Pre GE2025 Baada ya Mbowe kutetea uenyekiti wake, masikini Tundu Lissu, kwishney! Je, atabaki ama atatimka? Lissu Cool down, usiitishe Press kumjibu Mbowe!

Pre GE2025 Baada ya Mbowe kutetea uenyekiti wake, masikini Tundu Lissu, kwishney! Je, atabaki ama atatimka? Lissu Cool down, usiitishe Press kumjibu Mbowe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani uchaguzi hautakuepo, tunategemea nyie wakongwe kutetea demokurasia na kuongoza vijana sio kuonyesha upande wa ushabiki.

Hapo sioni wapi Tundu kavuliwa nguo au Mbowe ndo ana dhihilisha uchwu wake wa madaraka, sidhani kama wajumbe wote watamuunga mukono hata kama atawapa Rushwa wale ni watu wazima kuna uwezekano pia Mbowe kupoteza uchaguzi, hapa naona ndo patamu kuona dimokurasia inavo fanya kazi sio ushabiki......atakae shindwa akubali matokeo tu.
Mkuu nchi inavituko sana hii, kwamba kuna wakongwe hata tafasiri ya uchaguzi hawajui.

Mtoa mada alivyogombea katika kura za maoni kupitia chama chake na kupata kura sijui 3 so Kwake ilikua amevuliwa nguo ? Mbona yupo na maisha yanaenda ,ajabu sana hii
 
Ni ujinga kumshauri asijibu. Kwenye siasa lazima ujibu kila hoja, usiache makombora uliorushiwa yakaaminika ni kweli. Jibu hoja zote kuondoa upotoshaji, huu ni muda wa kampeni.

Kama una taarifa ya team wenje na mgawo wao aliokusimulia weka orodha hadharani. Sultan amekuwa muovu wa muda mrefu anayejificha kwenye siasa
 
Ukiona hadi majizi ya CCM yanampa support mgombea wa chama chako rudi nyuma jitafakari.

Lissu hawezi kupata kura 1 kama wewe wajumbe walivyokunyoosha Kawe.

Hivi ile kura moja uliwahi kuijua ilikuwa ya nani?
 
Kwani kugombea Chadema ni ugomvi au ni lazima ushinde? akishindwa kama chama kinaona anafaa kitampa nafasi nyingine, ila TUNDU LISU huwa ni mkweli zaidi ya ukweli na Chadema inahitaji hao watu wawili ni muhimu sana.
 
Ebu pima Akili za washauri wa mbowe ni Akina wenje, Paskal, sugu na wenzao unategemea nini hapo ?
Hivi Paskal ni Mwanasheria au ni Mhitimu wa Sheria?? Napata ukakasi kwenye chambuzi zake na misimamo yake ya kuyumbayumba.
 
Hivi Paskal ni Mwanasheria au ni Mhitimu wa Sheria?? Napata ukakasi kwenye chambuzi zake na misimamo yake ya kuyumbayumba.
Tatizo Pasco haandiki kitu kukufurahisha wewe, yeye anafanya uchambuzi kwa maono yake.

Lisu hawezi kumshinda Mbowe na akishindwa uchaguzi atarudi kuwa mwanachama wa kawaida, kile kitengo cha sheria nadhani kinaongozwa na Kibatala kwa sasa.

Subilini muda ni mwalimu mzuri.
 
Shida ya mbowe ni moja uchoyo kugeuza pesa za chama kuwa pesa zake binafsi na sasa atazitumia kuchakachua uchunguzi na hata akishinda tena chadema itakuwa chama legelege hakuna mtu anapenda kuwa na kiongozi mchoyo mroho wa pesa za chama
Hata wewe funza umekigeuka chama chako?
 
Wenje kakosea sana kumtuma Paskal mayala awasemee, alipaswa ajue kuwa Watanzania wa sasa wameamka wanajua mapungufu ya Mbowe, Mayala na Wenje, hapo mmechemka nendeni mkae mtafakari kwanza ndipo mjue cha kuandika.
Mkuu Minyo, minyoo , mimi situmwi na mtu, hivyo sijatumwa na Wenje au na yeyote, mimi huwa najituma mwenyewe!.
P.
 
Back
Top Bottom