Baada ya miaka 60 ya uhuru tunakopa IMF kujenga Madarasa?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Ni mshangao mkubwa TZ baada ya miaka 60 tunakopa tena kwa riba fedha za kujenga madarasa ya shule Za sekondari.?

Kama Taifa tujiulize tumekosea wapi au tumelogwa na nani?

Nilitarajia mikopo iombwe kwa ajili ya miradi mikubwa mfano SGR .

Next year kuna uwezekano kuomba tena mkopo kutoka WB kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo kwa ajili ya shule za sekondari.

Bajeti ya Serikali Kuu 2021/22 ya maendeleo iko wapi na imeelekezwa kufanya shughuli zipi Za maendeleo?

Ni Muhimu kukopa ila kwa ajili ya miradi ya Kimkakati Ili ichangie ajira na pato la Taifa ila madarasa serikali ilikuwa na uwezo na sababu ya kuyajenga bila mikopo na riba.
 
Nchi gani ilihukumiwa na deni la IMF.
Hizo hela za IMF zipo nje nje ,zikipatiwa nafasi lazima tuziwekeze.
 
Sikiliza mkuu,mzungu alipotuvumbua,aliona hiyo ni fursa kwake Kwa miaka mingi.Na hata alipoamua kuacha kututawala moja Kwa moja,alijitengenezea utaratibu maalum utaendelea kutulazimisha kuendesha nchi zetu hizi,Kwa namna anavyotaka yeye.

Mkijifanya wababe,ndiyo kama Yale ya Zimbabwe,au kama Yale maisha nchi yetu iliyapitia miaka ya 80.Maisha ambayo ilikuwa ukikutwa na Colgate moja au sabuni Geisha unapata kesi.
 
Watakwambia ni nchi changa.Halafu watakwambia ..."tukitoka sisi CCM nani mbadala wetu"...?Utadhani Nyerere alipokabidhiwa nchi alikuwa mwenyekiti wa kijiji.Merde,CCM...Merde!
 
Kwani reli si ina miaka Zaid ya 60 ya Uhuru? Kwa NN yenyewe tunakopa kujenga SGR? Population ya wanafunzi wanaopaswa kujiunga na shule mwakan Ni Sawa na miaka 60 iliyopita? Ant SSH mnahangaika Sana Ila mmekwama mapema.Polen
 
mzungu hafai lazima atufanye tegemezi maisha yetu yote
 
IMF inakopesha kwa Masharti na hapa starti ni UVIKO 19, bora Serikali imepeleka Fedha kwenye Sekta ya Elimu na Afya, Je tungekopeshwa kisha tulazimishwe kutoa elimu na kununua Sanitizer au Barakoa si ndio ingekuwa Balaaa.
Think Twice.... KIDOMOKRASIHASA
 
Hoja ya kujiuluza ije wakati tumejenga hayo madarasa
 
Hapo hayajengwi madarasa wala nini, zitanunulia maviieite ili wezi wa kura wazidi kupandisha mabega
 
labda ndiyo masharti ya mkopo! Cha kujiuliza je tulikuwa na ulazima wa kuomba mkopo huo?
 
Ammaaa ya Musa wa Fimbo Firaun yu upenuni. Miaka 60 bado tunatengeza Wauza miogo na chapati, mandazi upenuni mwa barabara. Huku Traffic lights zikivamiwa na Wauza miogo na chaki feki za kichina.

Ila unadhani mimi na wewe tungekuwepo hapo kwenye hizo nafasi tungefanya tofauti?
 
Madini yote

Gesi

Mafuta

Bandari

Utalii

Na bado wameleta TOZO

NA Sasa wanakopa

Tatizo ni kuwa na serikali kubwa mno, na utitiri wa viongozi Bila kuleta tija. Posho, V8, mafuta, nyumba, etc
Basi hiyo serikali kubwa ijichapishie hela zake za matumizi na mishahara na hela za kodi zetu zibaki kujenga Nchi ya kisasa na maendeleo yanayoakisi hii miaka 60 ya uhuru umri wa mzee anayestaafu kwa lazima.
 
Hiyo rate ya kuongezeka uhitaji wa madarasa ambayo haiwezi kuwa taken care of na bajeti ya wizara hadi uhitaji kukopa pesa IMF ni jambo lisiloingia akilini, hii nchi ni kama imelaaniwa hivi......
 
uko sahihi lakini si vyote mkuu. Fikiria hata kujenga choo cha shimo hatuwezi kuchimba na kujenga mpaka tuombe msaada JICA au USAID???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…