Uchaguzi 2020 Baada ya Nyalandu kuongoza kura za awali kwa 100%, Je ni dalili za Nyalandu kupeperusha bendera ya CHADEMA? Je, Lissu atarudi kweli J3?

Uchaguzi 2020 Baada ya Nyalandu kuongoza kura za awali kwa 100%, Je ni dalili za Nyalandu kupeperusha bendera ya CHADEMA? Je, Lissu atarudi kweli J3?

With all due respect, mkuu nikuulize ikitokea Lisu apate vikwazo vya kugombea then chadema ndio basi tena? Kingine nini maana ya demokrasia? Huwezi kulazimisha kitu hiyo sio demokrasia. Kingine Nyalandu deserves respect. Huyu alijivua ubunge na kuja chadema pasipo ku demand chochote. Very unfair ukimwita mwa ccm na uki doubt uaminifu wake.

90% ya waliorudi ccm ni wale waliotoka ccm. Sio kwamba walifukuzwa, bali walikosa nafasi huko ccm, wakaona wajitoe kuja cdm. Nyalandu hana record nzuri ya utendaji toka ccm, hivyo akiwa mgombea wa Cdm huku dola ikijua madhambi yake, ni rahisi kumbana mpaka asalimu amri kama Lowassa na Sumaye. Narudia tena, ni nadra sana mwanaccm yoyote, tena aliye na record yenye makandokando kuacha uanaccm wake, ccm ikiwa madarakani, regardless kaondokaje ccm.

Hilo la Lissu kuwekewa vikwazo kutokana na kesi za kubambikiwa tunalifahamu vizuri sana. Lakini sio kigezo cha kuwa na mtu ambaye tuna mashaka naye ya dhahiri, na mifano ya watu wa ccm kama yeye ipo wazi. Hiyo demokrasia unayosema nataka kulazimisha, ndio demokrasia hiyo hiyo hutaki mimi niitumie kumkataa mtu. Sina popote nimewashikia watu bunduki wamkatae Nyalandu, bali nashawishi na sababu naziweka wazi.
 
Ila tu tukumbule hata Dr. Slaa alitoka CCM!!!
Kuna funzo hapo!!

Ni kweli kabisa, hata Maalim Seif. Lakini nyakati zilikuwa zipi? Ni muda gani walikaa upinzani mpaka kupewa nafasi ya kugombea urais? Nyakati zao kulikuwa na hizi siasa za kuacha nafasi ya ubunge, na kwenda kurudishiwa nafasi hiyohiyo kwa chaguzi za kihuni? Kulikuwa na siasa hizi za kuhama na kuanza kufanyiziwa ili kukung'ong'onyeza hatimaye ulegee? Nyalandu sio mtu imara wa siasa za kukomoana za ccm fullstop.
 
Wakuu hili suala la Lissu na Mwenyekiti kwa maono ya kawaida ni suala dogo sana lakini KISIASA na KIUTAWALA WA VYAMA sio suala jepesi hivyo.

KISIASA: Mashambulizi makali ya CCM kuelekeza Chadema yametokana na siasa ambazo Lissu amekuwa akiendesha kumwelekezea Mkulu na hata uhoi wa Chadema leo ni Mchango hasi wa Mh. Lissu kichama.

Tukitaka Chadema ipotee kwenye ramani ya siasa za uwakilishi ni turuhusu Mh Lissu agombee Urais na ashindwe. Kwa mfumo wa siasa zake ushiriki wake utaacha donda ambalo kama atashindwa CCM basi watahakikisha watafanya kila wawezalo wafute Siasa za uwakilishi za Chadema Tanzania.

Kwa hali ya Chama ilivyo leo tunatakiwa kukubaliana kuwa gonjwa zito limeipitia Chadema na lazima tujipe muda wa kutosha kuponya maumivu. Kwa upande huo Yeyote mwenye siasa za kupoa ili tuweze kuponya majeraha anaweza kuwa wa msaada sana kwetu.

KIUTAWALA WA VYAMA: Chama chochote kizuri huendeshwa kwa vikao, na vikao hutoa nafasi ya kila mjumbe atoe hoja na nyongo. Na katika vikao watu wa aina mbili huangaliwa sana.

1) Wajumbe ambao michango yao katika mijadala hubalisha mwelekeo na muono kichama.

2) Wajumbe ambao wanaushawishi mkubwa na huvutia wajumbe katika kupiga kura za maamuzi hata kama maamuzi hayo ni magumu kuyatekeleza.

Sasa kitu ambacho hatujui LISSU yuko kwenye upande gani kuhukumiwa, ila tusione maamuzi ya Chama ni mapesi ya ama kumuunga mkono Nyalandu, au LISSU kwa uchaguzi huu wa 2020. NAWAKILISHA
 
Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.

Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Kwani Nyalandu siyo mwana- Chadema? Mbona mnambagua?
 
CDM nayo ina wenyewe.

Hawa Ghost supporters wa Lisu mitandaoni hata kadi tu ya CDM hawana.

Kama mnampenda sana jamaa yenu anzisheni chama chenu mumteue agombee.

Nyie subirini kuzungusha mikono na kudeki kwa yeyote mtakayeletewa na Kamati Kuu,hamtaki mnahama.

Mbowe alimwambia Slaa,"Time and tides wait for nobody".
 
Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.

Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Lowasa alifanya kosa gani? Nyinyi hamna shukurani zile kura milioni sota alizowapatia pamoja na wabunge kibao na ruzuku kede kede sasa subiri uchaguzi huu uone idadi ta kura na wabunge mtakaopata alau ndio utakumbuka umuhimu wa Loawasa kwenu.
 
Lissu tumemshauri Sana apumzike Kwanza mpaka akae vyema kiafya,kifedha na kiakili lkn inaonesha kapania Sana sasa mwacheni akatishwe tamaa ndani ya chama kwanza. Mbowe gambler anajua chadema haitakiwi kupoteza pesa ya kampeni urais wakati magu keshashinda!! Happy anamtanguliza Nyalandu napesa zake alizochumia Ccm... mnyiramba anajiona plesdent matirio mwacheni akapate kuratatu mzuka akisanuka amwachie tuu Membe wampiganie woote
 
Lowasa alifanya kosa gani? Nyinyi hamna shukurani zile kura milioni sota alizowapatia pamoja na wabunge kibao na ruzuku kede kede sasa subiri uchaguzi huu uone idadi ta kura na wabunge mtakaopata alau ndio utakumbuka umuhimu wa Loawasa kwenu.

Cdm haikuwa na tatizo la wapiga kura, usitake kumpa sifa asizostahili. Watu tulijiandikisha kwa hasira tukijua Lowasa angekuwa mgombea wa ccm, ila viongozi wa Cdm wakampa Lowassa nafasi baada ya kupigwa chini huko ccm. Kama Lowassa ndio alileta kura 6m+ akiwa na miezi miwili, sema alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili? Au hata alifungua matawi mangapi ya cdm?

Hizo kura 6m angezipeleka TLP tungekuelewa. Ni kweli safari hii cdm wanaweza wasipate hata jimbo moja, ila sio kwakuwa haina wapiga kura, bali ni kwakuwa Magufuli kwa kutumia madaraka yake vibaya, ataagizwa watoa rushwa wa ccm kutangazwa washindi na tume isiyo huru ya uchaguzi.
 
Nikisema sisi, ni mimi na mke wangu.
Unamwamini je mkeo wakati kura ni Siri?

Kwani hujui mkeo anachepuka na jamaa wa Kanisani kwenu? .. basi usimwamini hata kwenye Kura.
 
Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.

Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Mkuu Tindo, ninaunga mkono maono yako, umefika wakati sisi wapiga kura ama wanachama wa kawaida tuheshimike tusikilizwe. Mimi sio mwanachama wa CDM, tunahitaji upinzani imara wenye muelekeo, bila upinzani serekali itapata mteremko wa kutenda wayatakayo, upinzani is the check and balance ya serekali. Ni vizuri mkawa makini, pesa anazozileta Nyalandu ni za group fulani wanaoitafuta Tanzania kwa udi na uvumba, na wanahusiana na taasisi moja inayojulikana kwa kutaka kuzikomoa African countries
 
Wanajitia wana demokrasia chamani kwao wakati walitayarisha fom moja tu ya kugombea[emoji23][emoji23][emoji23]
Maajabu ya Dunia ccm kufurahia demokrasia ya Chadema. Wakati mlishindwa hata kuwakaribisha kwenye ufunguzi wa jengo ya NEC , Uchaguzi house pale Dodoma
 
Back
Top Bottom