Mimi Bibi Yenu Mpambanaji
Senior Member
- Oct 6, 2024
- 147
- 303
Kampuni ya OYA inayotoa huduma za ukopeshaji wa fedha wamekuwa wakitenda uovu na udhalimu mwingi katika operation zake za kudai madeni.
Miingoni mwa udhalimu wanaoufanya, ni pamoja na kupiga, kutesa, kutekwa nyara kwa muda na kisha kwenda kukubwaga mbali na eneo lako la makazi.
Binti ya wangu wa mwisho kuzaliwa, alikuwa amekopa huko OYA kiasi cha 2.5 mil.
Basi siku hiyo wakamvamia nyumbani usiku wa saa tatu, alikuwa amebakiza marejesho matatu amalize deni lake. Basi akawaomba awapelekee kesho yake hela zilizobakia, wakakataa katakata. Wampiga sana, wakambeba msobe msobe na kumwingiza kwenye Gari. Wakamzungusha usiku kucha, kutoka Boko Magengeni njia ya Mbweni, wakaenda kumbwaga Mbagala shule ya msingi Jaribu akiwa Hana shilingi hata moja wala simu.
Basi hapo kulikuwa na walinzi wa shule ndio wakamsaidia kumpa simu kutujulisha yaliyomkuta, tukawaomba walinzi wampeleke kituo cha Polisi Mbagala Zakhem kwa ajili ya usalama wake.
Kesho yake asubuhi tukawepo kituoni, tukamchukua na kurudi naye nyumbani. Uhuni wa kampuni wa OYA haufai, ni lazima ukomeshwe mara moja.
Juzi wamempiga MTU hadi kumuua huko Mlandizi, wakikaliwa kimya hawa wataua watu wengi sana directly and indirectly.
Pia soma
- Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji