Baada ya miaka 15 mdogo wangu wa kike ndiyo kaniambia rafiki yake alijua nitamuoa

maandamano

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2025
Posts
726
Reaction score
1,548
Hii ni stori ndefu sana kipindi hicho nilikuwa naishi Mwanza nikifanya biashara ya mavazi nikinunua Dar kwenda kuuza Mwanza,na mdogo wangu wa kike alikuwa anasoma UDSM,mda mwingi nilikuwa nikimsaidia mahitaji madogomadogo si unajua tena mambo yaa chuo,nilikuwa kila nikienda namkuta na rafiki yake wa kike,kwa hiyo nikawa nawatoa out wote ingawa haikuwa mbali maeneo yaleyale ya chuo,nitawanunulia pilau,chips au soda,

Kiuhalisia tayali nilikuwa na mpenzi wangu Mwanza ambaye tulikuwa tunapendana sana,na yule rafiki wa mdogo wangu nilikuwa namuheshimu sana namchukulia kama mwana famili,nakumbuka kuna siku niliugua nikiwa Dar homa kali sana,nikampigia mdogo wangu akanielekeza niende Hospitali moja ambayo ilikuwa kalibu na chuoni kwao,ilibidi nilazwe na kipindi chote mdogo wangu alikuwa anakuja na rafiki yake
Sasa juzi kati katika kupiga stori nikamuulizia kuhusu rafiki yake,alichonijibu nilishanga kwamba walikuwa wanaitana Wifi na rafiki yake yaani alijuwa nitakuja kumuowa,imeshapita kalibu miaka 14 nasikia anamtoto mmoja hana mume anaishi peke yake,hii stori imenifikirisha sababu kipindi hicho chote mimi sikuwahi kumfikiria au kumuweka kichwani mwangu
 
Cha kusikitisha hatukuwahi kuongea naye wala kupiga naye stori zaidi ya kuniamkia shikamoo,mda mwingi nilikuwa napiga tu stori na mdogo wangu,yeye alikuwaga mda wote yuko kimya,nikitoka hapo naludi zangu Geust kesho safari na sikuwa kumuwazia chochote na hakuwa ndani ya akili yangu
 
Hii ni stori ndefu sana kipindi hicho nilikuwa naishi Mwanza nikifanya biashara ya mavazi nikinunua Dar kwenda kuuza Mwanza,na mdogo wangu wa kike alikuwa anasoma UDSM,mda mwingi nilikuwa nikimsaidia mahitaji madogomadogo si unajua tena mambo yaa chuo,nilikuwa kila nikienda namkuta na rafiki yake wa kike,kwa hiyo nikawa nawatoa out wote ingawa haikuwa mbali maeneo yaleyale ya chuo,nitawanunulia pilau,chips au soda,

Kiuhalisia tayali nilikuwa na mpenzi wangu Mwanza ambaye tulikuwa tunapendana sana,na yule rafiki wa mdogo wangu nilikuwa namuheshimu sana namchukulia kama mwana famili,nakumbuka kuna siku niliugua nikiwa Dar homa kali sana,nikampigia mdogo wangu akanielekeza niende Hospitali moja ambayo ilikuwa kalibu na chuoni kwao,ilibidi nilazwe na kipindi chote mdogo wangu alikuwa anakuja na rafiki yake
Sasa juzi kati katika kupiga stori nikamuulizia kuhusu rafiki yake,alichonijibu nilishanga kwamba walikuwa wanaitana Wifi na rafiki yake yaani alijuwa nitakuja kumuowa,imeshapita kalibu miaka 14 nasikia anamtoto mmoja hana mume anaishi peke yake,hii stori imenifikirisha sababu kipindi hicho chote mimi sikuwahi kumfikiria au kumuweka kichwani mwangu

Mdogo wako alikuwa anakuletea mchongo, ila wewe ulikuwa kaka bize umeletewa mpaka puani lakini hujala wala kunusa.
 
Unajua ulishawahi kuwa na yale maisha hujawahi kumuwaza au kumfikiria mtu,ingawa mala nyingi hii iko kwa wanaume,unakuwa unamfikilia mwanamke ambaye hana taimu na wewe kabisa,na ndivyo ilivyokuwa kwangu
 
Back
Top Bottom