Baada Ya Mo Dewj Kunyimwa Simba, Msimu Huu wa Simba Utakuwa mbaya kuliko yote

Kina Aveva na Kassim Dewji walitumia mamilioni ya pesa kupitia kwa Ndumbaru kuhakikisha wanaingia kwenye uongozi. Kamwe hawataachia uongozi SSC. Wanajua faida wanazopata bila kujali kabisa maendeleo ya timu. Muulize mwanasimba yeyote i wapi timu ya vijana ambayo ilikuwa tishio? Uwanja ambao uliweka matumaini kwa wanasimba kuwa kuna hatua itapigwa uko wapi? Wameshindwa kuuza kile kiwanja kwa kisingizio cha kupata fedha za kununua wachezaji. Kumbuka Aveva aliwahi kuuza gari la club kwa kisingizio kuwa alikuwa anatafuta pesa ya kumnunua mchezaji. Nasikia juzi baada ya wanachama wa SSC kutamka wazi wanamtaka MO kina Dewji na Aveva wamepeleka katapila kwenye uwanja wa Bunju eti wanatengeneza uwanja!!! Hili ni kanyaga boya. Subiri hili vugu vugu la MO lipite. Naamini ule uwanja wa Bunju utauzwa kabla hawa wapiga dili Aveva na Dewji hawajamaliza muda wao wa kikatiba.
 
Huwa tuna msimamo mmoja kwenye mambo Fulani, lakini huku umenitwanga hadi kizunguzungu. Pamoja na mapenzi kwa mnyama lakini kuna mengi kama yana gusa penyewe hivyo uungwana ngoja nichutame.
 
Mkuuu Sodoku usitake kutuharibia timu...haya mawazo yako mgando nenda kashauri kwenye timu yako ya JANGWANI...aka kafungwa kafungwa tena!
 
Kwani kikao tayari wamekaa, mi nashauri apewa Mo atasaidia
 
Ninavyojua Mimi uongozi umesema ni wazi wanachama wanataka mabadiliko hii ilitokana na wanachama kuanza kupiga kelele kuwa wanamtaka Mo baada ya Aveva na Azim kuanza kukwepesha kwepesha kama kwamba haiwezekani ndipo alipokatishwa kwa makelele ya wanachama hao hivyo basi kinachofata ni kamati tendaji kwa kushirikiana na wanacheria walifanyia kazi...
 
MO alishindwa Singida United,African Lyon ataiweza simba????
 
MO kama anamapenzi ya dhati na Simba amwage fedha pale kuisaidia timu msimu huu wa 2016/2017 na si anachotaka kufanya. Afadhiri timu isajiri,ijenge uwanja wake
Yaani awape pesa wakahonge michepuko Tu?
 
Mo anachukua team hutaki acha, na pesa ya kuendesha tram anatoa....wanachama tumelipitisha hilo kwenye mkutano, tunataka mabadiriko.
 
Jamani mwenye maazimio ya mkutano mkuu Juu ya hatma ya mo kuchukua timu atujuze ili tujue nasiii
 
Mo anachukua team hutaki acha, na pesa ya kuendesha tram anatoa....wanachama tumelipitisha hilo kwenye mkutano, tunataka mabadiriko.
Ndiyo ninanyo jua nashangaa huyu mleta mada sujui katoka wapi...
 
Nilitaman sana kuona kile kizazi kinachojibu hoja kwa hoja. nasikitika kumekuwa na kizazi ambacho wazaz wake wamepoteza muda mwingi kuwafunza watoto wao matusi kuliko hoja. Hili ni taifa la ajabu sana. Kila anayeweza kutumia JamiiForums kwa sasa anahikikisha kwanza amejifunza matusi kadiri awezavyo ili mwingine atakpokuwa na msimamo tofaut naye amtukane mpaka mtukanaji mdomo wake uwe kama choo. ni mioyo hiyo hiyo inayosukuma damu ndo inayozalisha matusi hayo?

Tunahitaj mabadiliko makubwa kwenye Elimu .
 
Umeona ukiongelea upumbavu wenu na huyo Mo Dewj wenu haitoshi hadi uitaje Yanga si ndio ???
 
Kwa hiyo timu apewe MO ili naye anunue mechi ?
Afadhali umemuuliza swali zuri. Watu wamekaa mchangani hadi akili zimepotea kabisa.
Umebaki ujinga mtupu. Wanamtaka anunue mechi kwa ufinyu wa akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…