Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

swagazetu

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
4,250
Reaction score
1,470
Baada ya mdahalo uliokusanya Itv juu ya wananchi kujua nani anataka kuwazuia watanzania kupata katiba Mpya.

Je sasa unaweza kutoa jibu ulilopata?

Karibu....
 
ni wale ambao walisema hakuna haja ya katiba mpya(CCM);rejea matamko ya Celina Kombani wakati akiwa waziri (wa sheria),jaji Werema(jaji mkuu wa serikali) na sasa katibu mkuu wao.
 
Sio siri kuwa pamoja na kujitahidi sana walau kukabiliana na hoja za Prof Lipumba na mwanasheria nguli Tundu Lissu imeonekana dhahiri namna mzee Wasira alivyo pwaya kwenye kujibu na kukabiliana na hoja.

Ccm wamekuwa na utamaduni wa kukimbia midahalo. Je kwenye hili la leo wanajifunza nini?!
 
hao walioandaa rasimu ya katiba wasijifanye miungu watu taarifa zao tunazo walifyoahidiwa rasim yao ipite kwa nini wang'ang'anie yapite ya kwao ujinga mtupu
 
Ccm aibu tupu. Leo wameanikwa waaaaa uchi. Wakubali yaishe kwamba wananchi wameamua sio wao.
 
Ukianza kutegemea dola, polisi, nguvu, vitisho katika kuongoza nchi kwa kawaida ni kwamba uwezo wa kufikiri hupungua katika kiwango kilekile unachotumia nguvu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni wahafidhina wa Ccm wanaojiuliza nani atalinda
masilahi waliyoiba?Nani atakuwa Rais? atakayeongoza serikari atawalinda? Serikali ikishakuwa na wizara chache Wasira atakuwa waziri wa wizara ipi?
 
Back
Top Bottom