John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Mara baada ya Simba kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, bao ambao lilizua utata kutokana na baadhi kuamini kabla ya tukio hilo kulitokea Meddie Kagere kuwa offside kisha Clatous Chama kufunga, kuna maoni mengi yalitolewa.
Sehemu ya maoni hayo yalitolewa pia na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mdau mkubwa wa Klabu ya Yanga, akidai kuwa ni vema sasa Tanzania tukaanza kutumia VAR.
Kauli hiyo ilizua mjadala mkubwa kwa wadau wengi, huyu hapa ni Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally naye ametoa tamko lake kuhusu matumizi ya VAR…
“Nimeona mjadala wa VAR 👏👏 ni wazo zuri naamini nia ni kuufanya mpira wa nchi hii uendelee kuwa bora zaidi.
“Lakini kwangu VAR sio tatizo la msingi la mpira wetu.
“Tatizo la msingi la mpira wetu ni sehemu ya kuchezea (PITCH).
“Tuna pitch mbovu sana nchi hii ukitoa Taifa, Azam Complex na Kaitaba, viwanja vingi vilivyosalia ni changamoto.
“Mpaka leo viwanja vyetu vinapakwa chokaa kabla ya mechi na baada ya muda chokaa inafutika uwanja unakua hauna mistari.
“Mvua zikinyesha kidogo tuu mpira hauchezeki.
“Mechi nyingi zinachezwa kwa kulazimishwa mfano mechi ya Mbeya City Vs Ruvu Shooting haikupaswa kuchezwa pale Sokoine.
“Ushauri wangu kabla ya ku invest kwenye VAR tungejikita kuboresha viwanja.
“Europe walianza kuboresha viwanja ndo wakaja kwenye VAR.
“Na kabla ya kufika kwenye VAR mamlaka husika waendelee kuboresha viwango vya waamuzi wetu wapate seminar za kutosha na wapate mechi kubwa za Afrika ili kuongeza uzoefu na kujiamini kwao.
“Tukishamaliza kuwekeza kwenye Pitch ndo tutakuja kwenye VAR.”