Baada ya Matokeo ya jana: Mwanachama Agnatius Obel aibuka na haya

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Japo ni makala ndefu kidogo, wanamsimbazi wenzangu kipindi tunaendelea kutafakari matekeo ya jana.. nadhani ni vyema pia tukapata mawazo ya mwanachama mwenzetu AGNATIUS OBEL.


Waisome Masuke Freeland grafani11 geniveros Amavubi barafuyamoto Ngarna Komeo Lachuma na wanachama wote wa Simba Sc.


SOURCE: simbaplatinumsuppoters.blogspot.com
 
Sisi mashabiki wa hizi timu ni wanafiki sana,mimi ni mshabiki wa Yanga nilipenda sana Wambura aruhusiwe kugombea naamini angeshinda ndio kiongozi ambaye angeweza kuleta mabadiliko,watu walimfanyia fitina bila sababu za msingi,tatizo la Simba ni uongozi kibaya zaidi makocha wanatolewa kafara,misimu 2 iliyopita hakuna kocha wa Simba ambae amewahi kumaliza msimu,hiyo kamati ya usajili ndio hamna kitu kabisa
 

mi nashukuru sana kuwa mpira wa bongo na mimi mbali mbali,sina hata cha kushabikia zaidi ya kuwa mshabaki kama timu ya nyumbani inacheza na timu ya nje ya tz but otherwise,mpira ulaya
 
Simba yetu ina matatizo makubwa ya kimfumo

Kiongozi yeyote akiingia mfumo ukabaki uleule hataweza kufanya kitu

Timu inatakiwa ijitegemee...ifanye mambo yake kama timu

Inawezekana

Watupatie sisi timu waone kama in Five years haitakuwa na Billion shillings assets
 
kitu chochote ukiona kinayumba basi ujue aliyekuwa kiongozi wa kwanza ndie aliyesababisha hayo.laana ya kiongozi wa kwanza wa simba bado inaendelea kuitafuna hadi leo.hii si mara ya kwanza simba kufukuzafukuza makocha,hiyo fukuzafukuza alikuwepo kuanzia miaka 1950s labda nikuhabarishe
 
Tokea lini mkia ukawa kichwa...

Mwaka huu mtaambulia sare na vibano hadi mjute...
 
Huyu jamaa Agnatius Obel kanifanya nifikiri kwa nguvu saana yafuatayo;

1.Muenendo usioridhisha wa timu, ulianza tangu misimu kadhaa iliyopita.

2. Ndani ya kipindi hicho chote Friends Of Simba [FOS] walikua bega kwa bega na viongozi mbali mbali wa klabu hadi walipoamua kuchukua timu katka uchaguzi uliopita.

3. Lastly wanasimba wenzangu, nachokiona mimi tusitegemee jipya saaana msimu huu maana katika uongozi wetu tuna "sura mpya ila miguu ni ile ile ya zamani".
 

Mkuu ulichonena ni sawa kabisa. Taarifa nilizonazo ni kuwa sifa kubwa ya Aveva ni mpole pia ni mtu mwoga kuchukua maamuzi ya haraka.. na hufanya hivi ili kumfurahisha kila mtu anayemzunguka. Hii imesababisha kila mtu kuwa na sauti.. matokeo yake ni kama tunavyoyaona. Nadhani ni mda muafaka wa kuondokana na huu mfumo uliopo, lasivyo tutaendelea kuwa wanyonge kila siku.
 
Timu yetu inaharibiwa na Kaburu na Hanspope, inawezekana kweli wanatoa hela kwa ajili ya kusajili na pengine kusaidia kambi lakini ni kwa nini wajihusishe na uongozi wa timu? Kwa nini wao ndo wanajifanya wasemaji wa timu? Kitendo cha Hanspope kipindi kile kusema kwamba kama atachaguliwa Wambura yeye hatajihusisha na timu kilikuwa na maana gani au alijua Wambura hana sensor ya kunasa signal zake za remote control? Kwa nini Kaburu alijiuzulu kipindi cha Rage na baadaye akagombea kwa cheo hicho hicho kwa nini hakutaka kugombea hata cheo cha juu kabisa kama aliona kwamba walitofautiana na Rage kwa Rage alikuwa boss wake? Kaburu hutumika sana kugawa wachezaji na kauli za mara kwa mara anazozitoa Hanspope kwenye vyombo vya habari zinavunja moyo wachezaji.

Hanspope anatakiwa ajipime yeye kama m/kiti wa usajili kwa muda mrefu sasa ndo anayeangusha timu. Na kwani lazima kuwe na utitiri wa kamati hivyo, hivi hizi kamati zinasaidia nini hasa? Hivi kukiwa na m/kiti na katibu na wajumbe wachache halafu kukawa na kocha tu na msaidizi wake haiwezi kuwa timu? Huu mfumo wa kuwa na kamati lukuki hivi ulitoka wapi? Na je ni mfumo mzuri hadi sisi tuendelee nao?

Naamini wachezaji walioko Simba ni wazuri kwa standard ya mpira wetu wa kitanzania nadhani tatizo la wachezaji wengi linaweza kuwa saikolojia kuliko hata ufundi au utimamu wa mwili. Hanspope na Kaburu mwacheni kocha afanye kazi yake hata kama mnatoa hela zenu mbona Mohamed Enterprises walikuwa wanatoa hela nyingi sana kuliko hata hizo zenu na hakuwahi kuvuruga team? Mbona Dioniz Malinzi naye aliyeshawahi kutoa hela zake na hakuwahi kuvuruga team? Mbona TBL wanatoa hela nyingi sana na hawavurugi timu? Mbona mashabiki tunatoa hela zetu za viingilio na bado hatuvurugi timu?

Viongozi wa Simba na wachezaji lazima wajue wapo watu wengi sana tena mamilioni wako nyuma yao wanaumia sana kuona timu yao waliyoipenda toka utotoni ikizidi kuharibikiwa.
 

Nahisi hujanielewa sembo

Ndani ya simba kuna watu wazuri sana...Aveva anaweza kuwa mzuri,Hanspope,Kaburu,Rage na wengine

Tatizo ni kwamba ,Je timu ina mifumo imara ya kuifanya iendelee pasipo kutegemea pesa za watu binafsi.

Matatizo yetu yako kimsingi katika timu kutukuza watu binafsi na kudhani bila wao timu haiendi mbele

Sio kweli.

Simba hii inahitaji vijana wenye mitazamo ya kimapinduzi.

Hawa wafanyabiashara wana interest zao.

Brand ya Simba ni brand kubwa sana....You may get a lot of billions through it
 
Last edited by a moderator:
Mkuu unachosema ni kweli, lakini kama hujapata kiongozi mwenye hayo maono hela zinakujaje? Zitakuja watu watakula. Tatizo lililopo sasa pamoja na kwamba mfumo nao ni mbaya ni viongozi kugawa wachezaji na kila mmoja kujifanya ana amri juu ya wachezaji eti kwa sababu tu ni kiongozi. Team ya mpira ina mkusanyiko wa watu ambao wanatakiwa kufikia lengo moja hivyo wanahitaji commanding chain haiwezekani kila mtu aseme na wachezaji tena wakati mwingine kwenye mambo ya ufundi. Hizi kamati sizipendi kabisa na wala hata kuzisikia huwa sipendi lakini kwa sababu zipo tayari ingekuwa ni busara kila mtu afanye mambo yake yanayomhusu.
 
Last edited by a moderator:

Nimekusoma Mkuu
 
Last edited by a moderator:
Mimi hakuna kitu nashangaa kama Hans Pope kuwa msemaji wa hii Timu na kwa nini wanampa uongozi wa hizo kamati kama Katiba hamruhusu kugombea uongozi wowote huu ni ubabaishaj.
 
Bado tuna tatizo la ufundi tu ambalo licha ya mtoa mada kukosa flow ameliainisha mnwanzoni mwa mada yake, wachezaji wengi tunasajili kwa makeke lakn hawatusaidii kabisa

eti mesi wa tanga, mara adbi banda anagombewa na yanga, serunkuma, etc................yaani madogo ndio wanabeba timu kwa kiasi fulani na ambao wanaonekan kuchka mapema tizama ndemla ameshaanza misuli, mkude naye hatihati
 
mimi hakuna kitu nashangaa kama hans pope kuwa msemaji wa hii timu na kwa nini wanampa uongozi wa hizo kamati kama katiba hamruhusu kugombea uongozi wowote huu ni ubabaishaj.
you are missing the poitn
 
Timu yetu inaharibiwa na Kaburu na Hanspope, inawezekana kweli wanatoa hela kwa ajili ya kusajili na pengine kusaidia kambi lakini ni kwa nini wajihusishe na uongozi wa timu?
HE WHO PAY THE PAWPER PLAYS THE TUNE
 
nimejionea timu imepambana sana lkn soka la sasa si la utawala ule ambao tulizoea kwenda uwanjani na kushinda, tmu zina wafadhili kama MCC, zinakula vizuri, zina washangiliaji so simba inakua kama timu zingine tu, hata Liver tulitawala soka la UK, lkn leo hata akina QPR wanajipigia, lazima tukubali mabadiliko
 
Ujerumani katika miaka 88 ya soka walibadili makocha mara nane (8) tu, simba katika miaka nane ya soka huenda tuna makocha zaidi ya 88
 
Yes brother tell what is that.
read my threads, timu inajitahidi sana, lkn roho i radhi ilihali mwili ni dhaifu, nitakua wa mwishoi kuwalaumu hawa viongozi, nimekuwa kwenye soka naelewa what it means, jana Hanspope alikua anatoa machozi paple VIP unajua ni kwa nini, ana invest a lot while deliverables ni almost nothing
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…