Uchaguzi 2020 Baada ya Nyalandu kuongoza kura za awali kwa 100%, Je ni dalili za Nyalandu kupeperusha bendera ya CHADEMA? Je, Lissu atarudi kweli J3?

Uchaguzi 2020 Baada ya Nyalandu kuongoza kura za awali kwa 100%, Je ni dalili za Nyalandu kupeperusha bendera ya CHADEMA? Je, Lissu atarudi kweli J3?

Kiongozi huwa naheshimu michango yako, na naamini wewe sio mmoja wa walioamini Lowassa ataleta mabadiliko yoyote na haupo kwenye kundi la waliokuwa wakizungusha mikono. Amini nakwambia upeo wa watanzania wengi upo chini. Wanafata upepo tu, hata Mbowe ampitishe Nyalandu Kisha aungane na Membe kumsimamisha awe mgombea bado kuna nyomi kubwa litashangilia tu. Kuamini maneno yangu linganisha michango yako humu JF tu na wapuuzi wengine wasiotumia LOGIC michango yao ni mipasho tu. Mfano, sehemu zote humu ulipoulizwa humu JF Lissu asipopitishwa utafanyaje?, Jibu lako limekuwa uongozi wa CDM ndo utawajua vizuri. Wenzako wasiotumia akili wakiulizwa wanaanza matusi na kejeli, na kusisitiza tayari Lissu kashapitishwa. Meaning hawana plan B. Wakati mkifia chama na kuonyesha hisia zenu, kwa Mbowe na waliomzunguka ni picha tofauti. Wanaangalia maslahi zaidi. Jumatano jioni sio mbali,tutajua mbivu na mbichi.

Kimsingi mimi sio msemaji wa wafuasi wengine wa Cdm humu ndani, na ninakubali kutofautiana kimtazamo. Lakini sina shaka kwamba nje ya Lissu, baada ya uchaguzi huu, cdm itajikuta katika wakati mgumu. Ili cdm ibaki na nguvu yake, japo mazingira ya kidemokrasia sio rafiki, Lissu pekee ndio suluhisho. Huyo Nyalandu na Membe ni wanaccm wasaka fursa ndani ya upinzani. Sina chembe ya shaka na hili, hizo siasa za fursa kutoka kwa matapeli wa kisiasa tumeshazistukia.
 
Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.

Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Kuna uzembe unafanyika mahali au fitna dhidi ya lissu,nyalandu akishinda sipigi kura
 
Hivi hawa the so called wajumbe ni nani aliyewaroga?

Kwakweli nimeshangaa sana Tundu Lissu kuzidiwa kura ndani ya CHADEMA? Sio fair kabisa, Huyu Mbowe tuanze kumtazama kwa jicho la tatu.

Utashangaa siku ya kufika Lissu nchini yeye atakuwa zake na viongozi wa CCM kwenye msiba wa Rais Mkapa.
Tusubiri,kumsimamisha nyalandu ikifanikiwa itakuwa agenda ya mbowe kama wakati ule wa lowasa wakamwacha dr slaa,hakuna presidential material kama lissu ndani ya chadema
 
Tusubiri,kumsimamisha nyalandu ikifanikiwa itakuwa agenda ya mbowe kama wakati ule wa lowasa wakamwacha dr slaa,hakuna presidential material kama lissu ndani ya chadema
Ikithibitika kwamba ni kweli, itaonekana Mbowe anatumika na maccm
 
Ikithibitika kwamba ni kweli, itaonekana Mbowe anatumika na maccm
Haiwezekani 2015 wasimamishe lowasa aliyetoka ccm ,baada ya kuona watu watagundua mchezo membe akaenda ACT halafu sasa hivi wanakuja tena na Nyalandu?
Itakuwa ni kurudia makosa makusudi.
 
Nime screen shot hii msg yako wiki ijayo alhamisi nitakukumbusha, usije kukimbia kivuli chako. Kuna mengi msiyoyajua ingawa mmejawa na ushabiki mwingi. Watu Wana mikakati ya fedha sio ushabiki wa kufurahisha watu.
Watu wengi hawajui kama siasa ni vitega uchumi vya watu. Wanaamini watu wanapiga hizo show kuwatumikia wao. Ndio maana hilo somo unalotoa linadunda kueleweka.
Watu wamesahau kwanini Slaa aliyekuwa anauzika na mwenye uwezo wa kujiuza alitoswa akaingizwa Mzee mzima tena akiwa katika hali tete kiafya lakini ana fungu heavy.
 
Naona dalili ya wagombea wote wa ccm ili wagawe kura za upinzani!!jpm,membe na nyalandu!!Sasa cha kujiuliza Ajenda ya upinzani ni nini?kwa muelekeo huu Lisu hawezi teuliwa kuwa mgombea!!!Hata lema anamtisha lisu kuja nchini!!!
 
Nawakumbusha chaguo la nyerere mkapa kaenda waliobaki sio chaguo la nyerere hata mwinyi sio chaguo lake!!jpm ni chotara wa mkapa!!ngoja tuone mwelekeo mpya wa tanzania bila nasaba za nyerere katika uongozi!!
 
Michezo ya kisiasa ni migumu sana,Mara nyingi wanaoumia Physically and Psychology ni wanachama wa kawaida na mashabiki.

Siipendi siasa lakini ndiyo inaamua maisha yetu, Mkapa na Kikwete walimuweka Magufuli tunaoteseka ni sisi wananchi huku mtaani.

Ukiona CHADEMA wamempitisha Nyallandu basi more than 70% mgombea wa Upinzani ni Membe. Binafsi simkubali Lissu kwa sababu tofauti yake na Magufuli ni ndogo sana lakini kiukweli ndiye mgombea anayeweza kumtingisha Magufuli au kumtoa madarakani kabisa na CCM wanalijua hilo. Na wakimuibia kura zake nchi itawaka moto.
 
Maajabu ya Dunia ccm kufurahia demokrasia ya Chadema. Wakati mlishindwa hata kuwakaribisha kwenye ufunguzi wa jengo ya NEC , Uchaguzi house pale Dodoma
Wakafanye nini, wangelienda tu na hakuna wa kuwarudisha.
 
CCM endeleeni kumalizia malizia vyakula vya ikulu kwa sababu sasa ni dhahili kuwa mnamuogopa Lissu kuliko Kifo na njaa.
Ila niwaambie jambo, Chadema sio wajinga, wanajua akili zenu, wanajua mawazo yenu. Majibu ya mnachokifurahia leo mnaenda kuyapata hapo Jumatatu Lissu anavoenda kutua nchini na Tarehe 28 kwenye mkutano mkuu wa Chadema
Haha. Ataenda kusalimiana na Magufuli tu.
 
Uko sahihi sana kwa usemalo, ni kweli Mbowe alifanikiwa kumuweka Lowassa na watu walitii. Na hata sasa atamuweka anayemtaka, ila sio kila siku ni Ijumaa. Safari hii akikosea shabaha, ndio atajua sisi wapiga kura ndio wenye maamuzi ya kura. Tusiandikie mate, maana umekuja kwa mihemko kama mwanamke aliyemfumania mumewe na house girl.
Tulia wewe utumiwe na DJ kukumwingizia pesa. Wachagga tumetumwa hela Mjini, maendeleo yanafanywa na Magu. Sasa nyie nyumbu subirini kutumika kama desturi yenu
 
Back
Top Bottom