Pre GE2025 Baada ya Mchungaji Msigwa kuhamia CCM kutoka CHADEMA, unadhani kiongozi gani mwandamizi kufuata nyayo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii umeenda, chura kiziwi anakanyaga tu mafuta
 
Wanafuata Covid-19
 
Kinachokuvunja moyo ni kipi wakati mtu katumia uhuru wake kuchagua anachokitaka kwa sasa. Hajakosea chochote.

Siasa ni ajira mzee, huko chadema na ccm wenzio wananeemeka we endelea kuvunjika moyo, unadhani watu wanaingia kwenye siasa kunufaisha wengine tu? Masirahi yao kwanza mengine badae
 
Lakini si ukweli wanzinzibar wanafaidika na muungano kuliko wa Tanganyika(ambao wanelazimishwa kufa, maana mtu kujiita mzanzibar ni sawa ukianza kusema sisi watanganyika unaitwa mchochezi)
 
Lakini si ukweli wanzinzibar wanafaidika na muungano kuliko wa Tanganyika(ambao wanelazimishwa kufa, maana mtu kujiita mzanzibar ni sawa ukianza kusema sisi watanganyika unaitwa mchochezi)
Muungano upi wanaofaidika nao? Zanzibar ndio nchi pekee duniani ambayo wananchi wake wanalipa kodi mara mbili TRA na ZRA, halafu utashangaa hayo makusanyo ya TRA yanaenda kuwafadisha tanganyika tu kwenye mishahara yao na huduma zao za maendeleo zanzibar makusanyo ya TRA hawapati ata shilingi 1.

Ni vile tanganyika ili waishi waendelee kuinyonya zanzbar kupitia muungano., hakuna mzanzibar anaunga mkono huo unaoita muungano ukitoa hao walio kwenye mfumo ambao kuna maslahi yao binafsi
 
usimueleze ukweli sana maana ndio unamvunja moyo zaidi ujue, πŸ’
 
kuondoka kwa Mch. msigwa chadema kumeacha mwanya usiozibika chadema...

ameacha hofu, taharuki na sintofahamu kwa wengi kwenye chama hicho.

kuondoka kwake kunathibitisha yale yaliyokua yanakisiwa na kusemwa na wengi maeneo mbalimbali, kwamba ndani ya chadema hali si shwari..
kuna mwandamizi mwingine kumfuata msigwa wakati wowote...

ukiangalia body languages, facial expressions, tones za waadamizi kwenye mikutano yao, article zao kwenye social medias, utagundua na kusense anaefuata...

na kwamba, bundi bado anazengea zengea chadema. utaona yapo majonzi na huzuni ndani ya chadema japo yanafichwa kwa kujikaza kisabuni, uvumilivu na subra tu....

lakini kuweweseka bado ni kwingi ...

ukimgundua usimtaje
 
1 Yohana 2:19

[19]Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

They went out from us, but they were not of us; for if they had been of us, they would no doubt have continued with us: but they went out, that they might be made manifest that they were not all of us.
 
Msigwa alikuwa kiongozi wa CHADEMA wa kanda ya Nyasa kwa miaka kumi mfululizo, juzi wanaChadema wa kanda ya Nyasa wakamkataa kwa kura, akaona isiwe shida akaenda CCM. Hivyo CHADEMA haijapoteza kiongozi bali imepoteza mwanachama mwandamizi laghai.

Kisa cha Msigwa hakina tofauti kubwa sana na Sumaye, huyu alikuwa ni kiongozi wa Chadema kanda ya Pwani, akagombea uenyekiti wa Chadema akashindwa, akaenda kutetea nafasi ya kiongozi wa kanda ya Pwani nako akashindwa, kilichofuata akarejea CCM. Leo hii ni miaka mitano toka arejee CCM, kuna kipi ameweza kuisaidia CCM au kuweza kuibomoa CHADEMA? Sumaye leo hii ni kapi tu la kijani, wanaCCM hawawezi kumpa hata nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu kupitia nafasi za mikoa ikiwa atagombea sembuse ujumbe wa NEC. Leo hii Sumaye amebakia kuwa mtoa mawaidha ya kichawa ili kumpamba Samia. Useless kabisa!
 
chama ambacho kimejengwa kwenye misingi legelege kiitikadi, huweweseka na kubabaika sana panapotokea moja miongoni mwao kaamua kutumia haki yake ya msingi vinginevyo kadiri anavyoona inafaa kwa wakati huo πŸ’

ni vizuri kujipanga na kujiandaa kwa mabadiliko ndani ya vyama hakuna haja ya kubabaika na kupanic mwingine akitumia haki yake kikatiba atakavyo πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…