Baada ya MO kutekwa, morali ya wachezaji Taifa Stars yashuka , kuchezea kichapo dhidi ya Cape Verde

Hapana Mkuu.
Kila mtu tunamsikitia anapofikwa na majanga.
Wakati wa Ben Saa Nane tulisikitika,
Wakati wa Akwilina tulisikitika pia.
Sasa hivi MO amepata majanga tunamsikitika.
Baadae atakuja mwingine kupata majanga tutamsikitikia huyo na kuwasahau waliopita.
Ndivyo tunavyoishi mkuu.
 
mbona mpira ulichezwa wkt MV Nyerere imezama walio kufa kule cio watu
 
Ben saa8 amewahi kulipa mishahara ya simba??
Au lisu amewahi kununua basi la team yoyote..?

Usitake binadamu wote tuwe sawa..kila mtu anathaminika kulingana na mchango wake kwenye jamii husika..

Mimi personally ben saa8 nimemjulia jf.

Lakini MO amemlipia scholarship jamaa yangu ambaye hio hela ya scholarship tunaitafuna wote..
Unategemea wakipotea wote ntamsikitikia nani??

Binadamu anathaminika kulingana na mchango wake..
Ndio maana hata mzazi wako akipotea na akipotea mzazi wa mwingine maumivu ni tofauti..

#watu hawawezi kufanana
 
Wewe ndio uache upuuzi..
Hata Mungu hakutuumba sawa.
Kuna watu hata kwenye biblia Mungu amewachagua tangu hawajazaliwa na kuna wengine amewalaani hata kabla hawajazaliwa.

Unaanzaje kusema Watu tuko sawa..

Akipotea baba yako na akipotea baba yangu utaumia sawa sawa??

Kila mtu anathaminiwa kulingana na mchango wake..ndio maana waziri mkuu hapangi foleni barabarani lakino wewe unapanga wakati wote ni binadamu
 
kwa hiyo MO akifa, na Simba imekufa!
 
Hivi unapata faida gani unapozusha uongo? Dewji pamoja na umaarufu wake wote, thamani yake haiwezi kuzidi utaifa wetu. Iacheni timu ya taifa ituwakilishe vyema huko iliko na suala la dewji iachieni jeshi la Polisi mbona wanalifanyia kazi. Mijitu imekaa kimya lakini mitandaoni inashinda kulaumu serikali wakati hata kulisaidia jeshi kukamata wahalifu hajafanya inakera sana.
 
Hahahaha hao wasitafute kisingizio yaani hiyo team Tangu atokage yule maximo sijawahi ona maajabu zaidi kila wakienda kucheza ni kuchezea kichapo naonaga hiyo hela TFF ingewalipa walimu tu sio kwa kuchezea upatu na hao wachezaje wenyewe mijitu mizima unaskia linadanganya nina miaka 23
 
Asilimia kubwa ya wachezaji wa Taifa Stars wanatokea Simba...hivyo ni wazi morali itaporomoka
 
Muda wa kahawa ukifika fanya unicheck
 
Taifa Stars inao wachezaji wa Simba ambao maisha yao yanategemea uwepo wa MO , hili unalijua vizuri tu ila umeamua kuleta siasa kwenye jukwaa la michezo , sijui kwa faida ya nani .
Kwa hiyo wewe hao waliotajwa hawajaajiri au?hata wao pia wana watu wanaowategemea
 
I didn't expect you to go this low!

Yani unamsikitikia Mo kwa sababu amenunua basi la Simba ila Ben Saa nane hakuweza? Like serious?

Kama mtu hatoi scholarships basi yeye anafaa kutekwa au kuuwawa sio?

Yani hapo ulipoongelea nduguyo kupewa scholarship na wewe ukaitumia hela yake ndio umeonyesha kwamba unasikitikia your economic interests na sio uhai au usalama wa Mo Dewji.

As a matter of fact, Tanzania ni yetu sote. Kila raia anayo haki ya kuishi kwa amani bila kujali hali yake kiuchumi, au mlengo wake kisiasa!

Humanity first, Bring back Mo Dewji.
# Justice for Ben Saa Nane
# Stay strong Tundu Lisu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…