Mkuu umekosea sana kushauri hivyo.
Hakuna popote, iwe mabaraza ya usuluhishi kwa 'mwenyekiti', ya kata ama mahakamani utasikia mtu anawashauri wanandoa 'ondoka' kwa urahisi namna hiyo.
Wadhani hiyo 'ondoka' mhusika haifahamu, kwa nini mpaka sasa yupo na wanaendelea na maisha?
Kwa nini anatafuta ushauri badala ya kujichukulia maamuzi?
Nadhani kwa kuwa sote tunaelekea kuwa ni wazee, yanapokuja kwako mashauri yahusuyo ndoa, yakupasa ureflex brain yako sawasawa, wanasema kukaza fuvu ili uweze kutoa maamuzi ama ushauri usioumiza ama kuegemea upande na kuonesha mapungufu yako.
Masuala ya ndoa hayatakiwi kushauri kwa kutumia malezo ya upande mmoja.
Huyo 'mtuhumiwa' ilitakiwa naye tumsikilize ndiyo tueweze kutoa ushauri wa maana.
Vinginevyo haiwezekani, ni kupoteza tu muda.