beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Klabu ya soka ya Real Madrid imefuzu kucheza fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya goli 2-2 na klabu ya Bayern Munchen
Kwa matokeo haya pamoja na matokeo ya mchezo wa kwanza(Real Madrid 2-1 Bayern Munchen), Madrid inasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-3
Katika mchezo wa jana Bayern ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa J. Kimmich(3') kabla ya K. Benzema kusawazisha na kufunga tena goli la pili(11' na 46'). Goli la pili la Bayern lilifungwa na J. Rodriguez(63')
Madrid sasa nasubiri kuona atakutana na nani fainali kati ya AS Roma na Liverpool huku Liverpool akiwa na faida ya goli 5-2 alizopata katika mchezo wa kwanza
Hii ni fainali ya tatu mfulizo Real Madrid inaingia huku ikiwa imeshachukua kombe kwenye fainali zote mbili za nyuma
Je, mpenzi wa soka unadhani Liverpool atafanikiwa kucheza fainali au Roma itapindua matokeo?