Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Oktoba 23, 2024, Mwanachama wa JamiiForums.com aliandika andiko la kuomba msaada wa wapi anapoweza kupata fedha au ufadhili kwa ndugu yake ambaye ni mgonjwa aliyelatwa katika Tasisi ya MOI, akisema kuwa gharama ya upasuaji Tsh Milioni 1.6 ni kubwa kwa familia yake ambayo imejichanga na kupata Tsh. Laki 3 tu.
Kumsoma Mdau bofya hapa: Msaada wa haraka wapendwa, mgonjwa wangu anahitaji Upasuaji MOI na familia haina fedha
Muda mfupi baada ya andiko hilo, Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) umemjibu Mdau huyo kwa kumpa maelekezo ya nini anatakiwa kukifanya.
Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi anazungumza
Akizungumza na JamiiForums kuhusu Mdau huyo, amesema "Tumeona kwenye mtandao wenu kuhusu mgojwa kuwa na changamoto ya kifedha, tunamuomba Mgonjwa au anayemuuguza afike Ofisi za Afisa Mahusiano MOI ili asikilizwe. Tutaangalia kama alifuata hatua zinazotakiwa kufuatwa kwa mgonjwa ambaye hana fedha ili aweze kusaidiwa.
“MOI ni Hospitali ya Serikali na ina utaratibu wa kuwa inawasaidia wagonjwa ambao hawana uwezo wa kifedha, Mkurugenzi huwa anatoa huo uthibitisho wa msamaha wa Wagonjwa hadi wale wa Shulingi Milioni 10.
“Kuna wagonjwa ambao hawana hata ndugu na tunawahudumia, sasa huyo ambaye ana ndugu kwa nini tusimuhudumie?
"Niwaombe tuendelee kuelimishana, fika Ofisi ya Ustawi wa Jamii au ukiona hujapata majibu ya kueleweka fika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji au Afisa Uhusiano utasaidiwa."