Pole sana kwa unayopitia.
Machozi yanayokuja katikati ya tendo ni ishara kwamba kuna sehemu ya moyo wako bado haijapona. Sawa kabisa kulia ni sehemu ya kuachilia maumivu.
Jitunze na ujipende mwenyewe kwanza (self-care)
Fanya vitu vinavyokufurahisha au vinavyokupa utulivu wa moyo vaa vizuri pendeza vaa na usuke fashion pia inasaidia.
Usilazimishe kusamehe haraka
Kusamehe si jambo la ghafla, ni mchakato. Pia, kusamehe haimaanishi kwamba unasahau aliyotenda au kurudisha hali kama ilivyokuwa. Inaweza kuchukua muda mrefu, na hiyo ni sawa.
Chukua muda wa kutafakari maisha yako ya mbele. Je, bado unataka kuendelea na ndoa au lah.. Unajiona ukipata furaha tena ndani ya ndoa yenu?
Kumbuka kuwa Afya yako ya akili ni ya muhimu sana, na unastahili amani na furaha, hata kama itabidi kuchukua muda.