Baada ya miaka 6 ndio nimeanza kusikiliza hotuba ya Rais tena

Hauko peke yako ndugu, ukisikiliza hotuba ya Mkuu wa Nchi unategemea kufarijika na kujenga matumaini mapya, lakini enzi za Kinjekitile ni kufokena na makasiriko tu, ya nini kujiongezea stress....
 
Mimi ata nikikutana na mtu kavaa nguo za ccm simchukii tena, hii tabia imekuja baada ya stone kufa na mama yetu kushika hatamu ya uongoz.
 
Mama alikua anamsikiliza sio kwa kumpenda bali kupata faraja jipya katika biashara zake zilizotegemea nchi ya kenya lakini kila hotuba ni nyundo tu tumaini lilikua likikung'utwa nyundo.

Sasa basi wakati akimsikiliza mimi earphone zangu mziki hadi mwisho kama haitoshi natoka zangu ndani njeeeee...

R.I.P Jiwe.
 
Ipo siku yataanikwa maovu ndipo wafuasi watastaajabu na kuachama kinywa
 
Soon utarudi huko kwenye kutosikiliza hasa ikizingatiwa kuwa wote ni wanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…