Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
S/N | MASWALI | MAJIBU |
| 1 | Mtoto wa umri gani analazimika kisheria kubaki na mama pale wazazi wanapotengana au kuachana? | Kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019 kifungu cha 26 (1) (a), (b) (c) na (2) inaeleza kwamba endapo wazazi watatengana mtoto atakuwa na haki ya kupata huduma zote za msingi kabla ya wazazi kutengana, kuishi na mzazi aliyeteuliwa na mahakama na anaruhusiwa kumtembelea mzazi mwingine bila kuathiri ratiba ya masomo, na mtoto chini ya miaka saba anatakiwa kuishi na mama yake kwa kuzingatia maslahi mapana ya mtoto kwa kuzingatia masharti ya sheria ya Ndoa Kifungu cha 125 (3). Aidha, Mahakama itazingatia maslahi mapana ya mtoto na umuhimu wa mtoto kulelewa na mama yake wakati wa kutoa amri ya matunzo ya mtoto kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) ya sheria ya mtoto. |
| 2 | Sheria inamlindaje mtoto wa nje ya ndoa kupata haki ya matunzo kutoka kwa baba au mama yake? (malazi, makazi na malezi) | Kwa mujibu wa kifungu cha 8 (1) (a-g) cha sheria ya mtoto, ni wajibu wa mzazi, mlezi au mtu yeyote mwenye jukumu la kutoa matunzo kwa mtoto kuhakikisha kuwa mtoto anapata haki zake za msingi zikiwemo chakula, Malazi, Mavazi, matibabu, elimu na ulinzi, uhuru na haki ya kucheza. Aidha, kifungu cha 43 (1) kinaeleza kuwa ombi la amri ya matunzo linaweza kufanywa dhidi ya anayedaiwa kuwa baba mzazi Mahakama kuhusiana na mtoto kuanzia kulea mimba hadi mtoto atakapozaliwa |
| 3 | Je, ni kweli baba wa mtoto ana hiari kutoa matunzo kwa kutamka kiwango anachotaka yeye au kuna sheria inayombana baba kuhakikisha anatoa matunzo ya kiasi fulani cha fedha kwa ustawi wa mtoto? | Kifungu cha 129 (1) cha Sheria ya Ndoa kinafafanua kuwa ni jukumu la mwanaume kutoa matunzo ya mtoto wake akiwa mikononi mwake au akiwa analelewa na mtu mwingine na kifungu cha 44 (c) cha sheria ya mtoto kinafafanua kuwa Mahakama itazingatia uwezo au kipato cha baba wakati wa kutoa amri ya matunzo. |
| 4 | Iwapo mtoto anaishi na Baba, Mama anawajibika kisheria kutoa matunzo ya mtoto kama ilivyo kwa baba? | Kifungu cha sheria ya Mtoto Na. 9(3) kinaeleza kuwa kila mzazi ana jukumu na wajibu kwa mtoto wake ambao unaweza kuwa umewekwa na sheria au laa unaojumuisha; Kumlinda dhidi ya Ukatili, kutelekezwa, Kubaguliwa, kunyanyaswa na kuepushwa katika hatari za kimwili na kihisia, kutoa mwongozo mzuri, malezi, matunzo, makuzi na kuhakikisha usalama na maendeleo ya mtoto. |
| 5 | Iwapo baba atakwepa kutoa matunzo kwa mtoto, ni njia gani za kufuata ili baba aweze kutimiza wajibu huu muhimu kwa ustawi wa watoto | Iwapo baba amekwepa jukumu la matunzo ya mtoto, mama anatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wa familia ikishindikana anatoa taarifa kwenye mamlaka ya Serikali za mitaa, Baraza la Kata au Ofisi za Ustawi wa Jamii na ikishindikana shauri litapelekwa Mahakamani kwa kuwa Mahakama ndio Chombo pekee kinachotoa Amri ya Matunzo kwa Watoto. |
| 6 | Je, kuna adhabu yoyote kisheria ambayo anaweza kuipata baba au mama kwa kukwepa kuwajibika kutunza mwanaye? | Kwa mujibu wa Sheria Kifungu cha 51 (b) mtu yeyote anayeshindwa kutoa mahitaji kwa maendeleo na makuzi ya mtoto yaliyoidhinishwa kisheria katika kifungu cha 41 na 46, atakuwa ametenda kosa kisheria ambalo litapelekea kutiwa hatiani na kutozwa fidia isiyopungua kiasi cha Shilingi za kitanzania 5,000,000/= au kwenda Jela kwa muda usiozidi miezi sita na sio zaidi ya miaka mitatu au vyote kwa pamoja. |
| 7 | Kwa baba au Mama anayekwepa jukumu kwa kukatisha mawasiliano na anakolelewa mtoto(kubadili na ya simu au kutopokea n.k) Nini kifanyike? | Hatua za kisheria zitafuatwa kwa kutoa taarifa Kituo cha Polisi na baadae akipatikana na hatia shauri litapelekwa Mahakamani. |
| 8 | Je, Ni kwa mazingira gani mtoto atapoteza haki ya matunzo kwa baba yake? (Wapo wababa wanaokataa kutoa matunzo kwa kigezo cha mama aliondoka na mtoto au ugomvi wao) | Mtoto atapoteza haki ya matunzo kwa baba yake iwapo itabainika kuwa si mtoto halali wa baba na kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto kifungu cha 47 atakosa matunzo pale ambapo atatimiza umri wa miaka 18, ameajiliwa kwa Malipo au atakapofariki kabla ya kufikisha umri miaka 18. |
| 9 | Kutokana na wimbi kubwa la wazazi kutelekeza malezi ya watoto hali inayopelekea watoto kukosa malezi, Hatua zipi zinachukuliwa kupambana na hali hiyo | Hatua zinazochukuliwa ni Pamoja na;
|
Pia soma:Baada ya Ndoa kuvunjika, sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto? Ni hiari au ni lazima Wazazi kutunza watoto?