Baada ya Oktoba 29, 2025. Tulikosea je, tunaweza pia kusema tuwajibike?

Baada ya Oktoba 29, 2025. Tulikosea je, tunaweza pia kusema tuwajibike?

teknoubongo

New Member
Joined
Sep 23, 2026
Posts
2
Reaction score
2
BAADA YA OCT 29, 2025 “TULIKOSEA”JE, TUNAWEZA PIA KUSEMA “TUWAJIBIKE”

OKTOBA 29, 2025 2025 ni siku ambayo WaTanzania(Bara) inabidi kuungana katika kuyatafakari yaliyotokea kwa pamoja. Lakini baada ya matukio ya Oktoba 29, suala la uwajibikaji linahitaji zaidi ya kukiri kwa ujumla kwamba “tumekosea.”

Linahitaji viongozi wa kisiasa , watendaji wa serikali na watu binafsi :-
  • Kutafakari na Tathmini kwa ukweli ,
  • Kuona kiuhalisia
  • Kisha kueleza ni wapi (tu)likosea,
  • Kuwajibika
Baadhi ya mambo mawili makuu kwenye tafakari na tathmini tunayoweza kujikita kwa kuangalia na kudadavua ni maamuzi gani yalifanyika na kwa nini?

Tunakaribia Mwanka sasa tangu OKTOBA 29, 2025 2025 . Tumerudi katika maisha ya kawaida au si ya kawaida( Inategema na mtazamo au muktadha ), mijadala ya kisiasa inaendelea na mara nyingi kila pande kukumbusha au kusisitiza upande mwingine ndio wenye makosa

Mara nyingi mwanasiasa aliyeupande tusiokubaliana na mtazamo au sera zake akifanya kosa, tunataka awajibishwe. Lakini mtu tunayemuunga mkono akifanya kosa, ghafla tunaanza kutafuta mazingira ya kumtetea. Nimeleta mada hii ili watu wa jamii intelligence tujikite kwenye Hoja

Wakati siasa ndio zao la viongozi wetu wanaofanya maamuzi ya masingi kwa niaba yetu wanacnhi lakini binasfi naona zaidi ya wanasiasa kuna maswali na majibu ya “matukio” ya October 29 na mambo mengine ya msingi yanabidi yatolewe majibu kitalaamu na wataalamu walioaminiwa na kuteuliwa na wanasiana kuongoza taasisi fulani nyeti ambazo watendaji wao kwa nafasi zao binafsi wana maswali ya kujibu kwa mambo yaliyotokea . Vile vile wanachi wanataka kujua walifanya au hawakufanya nini.

Kifupi Baada ya yale yaliyotokea Tanzania(Bara) tangu Oktoba 29, jamii ( Viongozi/Watendaji/ Wananchi) inapaswa kujifunza kufanya mambo tofauti na kwa weledi.

Umma una haki ya kuuliza maswali

Mfano WaTanzania(Bara) wana haki ya kuwauliza viongozi waliokuwa wakifanya maamuzi kwa niaba yao:
Katika matukio ya vifo vilivyoripotiwa, ni nani aliyefyatua risasi, katika mazingira gani, kwa amri ya nani, na kwa mujibu wa mamlaka gani ya kisheria??

Ikiwa matumizi ya nguvu yalikuwa ya kisheria, ni ushahidi gani unaonyesha hivyo? Ikiwa hayakuwa ya kisheria, ni nani aliyewajibika kwa uamuzi huo na nani aliyetekeleza

Je kulikuwa na taarifa na tahadhari zilizokuwa zimetolewa kabla ya matukio?

Majibu ya maswali haya si kwa ajili ya kulipiza kisasi. Ni maswali ambayo majibu yake ni muhimu kwa watu wanaotaka kujua kama wanaweza kuishi kwa usalama mfano baada ya changuzi za kisiasa zijazo au hata kuishi na usalama hata kama watu hawakubaliani kisiasa na wana maoni ambayo hayaupendezi upande fulani

Uwajibikaji unahitaji maelezo

Viongozi wa kisiasa na kiusalama wanapaswa kuwa tayari kueleza taarifa walizokuwa nazo na maamuzi waliyofanya.

Kukubali kuwajibika hakupaswi kuishia katika kusema, “Tulishindwa wote.” Kunapaswa kuwe na maelezo:

Ni nini kilikwenda vibaya?

Ni maamuzi gani yalifanyika chini ya mamlaka ya kiongozi husika?

Ni hatua gani ( Kisheria, kiutendaji, kimifumo , etc ) zitachukuliwa ili kosa hilo lisijirudie?


Umma una haki ya kusikia maelezo hayo na kisha kuamua kama maelezo yaliyotolewa yanatosheleza.

Kuna hatari pia ya kutoa majibu ya ujumla sana kwamba “sote tulishindwa.” Kauli kama hiyo inaweza kuficha tofauti za viwango vya uwajibikaji.

Uwajibikaji wa kiongozi/mtendaji mkuu wa serikali au watendaji wa vyombo vya usalama hauwezi kuwa sawa na uwajibikaji wa raia aliyewaamini viongozi hao. Familia zilizopoteza watu/ mali zina haki ya kupata majibu kutoka kwa wale waliokuwa wamepewa dhamana ya kuwalinda.

Lakini uwajibikaji hauishii kwa viongozi

Lakini pia Kunaa suala gumu zaidi: kila mmoja tujiulize kuhusu uwajibkaji wako/wetu mwenyewe kama raia mmmoja mmoja nje ya muktadha wa kisiasa
  • Je, tuliwahi kusambaza taarifa kwa sababu tu ilikubaliana na tunachoamini, bila kwanza kuhakikisha kama ni kweli?
  • Je, tuliwahi kumsamehe au kumtetea mtu kwa sababu tu alikuwa upande wetu wa kisiasa?
  • Je, tuliwahi kumshutumu mtu bila ushahidi wa kutosha?
Kama tulisambaza taarifa ya uongo ,kutoa ushuhuda wa uongo na mambo yanayoendana na hayo basi tulipaswa au tunapaswa kuwa tayari kurekebisha taarifa hiyo(zo) au ushuhuda huo kwenye platform hizo hizo tulikofanyia maovu hayo iwe ni kwa kujua au kutokujua au kushinikizwa

Kama tulimshutumu mtu bila haki, tunapaswa kuwa tayari “kuwaambia” wale waliosikia shutuma hizo kwamba tulikosea.

Tendo mojawapo la “kuwaambia” wananchi ni kuondoa shutuma zisizo na ukweli wala tija zilizoko kwenye vyombo mbali mbali vya kimamlaka

“Ni(tu)mekosea” si udhaifu

Kukiri kosa si lazima kumaanishe kwamba kila kitu ulichofanya kilikuwa kibaya.

Inaweza kumaanisha tu kwamba uliamini taarifa isiyo sahihi, ulimwamini mtu ambaye hakustahili kuaminiwa, hukuliona tatizo mapema, au uliendelea kutetea uamuzi kwa muda mrefu kuliko ulivyopaswa.

Tatizo kubwa huanza pale jamii inapofanya kukiri kosa kuwa jambo lisilokubalika kisiasa/ kiutendaji au kimfumo. Sababu kwenye siasa kukwepa uwajibikaji ni jambo la kawaida au linalukubaliko inabidi tutambue OCT 29 ni beyond siasa. Kwenye utaalamu , taaluma na weledi wa majukumu kwenye sekta mbali mbali UWAJIBIKAJI ni jambo la msingi

Kiongozi anayekiri kosa anaweza kuogopa kwamba maneno yake yatatumika dhidi yake katika kampeni ijayo (Siasa) . Ni Sababu hiyo watu wanaweza kuficha makosa badala ya kuyakabili. Au kwa maslahi binafsi au ya kisiasa kuwashawishi kuwaeleleza “watendaji” au “wataalmu” wao kufumbia macho weledi katika kutekeleza majukumu yao

Jamii yenye afya ya majadiliano ( Kukubali kutokubaliana bila kuumizana) inapaswa kuwa na nafasi ya n “wahusika wakuu: kueleza tathmini zao,, kusikilizwa, na kisha wananchi au mifumo ya kisheria kufanya tathmini na maamuzi kwa HAKI

Somo pana zaidi kwa Tanzania

wananchi wanapaswa kupata majibu gani kutoka kwa wale waliokuwa na dhamana ya kufanya maamuzi?


Tume ya kwanza ya Tanzania ilichunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi. Mwenyekiti wake, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, alisema tume ilikusanya ushahidi kutoka kwa watu 63,603 na kwamba ripoti ilieleza kilichotokea, ilichokibaini na mapendekezo yake.

Hata hivyo, mjadala au mada ya uwajibikaji inasemekana haikuwa katika hadidu rejea za tume ya Kwanza . Tume nyingine ( No2) ilianzishwa kuchunguza wahusika na ukiukaji wa sheria wakati na baada ya uchaguzi.


TUME YA PILI TUNATARAJIA KUJA NA MAJIBU GANI?
Kwa kuwa Tume ya pili imepewa jukumu la kuchunguza wahusika na ukiukaji wa sheria wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, matarajio ya wananchi si kupata simulizi nyingine tu ya matukio yaliyotokea.

Wananchi wanahitaji kuona hatua inayofuata ya uchunguzi: uwajibikaji wa mtu binafsi, wa kiutendaji, wa kitaasisi na wa kimfumo.

Kwa mfano ripoti ya Tume no2 inatarajiwa kusaidia kujibu maswali yafuatayo:

1. Kuhusu vifo
  • Ni watu gani walifariki?
  • Walifariki wapi, lini na katika mazingira gani?
  • Chanzo cha kila kifo kilikuwa nini kwa mujibu wa ushahidi wa kitabibu na uchunguzi?
  • Katika matukio yaliyohusisha risasi, ni aina gani ya silaha iliyotumika na ni nani aliyekuwa akiimiliki au kuitumia?
  • Je, matumizi ya nguvu yalikuwa ya lazima, sawia na halali kwa mujibu wa sheria?
  • Ikiwa matumizi ya nguvu hayakuwa halali, ni nani anayewajibika kwa uamuzi huo?

2. Kuhusu amri na mlolongo wa mamlaka

  • Ni nani aliyekuwa na mamlaka ya kutoa amri katika kila eneo?
  • Ni maagizo gani yalitolewa kabla na wakati wa machafuko?
  • Je, maagizo hayo yaliandikwa, yalitolewa kwa mdomo au kupitia njia nyingine?
  • Ni nani aliyepokea maagizo hayo?
  • Je, waliotekeleza maagizo walikuwa na sababu ya kuamini kwamba yalikuwa halali?
  • Ikiwa kulikuwa na amri isiyo halali, ni nani aliyeitoa na nani alipaswa kuizuia?

3. Kuhusu taarifa za awali
  • Je, taasisi za usalama zilikuwa na taarifa kwamba vurugu zinaweza kutokea?
  • Ikiwa zilikuwa nazo, taarifa hizo zilifikishwa kwa nani?
  • Ni hatua gani zilichukuliwa kutokana na taarifa hizo?
  • Ikiwa taarifa zilikuwepo lakini hazikufanyiwa kazi, kwa nini?

4. Kuhusu matumizi ya nguvu
Tume inatarajiwa kutenganisha matumizi mbalimbali ya nguvu: maandamano, uporaji, uharibifu wa mali, kushambulia watu, matumizi ya silaha na matukio mengine.

Si kila mtu aliyekuwa katika eneo la tukio anaweza kuchukuliwa kuwa na jukumu sawa.

Kwa hiyo, Tume inapaswa kutofautisha kati ya:
  • waandaaji;
  • wachochezi;
  • waliotekeleza vitendo vya uhalifu;
  • waliotoa fedha au vifaa;
  • waliotoa amri;
  • waliotekeleza amri;
  • waliotakiwa kuzuia uhalifu lakini hawakuchukua hatua;
  • na wananchi waliokuwepo bila kushiriki katika uhalifu.
5. Kuhusu uporaji na uharibifu wa mali
  • Ni nani aliyepora au kuharibu mali?
  • Je, vitendo hivyo vilikuwa vya mtu binafsi au kulikuwa na uratibu?
  • Je, kulikuwa na watu waliotoa fedha, usafiri, vifaa au maelekezo kwa ajili ya vitendo hivyo?
  • Ni hatua gani za kisheria zimechukuliwa?

6. Kuhusu watu waliopotea au kutoweka
  • Ni watu wangapi waliripotiwa kupotea?
  • Ni wangapi wamepatikana?
  • Ni nani bado hajulikani alipo?
  • Kwa kila kesi ambayo ushahidi unaonyesha uwezekano wa kutekwa, kuzuiliwa au kuuawa, uchunguzi wa mtu binafsi unapaswa kufanyika.
  • Familia hazihitaji tu takwimu. Zinahitaji kujua kilichompata ndugu yao.

7. Kuhusu taasisi
  • Tume isiishie kwa kutaja watu binafsi. Ijiulize pia:
  • Je, taasisi zilifuata taratibu?
  • Je, kulikuwa na mapungufu katika mfumo wa kutoa amri?
  • Je, kulikuwa na udhaifu katika usimamizi?
  • Je, kulikuwa na kushindwa kuwajibisha watendaji baada ya tukio?

Na kama kulikuwa na mapungufu ya kimfumo, ni mabadiliko gani yanapaswa kufanyika?

8. Kuhusu uwajibikaji
  • Hatimaye, kila tukio linalothibitishwa linapaswa kuhusishwa na hatua inayofaa.
  • Ikiwa mtu alifanya kosa la jinai, hatua ya kisheria ichukuliwe.
  • Ikiwa mtendaji alikiuka taratibu za kiutumishi, hatua ya kinidhamu ichukuliwe.
  • Ikiwa taasisi ilishindwa kutekeleza wajibu wake, marekebisho ya kitaasisi yafanyike.
  • Ikiwa sheria yenyewe ina mapungufu, mapendekezo ya marekebisho ya sheria yatolewe.
  • Na ikiwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya mtu aliyeshutumiwa, hilo pia lisemwe wazi.

NB: Matarajio haya si mwisho ila wada wanaweza kuongeza maswali mengine muhimu.”

UWAJIBIKAJI

Si lazima uwajibikaji uwe: “Mtu mmoja ndiye mwenye makosa yote.” Tunaweza kuwa na ngazi kadhaa za kuainisha uwajibikaji kama vile

Ngazi Swali
Mtu binafsiNani alifanya kitendo?
Uongozi/AmriNani alitoa au kupitisha uamuzi?
TaasisiTaasisi ilifanya au ilishindwa kufanya nini?
MfumoNi sheria/taratibu gani zilishindwa kuzuia tatizo?
Kwa mfano wa kinadharia:

Afisa A anatumia nguvu kinyume cha sheria → uwajibikaji binafsi.

Kamanda B alitoa amri isiyokuwa halali → uwajibikaji wa amri.

Taasisi C ilishindwa kusimamia matumizi ya silaha → uwajibikaji wa kitaasisi.

Sheria/taratibu D zilikuwa na pengo lililoruhusu tatizo → marekebisho ya kimfumo.

Asiyejulikana XXX aliua watu è

Hii ni muhimu kwa sababu uwajibikaji haupaswi kuishia kwa mtu aliyeshika bunduki, kama ushahidi unaonyesha kwamba maamuzi ya juu yalichangia tukio; lakini pia haupaswi kumfanya kiongozi wa juu awajibishwe moja kwa moja kwa kila kitendo cha mtu wa chini bila ushahidi wa uhusiano huo.

Hii ndiyo tofauti kati ya kulipiza kisasi na kuwajibisha.

Lengo la uwajibikaji si kutafuta mtu wa kulaumiwa kwa lazima. Lengo ni kuhakikisha kwamba kila jambo linalothibitishwa linapata jibu linalolingana na ushahidi na sheria.

Haya si maswali yanayopaswa kujibiwa kwa kauli za jumla tu kwamba “sote tulikosea” au kwamba “kulikuwa na wahusika kutoka upande fulani.” Uwajibikaji wa kweli unahitaji kutenganisha madai, ushahidi, maamuzi na majukumu ya kila upande na kila mmoja wetu.

Baada ya tukio kubwa la kitaifa, uponyaji wa jamii hauhitaji tu kusahau yaliyopita. Unahitaji pia kujua yaliyotokea.

Na kujua yaliyotokea kunahitaji taarifa zilizo wazi, uchunguzi unaoaminika, majibu kwa familia na biashara zilizoathirika, na maelezo kutoka kwa wale waliokuwa na mamlaka ya kufanya maamuzi.

Hatimaye, jamii inahitaji kufikia mahali ambapo kauli ya “Tulikuwa tumekosea” haionekani kama kushindwa, bali kama mwanzo wa kujifunza kutokana na kosa hilo.

Uwajibikaji haupaswi kuwa wa upande mmoja.

Angalizo


Ninapotumia neno Tanzania Bara, sifanyi hivyo kuwatenga ndugu zetu wa Zanzibar katika mjadala wa kitaifa. Ninarejea zaidi mazingira ya matukio ya Oktoba 29, 2025 ambayo kwa taarifa zilizopo yalijikita zaidi katika maeneo ya Tanzania Bara. Hata hivyo, historia ya Zanzibar ina uzoefu muhimu wa migogoro na vurugu zinazohusishwa na uchaguzi, hasa baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 na matukio yaliyofuata mwaka 2001. Uzoefu huo haupaswi kusahaulika; kinyume chake, unaweza kuwa sehemu muhimu ya mjadala wa kitaifa kuhusu namna Tanzania inaweza kuvuka mzunguko wa migogoro ya uchaguzi

TUJADILIANE: TUNATAKA TUME ITUAMBIE NINI
  • Ni swali gani kubwa ambalo bado hujaona likijibiwa kuhusu matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuata?
  • Ni ushahidi gani unaamini unapaswa kuangaliwa ili kupata jibu la swali hilo?
  • Katika tukio ambalo mtu alijeruhiwa, aliuawa, alipoteza ndugu au mali—familia yake inapaswa kupewa majibu gani?
  • Ikiwa Tume itabaini kwamba sheria ilikiukwa, uwajibikaji unapaswa kuchukua aina gani—kisheria, kinidhamu, kiutendaji au kitaasisi?
  • Ikiwa Tume itabaini kwamba kulikuwa na mapungufu katika taasisi, ni mabadiliko gani yanapaswa kufanyika ili hali hiyo isijirudie?
  • Je, kuna mambo ambayo wananchi wenyewe tunapaswa kujifunza kuhusu matumizi ya taarifa, mitandao ya kijamii, uchochezi, maandamano na tofauti za kisiasa?
  • Ni mambo gani ambayo Tanzania inaweza kujifunza kutoka katika uzoefu wa Zanzibar wa migogoro ya uchaguzi ya miaka iliyopita?
  • Na muhimu zaidi: tunataka kumbukizi ya Oktoba 29 iwe kumbukizi ya nini—maumivu pekee, au pia iwe mwanzo wa kujenga mifumo bora zaidi ya uchaguzi, usalama, haki na uwajibikaji?
  • Ni Kwa asilimia ngapi unadhani tume no 2 itaweza kujibu maswali yako ?
  • Ikiwa Tume itapendekeza uwajibikaji kwa wahusika (taasisi na watu binafsi) je unadhani utatekelezwa ?

Majibu ya maswali haya maswali mengineyo na hoja nyinginezo ni kusaidia kujenga mjadala mpana na endelevu zaidi

HITIMISHO: TUSISUBIRI KUMBUKIZI TU—TUITUMIE KUJADILI


Oktoba 29, 2025 ni sehemu ya historia ya Tanzania ambayo haiwezi kubadilishwa.

Lakini namna tunavyoikumbuka, tunavyoijadili na tunachojifunza kutokana nayo bado iko mikononi mwetu.
 
Back
Top Bottom