Baada ya matendo yake sina hisia nae tena, nifanyaje?

Wewe kwanza, hamna atakaekuja kukujali kama usipojijali wewe.

Tatizo la wanawake wengi ni kua nikiachana nae nitaonekanaje, nitakua sina mume, umri huu siwezi kupata mume na vitu kama hizo ila kama moyo haupo hapo ni kheri mkaachana.
 
Kwanza pole lakini mjifunze kushirikisha watu katika ndoa zenu hakuna cha rafiki wala nini japo sio solution moja kwa moja ila hatua moja umefanya kuepuka haya mambo. Mimi naamini hujasamehe bado inaweza kuchukuwa muda sana na uhakika viti viwili vimekuumiza sana, ku cheat na mtu wako wa karibu angekuwa mtu humjui nafsi yako ingesamehe, pili kutolewa siri zako na mumeo kwa rafiki yako. Sasa sijui hivo vikao vya family huwa mnaongea nini? Ila kwa sisi wanaume basi hata kama unacheat jitahidi kwenda mbali lakini kubwa tusiwavunjie heshima wake zetu kwa kuwasema vibaya nje, kwani ku cheat lazima umkashifu mkeo? Mimi siku zote nasema ukiona mtu anamsema mkewe au mke anamsema mume nje huyo kama unaweza kimbia.
 
Tatizo ni yeye mwenyewe.
To yeye Mwanamke wa mithali 31 Lamomy Numbisa kapitieni huo uzi wake halafu mumshauri tena.
 
Mwishowe mtaachana tu, huwa haviponi vidonda vya hivyo!
 
Bi dentamol una vita ya kiroho aisee, kama ni muumini anza kusali kwa bidii uondokane na hizo roho zilizokuvaa. Sasa wewe kumbe ndio ulikuwa ni mkorofi unapigana na Mumeo kwa mujibu wa uzi wako rejea post #171. Pambana anza kusali. Kama ni MKristo tafuta kanisa lenye mafundisho ya kukujenga kiroho. Maana hela na uchumi tayari unao 🤣🤣🤣

Kama ni Muislamu anza kwenda msikitini anza kusali kwa juhudi zote, soma quran zifuate na nguzo zote za Uislamu.
Simple like that.
 
msamehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…