Dawa ya Uvccm
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 2,223
- 4,717
kisa kasema sukuma gangMbowe Kwisha ndembe ndembe
Kwa siasa zile za kishetani za mwendazake,Acha mama atutoe huko na mbowe hata lama atakuwa Mrema sawa tu,cha msingi turudi kwenye siasa zetu za 2015 kurudi nyuma.Najua wafuasi wa JIWE Mnaumia sana kwa hiki mama anachokifanya!!!!Ndio basi tena na kosa hilo la kumpa nchi MPOLI POLI halitajirudia tena!MUNGU FUNDI
Tatizo lako umeaangalia upande mmoja siasa ni kutumia akili nyingi kushika dola bila madhara mbinu nyingi zimetumika hakukuwa na mafanikio labda ulitaka damu imwagike lkn hata hivyo watz hawako tayari kutumia nguvu kushika dola badala yake ni kujaribu mbinu za klia aina ili kuoweka nchi salama wewe unafikiri ni rahisi rais wa ccm kuhudhuria shughuli za cdm? Huoni kuwa ccm inweza kumezwa na cdm? Au na wao ccm wamelamba asali? Hapa kama kuna political technic inachezwa? Sawa na mchezo wa draft?
kisa sukuma gang kasema, nenden mkamuulize yule mbwa mliyemtupa chato kama aliweza kuiuwa chadema ukipata hilo jibu ndio uje hapa useme kama inakufa kwa mara nyingine.Mlalo wa Mende, chali
Ungekuwa hata wewe ungebadili tu mtizamo maana unaowapigania hawajielewi na wakati huo huo dola inakuumiza kwa kuharibu biashara zako na kesi za kutunga hadi kuwekwa ndaniKwa hali inavyoendelea nchini ni dhahiri hakuna tena upinzani. Bali kuna uungwaji mkono juhudi wa Wapinzani kwa CCM kila mmoja kwa staili yake. ACT Wazalendo wanakula pamoja na CCM kule Zanzibar na CHADEMA nao wanatafuta robo mkate wao huku Tanganyika.
Kabla CHadema hawajaanza kupetiwapetiwa, Kutomaswatomaswa na kulambishwa asali na CCM hii ya leo ya Kinana na Samia, walikuwa wakitokwa povu sana kuhusu ACT Wazalendo kuingia katika serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar. ACT walikuwa wakijitetea kuwa eti ni takwa la kikatiba kuingia humo huku CHADEMA wakiwaita ACT Wasaliti kwa hoja ya kuwa wamewasaliti Wazanzibar kwa kushiriki kula matunda ya uchaguzi haramu.
Leo tunaona CHADEMA nao wamekinga mkono kula ruzuku ambayo hapo mwanzo walisema ni haramu kwa kuwa imetokana na uchaguzi haramu. Kiufupi wamelamba matapishi yao!.
Ukiachilia mbali hilo, CHADEMA walikuwa wakijulikana sana kuwatukana akina hayati Lyatonga Mrema , John Cheyo na Shibuda kuwa eti ni makada wa CCM kutokana na kuwa na siasa za mrengo wa kukubaliana na CCM katika mambo mengi. Leo tunamuona Mwenyekiti Mbowe naye akigeuka kuwa Cheyo na Shibuda aliyechangamka zaidi.
Mbowe leo kaibeba rasmi mikoba ya John Cheyo na ameanza kutumia arguments zilezile za John Cheyo kuwa anataka siasa za "maridhiano", ambazo kimsingi siasa za hivyo ni za kutomasanatomasana, kubembelezanabembelezana ilimradi tu kila mtu aachiwe sphere yake ya influence ili aweze kula kwa urefu wa kamba yake.
Tujiulize, Hizi sifa ambazo Mbowe anazitoa kwa Samia zina tofauti gani kwa mfano na Sifa za Cheyo au Shibuda walizokuwa wakizimwaga kwa Magufuli?
Hii inaonyesha kuwa pengine ukiwa mpinzani na ukaanza kuzeeka, unaanza kuwa na tabia za OLD MAN CCM SYNDROME. Yaani unaanza kuwa na tabia zile za kiCCM CCM. Unaanza kujisogeza kwa CCM, unaanza kuongea kama wanaCCM, na unaanza kubehave kama wanaCCM
Huu ni muda muafaka kwa wanaCHADEMA kumtafakari Mwenyekiti Mbowe kuona kuwa , Je ni kweli siasa hizi za kulala kitanda kimoja na CCM anazoanza kuzifanya zinatokana na utafiti wa kina na upeo wa kisiasa au zinatokana na
1. Mosi, Je ana makubaliano ya siri na CCM ikiwa kama sababu ya kuachiwa kwake Jela na kwa hivyo anafuata script aliyotengenezewa AU
2. Je ana masilahi bianfsi ikiwemo ya kibiashara au kurudishiwa mali zake alizoporwa na serikali ya CCM kipindi cha Mwendazake?
3. Au je ni uzee na uchovu(wa Kisiasa) kwa hiyo ndo ameamua kwenda na falsafa maarufu ya "Kama huwezi kuwashinda, basi ungana nao?".
Katika nchi yoyote ukiona UPINZANI unafanya ROMANCE na Chama Tawala, Jua kuwa hakuna upinzani hapo bali kuna genge la wapiga dili wa kisiasa
anzisha chama chako ili uwe na upinzan wako nyumban kwenu.hayana tofauti na yale yaliyofanyika awamu ya 5 😃 huku tunaambiwa ni maridhiano kule ilikuwa ni kuunga mkono juhudi
upinzani Tanzania haujawahi kuwepo na hautokaa kuja kuwepo
ulitaka imezwe na sukuma gang.Yaan system imezwe na Wachaga wa Machami[emoji13][emoji13][emoji81]
Ebu amkaa utajikojolea bwashe
kisa bwabwa la sukuma gang limesema.Kama ni hivyo basi Jiwe ana wafusi wengi kuliko hata sacoss yenu.
Kati ya wanajf 5000 unakuta 4000 wana wasiwasi na maridhiano feki[emoji23]
Kwa iyo shibuda na cheyo walikuwa watu makini sana eeKwanin wewe unataka watu wataseke kwa niaba yao huku wewe ukiwa nyuma ya keyboard kama unaona wameshindwa kazi ingia mzigoni hujakatazwa
Umesema wewe na sio mimKwa iyo shibuda na cheyo walikuwa watu makini sana ee
Kuna watu na vyama vyao waliowahi kujiweka sawa na serikali ya awamu ya 6 wakitarajia kutambulika kama ndio viongozi rasmi wa upinzani wakiamini CHADEMA itaendelea kuwa adui wa serikali kama ilivyokuwa enzi za giza za Magufuli.Yes. Ni kweli kabisa..
Sijui kina Missile of the Nation ni kwanini tu wanaendelea kulilia siasa za uhasama za kuviziana na kupigana risasi, kutekana, kupotezana na kuuana ziendelee..
Mimi naona mambo yanaendelea vizuri kabisa. Vyama vya upinzani vinaendelea na siasa za majukwaani vyema Kwa kuikosoa na kuisema CCM kwelikweli. Katika situation kama hii mtu anawezaje kudai upinzani umekufa? Umekufaje Kwa mfano? Kwa kuwa CCM na CHADEMA wameweza kukaa pamoja na kukubaliana kuachana na siasa za uhasama wa kuuana?
Aaah, please give me a break ndugu Missile of the Nation !!
Hayo alifanya lipumba mkamtukana sanaKuna watu na vyama vyao waliowahi kujiweka sawa na serikali ya awamu ya 6 wakitarajia kutambulika kama ndio viongozi rasmi wa upinzani wakiamini CHADEMA itaendelea kuwa adui wa serikali kama ilivyokuwa enzi za giza za Magufuli.
Wametibuliwa sana kwanza na jinsi Mama SSH alivyoanza na kuwanyooshea CHADEMA tawi la mzeituni kuomba amani na kuanza kusahihisha maovu mengi waliyofanyiwa. Pili kwenda na CHADEMA kuhusu hoja ya katiba mpya kisha tume huru. Tatu kufuta kesi za kihuni na kuachia wafungwa wa kisiasa. Na sasa mazungumzo yanayoendelea ya maridhiano!
Imewachanganya sana waliozoea kuona nguvu kubwa ya serikali na dola ikitumika kuifanyia CHADEMA hujuma na udhalilishaji wa kila aina kama uliowalegeza kina Mdee, kuwaibia ushindi halali wa ubunge, kisha “kuwasweka” Bungeni kama viti maalum kinyume cha Katiba.
Waliozoea na kufurahia hayo sasa wanahangaika kumchafua Mbowe na chama chake. Nawaambia wavute subira. Ukweli kuhusu hayo maridhiano utafika soon. Kwa watu waliozoea kuishi chini ya udikteta wa TANU/CCM tangu 1961 hawastahili kukosa subira kwa hili.
Sawa. Basi tusubiri hiyo “serikali ya umoja wa kitaifa” kati ya CCM na CHADEMA.Hayo alifanya lipumba mkamtukana sana
Mkuu Tindo ahsante kwa hii komenti Jana nimesema Sana lkn nikatukanwa lkn ukweli usemwe ...Hayo yanayofanywa Wala sio maridhiano Bali Ni mgawo wa Asali TU... Nipo tayari kuuawa kwa msimamo huu,, Upinzani kukaa na serikali hayo sio maridhiano,,Wapinzani sisi hatuelewi huo msimamo wa viongozi wa CDM kwa muongozo wa Mbowe. Wao viongozi waendelee na siasa za kujikomba, lakini sisi hatuna muda huo. Kama Mbowe aliweza kumpokea Lowassa na watu wakamvumilia, basi safari hii atajua hana ushawishi huo aliodhani anao. Ni muda mrefu Mbowe alishaonyesha kupoteza mwelekeo.