Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

Baada ya Mdahalo: Nani anazuia upatikanaji wa Katiba Mpya?

Kama kuna aliyeweza kurekodi tunaomba atuwekee hapa jamvini tafadhali.
 
Kwa kuwa serikali ilifunga tovuti ya tume ya Warioba ambako tungeweza kupata ufafanuzi wa jinsi walivyofikia uamuzi wa muundo wa serikali tatu,nashauri mwandaaji maarufu wa midahalo ya aina hii bibi Rosemary Mwakitwange,aandae mdahalo mwingine ambao wazungumzaji wakuu wawe wajumbe wa iliyokuwa tume ya Warioba ili watufafanulie masuala mbalimbali kuhusu rasimu ya pili ya katiba nasi tuwaulize maswali.Wanasiasa tumewasikia sana.
Katika mdahalo wa leo ITV,yule bwana mdogo Polepole amelalamika sana kupewa muda mfupi usioweza kutosha kufafanua mambo.
 
hao walioandaa rasimu ya katiba wasijifanye miungu watu taarifa zao tunazo walifyoahidiwa rasim yao ipite kwa nini wang'ang'anie yapite ya kwao ujinga mtupu

Lakini waliandika tulichopendekeza.
 
Kwa kuwa serikali ilifunga tovuti ya tume ya Warioba ambako tungeweza kupata ufafanuzi wa jinsi walivyofikia uamzi wa muundo wa serikali tatu,nashauri mwandaaji maaufu wa midahalo ya aina hii bibi Rosemary Mwakitwange,aandae mdahalo mwingine ambao wazungumzaji wakuu wawe wajumbe wa iliyokuwa tume ya Warioba ili watufafanulie masuala mbalimbali kuhusu rasimu ya pili ya katiba nasi tuwaulize maswali.Wanasiasa tumewasikia sana.
Katika mdahalo wa leo ITV,yule bwana mdogo Polepole amelalamika sana kupewa muda mfupi usioweza kutosha kufafanua mambo.

Ni kweli kaka.
 
Wassira amezomewa hadi nikamuonea huruma, alionekana dhahiri amepandwa na jazba...ila naamini amesoma mchezo na naamini ndicho alichofuata. Akawaambie wenzie kuwa wananchi wanataka nini na sio kutumia ubabe na wingi wao kupitisha wanachotaka kwa maslahi ya watu wachache.

Yote kwa yote Humphrey Polepole ni mfano wa kuigwa na vijana wote kwa maslahi ya Taifa hili.
 
Sio siri kuwa pamoja na kujitahidi sana walau kukabiliana na hoja za Prof Lipumba na mwanasheria nguli Tundu Lissu imeonekana dhahiri namna mzee Wasira alivyo pwaya kwenye kujibu na kukabiliana na hoja.

Ccm wamekuwa na utamaduni wa kukimbia midahalo. Je kwenye hili la leo wanajifunza nini?!

Aliezoewa vyakunyonga vya kuchinja haviwezi (ccm kazowea vya kunyonga halal haiwezi)

Aliezowea hoja za kulazimisha, nguvu za hoja huwa hana wala uwezo wa kuzijenga (ccm wamezowea kulazimisha)

Kukimbia kwao midahalo nikwasababu hoja nyingi kwa upande wa ccm zimekaa vibaya. CCM wanasifa zifutazo bila kuwasingizia.

-majangili

-mafisadi

-wabinafsi

-matapeli wa siasa

-hawasimamii wanayoyahubiri majukwaani nk

Hivyo hawana hoja zamashiko kujibu hoja za upande wapili, njia pekee ya kujiepusha na aibu

ni kukwepa mijadala wasiumbuke. (hawana la kujifunza maana ni sikio la kufa ..........halisikii dawa)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mchawi mkubwa ktk katiba mpya ni mafisadi na wezi wakubwa wa mali za umma walioko ccm.
 
Kwa kuwa serikali ilifunga tovuti ya tume ya Warioba ambako tungeweza kupata ufafanuzi wa jinsi walivyofikia uamuzi wa muundo wa serikali tatu,nashauri mwandaaji maarufu wa midahalo ya aina hii bibi Rosemary Mwakitwange,aandae mdahalo mwingine ambao wazungumzaji wakuu wawe wajumbe wa iliyokuwa tume ya Warioba ili watufafanulie masuala mbalimbali kuhusu rasimu ya pili ya katiba nasi tuwaulize maswali.Wanasiasa tumewasikia sana.
Katika mdahalo wa leo ITV,yule bwana mdogo Polepole amelalamika sana kupewa muda mfupi usioweza kutosha kufafanua mambo.

Aisee kama serekali ilifunga tovuti ya tume ya warioba basi nimepata jibu la kwanini hatuoni youtube video za BMK. Inasikitisha swala la maana namna hii haliwekwi kwenye mtandao kwa kila mtu kujionea kwamuda wake.
 
Nitumie jukwa hili kueleza kwa hakika namna ninavyomkubali kijana mzalendo POLEPOLE, kwenye mijadala mingi ambayo nimekuwa nikifuatilia nimeona namna anavyojenga hoja, hakika ana uwezo mkubwa wa kufafanua mambo anaeleza mambo kwa kina na hivyo amegeuka kuwa darasa kwa watanzania wengi walioukuwa hawaelewi mchakato mzima wa katiba mpya.
Anatumia kipawa chake na elimu yake ipasavyo kwa watanzania, hawa ndio vijana tunaowahitaji tanzania ya leo. Hatutaki vijana wabinafsi, waoga, na wasio simamia haki na ukweli kwa nchi yao.
kijana POLEPOLE usife moyo endelea mpaka katiba ipatikane yenye maslahi mapana kwa watanzania wote. MUNGU AKUBARIKI.
 
ukawa wameshindwa hoja kwenye mdahalo wao ndio kikwazo kikubwa

Towa sababu................kivipi?

Selina kombani ...........hakuna haja ya katiba mpya ....ccm

Fredriki welema............hakuna haja ya katiba mpya.....ccm

Chikawe......................hakuna haja ya katiba mpya.....ccm

kwanini tusiaamini kwamba ccm ndiyo kikwazo?
 
Back
Top Bottom