Airmanula
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 3,527
- 5,762
daaaaah..
Sent using Jamii Forums mobile app
Oky Inaendelea..........
Baada ya kutoka pale chooni huku nikiwa kifuawazi na nimesha muona mama mwenye nyumba ananichora asee nilipandwa na hasira nilivuta sura moja ya kibandidu nikasogea mpaka pale mlangoni nikasimama nikamkata jicho lakini hakuonesha mshituko wowote yeye aliendelea kunitazama kwa macho makavu
Basi ikabidi ni ninyooshe mikono juu nikaingia ndani nikajifanya kufunga mlango kwa nguvu lakini nilikuwa bado naendelea kuzuga nikijua yule ni mwanamkee tu atarudi kulala kama mnavyojua kwenye milango mingi kwa juu huwa wanaachaga space wengine wanaweka hata nyavu ikabidi niweke stuli nipandishe kwa juu mdogo mdogo nichungulie kama mama mwenyewe nyumba atakuwa katoka pale mlangoni basi nikaweka stuli nikapanda taratibu sana nikatoa kichwa kidogo nichungulie.
Asee yule mama ni alqaida yani nimetoa jicho sehemu ndogo sana nikaona bado yupo halafu amenikazia jicho sehemu ile ile niliokuwa nachungulia daa nikasema sasa hii ngoma imekuwa ngumu nikakaa pale chini kwa muda kidogo nikaenda kumuangalia agustino nikahisi kama anaanza kutoa harufu daa hapo ndio nikachanganyikiwa nikainama uvunguni kulikuwa na neti inamatobo matobo nikatoa nikajaribu kutandika chini ili nione kama ninaweza uweka ule mwili nikaufunga nikautoa kama mzigo
Hapo hofu inazidi kuniingia niki imagine nimekaa na mtu hadi ameanza kuoza ghafla nilisikia kishindo kama mtu anakaribia mlangoni ikabidi nipande tena juu ya stuli kuchungulia daa namkuta bado yule mama yuko pale pale anachungulia nilizidi kuwaza pale bila kupata majibu ikabidi nibebe tena mwili niuweke juu ya ile neti nikajaribu kufunga mwili naona bado ni kazi bure maana ilikuwa haifuniki mwili vizuri
Nilichoka sana ikabidi nikae pale chini nikasema leo huyu mama amenizidi ujanja wakati huo nazidi kusikia harufu kali inazidi kutoka kwenye kile chumba yaani inatoka halafu inakata ikabidi niuache ule mwili pale chini nikapanda kitandani na viatu hata siku vua
Nilipiga usingizi kama masaa wawili baada ya hapo nikashituka kuangalia mwili unazidi toa harufu mbaya halafu chini kulikuwa na damu nyingi hadi zimetoka chini ya mlango nikasema leo ndio leo hii siku nikipona basi siwezi fanya ujinga tena.
Niliamka pale nikafungua mlango kuangaza huku na huku nikaona hali ni shwali basi nikatoka njee nikachota maji kwenye kidumu nikaweka kwenye ndoo nikavuruta ule mwili kwenda ndani zaidi nikapata space nikafuta zile damu fasta nikaenda mwaga maji kurudi ndani nikasema ngoja niangalie muda nikawasha simu ili niangalie muda yaani imeonesha muda tu ikazima ilikuwa kama saa 10 kasoro nikasema bado ninamuda naweza toa ule mwili ndani.
Basi nikarudi ndani nikajaribu kubeba ule mwili begani ikashindikana yaani ulikiwa mzito balaa nikasema ngoja niuburuze hadi kwenye kingazi cha mlango ili nipate sapoti ya kuunyanyua. Nikaanza kuuvuruta taratibu mlango nikauvuta wote mpaka mwisho nilivyo ufikisha pale kwenye ngazi nikapata balance ya kuubeba ile nimevimba ili ni ubebe ule mwili nilisikia nyuma yangu kishindo cha geti kama linafunguliwa ilibidi ni ruke kwa ndani halafu nikauvuta ule mwili fasta kurudi ndani
Kisha nikatoka nikakaa pale mlangoni lakini nilikaa pale kwa madakika kadhaa sikusikia tena kama mtu anatoka njee nikarudi ndani nikafunga mlango nikajitupa kitandani daa nikajua mambo yameharibika maana nilijua any time yule mama anaweza kunichoma hata kwa askari
Basi kulikucha bado agustino yuko mulemule getto halafu alikuwa ameanza kutoa harufu kama ya mzoga nikasema leo sitoki humu ndani maana unaweza toka mtu akaja kupanda pale kwa juu ya mlango kuchungulia. Pia yule mama hakuwahi hata siku moja kuniuliza eti agustino yuko wapi maana mimi pale nilikuwa sii mpangaji nilikuwa kama mgeni tu.
Basi nimekaa mule ndani naangalia ile maiti mpaka mapua yakazoea ile hewa ya mule nilikuwa nikitoka njee kwenda chooni nikirudi ndio naisikia vizuri .Nilikaa sana mule ndani nisijue la kufanya baada ya njaa kuzidi ndio nikasema ngoja nitoke niende kwa mpishi maana nilikuwa sina hata mia mbovu mfukoni basi nilichukua ule mwili nikaukanyaga kuusukuma uvungumi kisha nikafunga mlango nikasepa
Nilienda hadi shuleni kiukweli nilikuta watu wengi wamesharudi kutoka likizo nilizunguka hadi jikoni nikamfata mlinzi nikamwabia kama anamsosi wowote anisaidie akasema kuna uji msosi mpaka saa 9 hapo ilikuwa mida ya saa 7 akatoa uji kwenye kindoo akanipatia tukaanza kupiga nilitaka nimwabie ishi inayonisibu ila roho ilikata kabisa
Nikamwabia anisaidie ganja alikataa akasema hana basi tuliendelea kupiga story za hapa na pale nikisubiri msosi uive baada ya kazi kuwa nyingi nikaona anatoa kipisi cha bangi mfukoni na mimi akanipatia kimoja msosi ulivyokuwa tayari akapakuwa tukala hadi nikavembewa kisha nikasepa
Niliwahi haraka getto nisijue nini cha kufanya huku ile pisi ya bangi nikasema nitaivuta usiku halafu hata kama yule mama atatoa macho pale njee nitatoka na mwili anaagalia mzima mzima
Basi nikarudi nikakuta chumba kama nilivyokiacha lakini harufu ilizidi kuongezeka ikawa kali kinoma yaani kanakwamba mtu hata akipita dirishani lazima asikie
Yaani ilikuwa harufu kama mzoga wa paka aliyekufa unaona jinsi anavyo chafua mtaa , basi nilijifungia mlango sikutaka kelele na mtu yoyote ila nilikuwa na asilimia mia mchezo wote atakuwa amahusika yule mama kwa namna moja ama nyingine
Nilipiga usingizi kidogo nikiwa na hamu muda uzidi kusogea ili niweze kutoa ule mwili maana angelala tena pale ilikuwa mara ya tatu basi nilikuwa kama nimejiegesha mikaamka muda ulikuwa umeenda kidogo nikachukua simu jaribu kiwasha wapi nikatoa betri paka mate nikarudisha tena wapi sasa ikabidi nikadirie tu muda
Baada kama ya dakika arubini na tano kupita nikachukua ile ganja nikawasha nikapuliza wewe niasikia hadi kichwa kimekuwa kizito basi nikamaliza nikavaa viatu vizuri ,nikafungua mlango hadi mwisho toa ile maiti ndani wakati naivuta pale nikaona masikioni mdomoni na puani anatoa kama ute ute wala sikujali.
Sikuangaika kuangalia nani ananiangalia au nani haniangalii nikashika ile maiti kiunoni kumbuka alikuwa kifua wazi nikainyanyua kwa nguvu zote nikaipandisha hadi mabegani yaani utadhani ni leisner anataka kupiga mtu F5 kisha niaanza mwendo wakati huo sijapanga niwapi nitaenda kuitupa na nitaificha vipi.
Nikaanza kutembe sikuta nifate bara bara nikaingia kwenye njia za mkato nilitembea nikatembea nikatembea nikatembea wakati huo sina tochi nikahisi ule mwili unakuwa mzito nilivyo ingia ndani ndani kwenye vichaka nikasema hii hii ndio sehemu natupa huu mwili basi nikazidi kujongea ile nimefika naenda kutua asee kuangalia shingoni nilikuwa nimebeba mnyama wa ajabu kama nguruwe mwitu
Niliogopa sana nikaanza kukimbia kurudi getto nilikimbia ikafika mahala nikakaribia kufika getto kwa mbali nikaona kama watu wamejaa pale kwenye ile nyumba nikaanza kujiuliza au hii ishi mama mwenye nyumba ameita raia daa nikasema mungu saidia wasije wakawa wameingia kwenye kile chumba maana nilikuw nimekiacha wazi baada ya mzigo kunilemea.
Hazikupita hata dakika 5 kuangalia vizuri naona kimya hakuna watu basi nikaliunga taratibi hadi getto kufika nakuta mlango umefungwa kwa ndani ikabidi nianze kuusukuma kwa nguvu bila kuita mtu yoyote...
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app