masasi mwingine Tunduma wamewasilianaje wakaenda leo na muda ule ule wote??? otherwise kuna dhehebu moja tu la kikristo kalihonga plz anaejua atujuze kwa hili.

Inawezekana hawa wamenunuliwa suti tu na tai kama wachungaji ili kuendeleza igizo, ngoja watazamaji tuendelee kusubiri movie inaishaje ila wakumbuke star hafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…