Baada ya Ndoa kuvunjika, sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto? Ni hiari au ni lazima Wazazi kutunza watoto?

Baada ya Ndoa kuvunjika, sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto? Ni hiari au ni lazima Wazazi kutunza watoto?

goodhearted

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
978
Reaction score
1,237
Jamaa amezinguana na mkewe.

Mkewe kakimbilia kufungasha mizigo na vyombo vya ndani. Ameacha amefanya uharibifu kwa kuvunja simu ya msela kwa makusudi. Simu hiyo alinunuliwa na mme wake sasa wakati anaondoka mme alimtaka aiche (lengo mme akague kuona kama kuna ajenda iliyojificha yq yeye kuondoka)

Sasa mke kakimbilia ustawi wa jamii anataka matunzo ya mtoto. Mtoto ana miaka miwili.

Hii imekaaje, jamaa adai mwanae akae nae(uwezo wa kumlea anao) au ni lazima tu apeleke matuzo getoni
kwa mama wa mtoto alieamua kuondoka mwenyewe bila kufukuzwa wala kupigwa?

=======
1718795946007.png
Baada ya ndoa au mahusiano yaliyokuwa yamepata mtoto kuvunjika, imezoeleka mtoto au watoto mara nyingi walio chini ya miaka 7 hubaki au kuondoka na Mamama yao na kuanza maisha mapya. Kwa ndoa zinazovunjwa mahakamani hutolewa amri ya mahakama kuhusu uangalizi na matunzo ya watoto.

Haki ya kuishi na watoto hutegemea umri wa mtoto au watoto, uwezo wa kifedha wa kuwatunza na ustawi wa mtoto mwenyewe.

Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 7 hupaswa kuishi na mama kwaajili ya ustawi wake kama mtoto, lakini ni lazima ionekane wazi kuwa mama ana tabia njema na ustawi wa mtoto hautaathiriwa.

Mtoto mwenye miaka zaidi ya saba anaruhusiwa kuchagua kuishi na baba au mama. Baba atawajibika kutoa matunzo ya kifedha kadri ya uwezo/kipato chake kama mahakama itakavyoona inafaa.

Endapo mama ana tabia za ulevi uliopindukia, uchangudoa n.k mtoto au watoto wataishi kwa baba kwaajili ya ustawi bora wa watoto.

Hata hivyo, kwa mujibu wa RITA hali ya mtoto wa umri wa miaka 7 kuishi na mama inaweza kuwa tofauti kwa mujibu wa mabadiliko ya sheria ya mtoto ya mwaka 2009 kwa kipengele kichachosema "Best Interest of the Child" yaani maslahi Makuu au Muhimu ya mtoto ambapo best intrest ya mtoto inaweza kuwa tofauti na mama husika na hivyo kulelewa na mtu tofauti au mtu kutoka upande wa baba.
1718795415820.png
Pia soma:
 
Matunzo kwa shart moja,
Asiishi na mwanaume mwingine..

Nje ya Mada...
Njia gani nzuri ukillala usisikie kunguni wala mbu wakikung'ata?
Yaani ulale kwa starehe, usiwasikie.?
Jibu plz.
 
Matunzo kwa shart moja,
Asiishi na mwanaume mwingine..

Nje ya Mada...
Njia gani nzuri ukillala usisikia kunguni wala mbu wakikung'ata?
Yaani ulale kwa starehe, usiwasikie.?
Jibu plz.
Tumia smart Jinn au konyagi kila unapoenda kulala
 
Jamaa amezinguana na mkewe. Mkewe kakimbilia kufungasha mizigo na vyombo vya ndani. Ameacha amefanya uharibifu kwa kuvunja simu ya msela kwa maksudi. Simu hiyo alinunuliwa na mme wake sasa eakati anaondoka mme alimtaka aiche (lengo mme akague kuona kama kuna ajenda iliyojificha yq yeye kuondoka)

Sasa mke kakimbilia ustawi wa jamii anataka matunzo ya mtoto. Mtoto ana miaka miwili.

Hii imekaaje, jamaa adai mwanae akae nae(uwezo wa kumlea anao) au ni lazima tu apeleke matuzo getoni
kwa mama wa wa mtoto alieamua kuondoka mwenyewe bila kufukuzwa wala kupigwa
hoja je hiyo ndoa ilifungwa kwa madhehebu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ndoa ya kanisani? msikitini au ni ile ya sogea tukae?
je msimamo wa jamaa ni kuendelea na mke au la?
Je chanzo cha mke kuondoka ni nini?

Kama ndoa ni ya kanisani/ msikitini.
kama jamaa haitaji kuendelea na mke.

cha kufanya:
Akae kimya, mbali na mke na ipite miezi sita.
nenda mahakamani (kuna maelezo marefu hapa)
Kuondoka kwa mke ni sbb nzuri sana na tamu ya kuvunja ndoa.
kikubwa wawepo mashahidi hasa mjumbe, msicha wa kazi kama yupo au mwanafamilia wa kuja kuthibisha kuondoka kwa mke.

Kama jamaa ndio alisababisha mke kuondoka.
Mshauri kujishusha na kutafuta suruhu.
Hawa wana wake ni dada zetu, wake zetu, mama zetu.
Muhimu:Hali ya kutengana na kutalikiana, inakwenda mpaka uzao wako wa nne!
Hata walio tengana sasa, chunguza historia za wazazi wao
 
Walikubaliana tu kuishi baada ya mdada kubeba ujauzito. Huyo mdada amekutana na jamaa akiwa na watoto wawili wa jamaa mwingine ambae alimtelekeza so walikuwa kwa bibi yao mzaa mama
Tatizo lipo hapo kwenye nimeweka bold, usioe, kuzaa au kuishi na Mwanamke aliefika hio stage huyo ni wa kumla tu na kupitia kushoto, usijenge kiota ukasema umepata ukitaka Mwanamke tafuta damu changa ambae hajawahi kuzalishwa zaidi ya mara 1
 
Ni ndoa ya kanisani? msikitini au ni ile ya sogea tukae?
je msimamo wa jamaa ni kuendelea na mke au la?
Je chanzo cha mke kuondoka ni nini?

Kama ndoa ni ya kanisani/ msikitini.
kama jamaa haitaji kuendelea na mke.

cha kufanya:
Akae kimya, mbali na mke na ipite miezi sita.
nenda mahakamani (kuna maelezo marefu hapa)
Kuondoka kwa mke ni sbb nzuri sana na tamu ya kuvunja ndoa.
kikubwa wawepo mashahidi hasa mjumbe, msicha wa kazi kama yupo au mwanafamilia wa kuja kuthibisha kuondoka kwa mke.

Kama jamaa ndio alisababisha mke kuondoka.
Mshauri kujishusha na kutafuta suruhu.
Hawa wana wake ni dada zetu, wake zetu, mama zetu.
Muhimu:Hali ya kutengana na kutalikiana, inakwenda mpaka uzao wako wa nne!
Hata walio tengana sasa, chunguza historia za wazazi wao

Ni ile ya sogea tukae .Mwanamke hakufukuzwa hii inathibitishwa na mdogo wa mwanamke ambae alikuwepo siku ya tukio. Na pia anatibitisha kuwa alimwona akivunja simu kwa hasira mumuwe akimwomba asifanye hivyo bila mafanikio
 
Huyo jamaa mmeshibana sana yani kila kitu kuhusu ndoa yake unakijua[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni ile ya sogea tukae .Mwanamke hakufukuzwa hii inathibitishwa na mdogo wa mwanamke ambae alikuwepo siku ya tukio. Na pia anatibitisha kuwa alimwona akivunja simu kwa hasira mumuwe akimwomba asifanye hivyo bila mafanikio
HAKUNA MAHUSIANO HAPO.KILA MTU AENDELEE NA HAMSINI ZAKE.MTOTO ABAKI KWA MAMA, BABA AMCHUKUE MTOTO AKIFIKA UMRI AMBAO NI RAHIS KUJITETEA,KUJISIMAMIA,
 
Huyo jamaa hana kazi ya kufanya au?
Hapo hakuna cha ndoa wala mapenzi ya dhati. Hebu kuwa bize kutengeneza pesa HUYO NI FISI KALI.
 
Kama kaondoka mwenyewe hapo hakuna kesi,kajifukuzisha mwenyewe

Ova
 
Back
Top Bottom