Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,204
- 3,277
Tangu Rais Magufuli aingie madarakani, tumeshuhudia kila mbinu imetumika kuhakikisha mwenye mawazo mbadala hatoi maoni yake kwa namna yoyote ile. Kwa miaka 5 vyazo vyote vya habari vilitekwa, kila chombo cha habari kilihakikisha kinatangaza sifa za mfalme, kuna TV zimediliki hata kuacha mipangilio yao ya vipindi na kupiga kambi kwenye jumba la mfalme ili kurusha uapisho wa mkuu wa wilaya Live ili sifa na taarifa za mfalme zifike kila kona ya nchi, walishindwa tu kuingia chumbani kwa mfalme.
Baadhi ya TV zilienda mbali, zilihakikisha 80% matangazo yake ni vipindi maalum kwa ajili ya kusifu madege ya bombadier, fly over nk. Baadhi ya vyombo vya habari kama Tanzania Daima hadi sasa limefungiwa kwa sababu halikuweza kumsifu mfalme inavyotakiwa, lakini waliofanikiwa kumsifu mfalme tena kwa kutukana wapinzani wameachwa (Uhuru, Jamvi la habari, nk).
Upande wa wapinzani; Wapinzani wamefumbwa mdomo kwa miaka mitano, hawakuruhusiwa hata kufanya mikutano yao ya ndani, wakifanikiwa kufanya basi taarifa zao zitokee youtube yenye usajili wa nje ya nchi. Wafanyakazi wa serikali walitakiwa kabla ya kutoa hotuba/speech ni lazima asifu jina la mfalme ndipo iwe kheri yake.
Pamoja na hayo yote juu, tulitarajia kuwa upinzani umekufa kabisa na mfalme arudi bila kupingwa, cha kustaajabisha kuna wagombea zaidi ya 15 wamejitokeza kupambana na mfalme. Lakini jambo la kushangaza, tangu mwana wa risasi 16 aliporejea nchini, Watanzania wameonesha kuwa pamoja na vyanzo vyote vya habari kuhakikisha wanamsifu mfalme, bado upinzani unaonekana kuwepo kuliko ilivyodhaniwa.