Baada ya Real Madrid kufuzu Fainali jana! Je, atakipiga na nani, Roma au Liverpool?

Baada ya Real Madrid kufuzu Fainali jana! Je, atakipiga na nani, Roma au Liverpool?

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Klabu ya soka ya Real Madrid imefuzu kucheza fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya goli 2-2 na klabu ya Bayern Munchen

IMG_20180502_071340.jpg


Kwa matokeo haya pamoja na matokeo ya mchezo wa kwanza(Real Madrid 2-1 Bayern Munchen), Madrid inasonga mbele kwa jumla ya magoli 4-3

Katika mchezo wa jana Bayern ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa J. Kimmich(3') kabla ya K. Benzema kusawazisha na kufunga tena goli la pili(11' na 46'). Goli la pili la Bayern lilifungwa na J. Rodriguez(63')

Madrid sasa nasubiri kuona atakutana na nani fainali kati ya AS Roma na Liverpool huku Liverpool akiwa na faida ya goli 5-2 alizopata katika mchezo wa kwanza

IMG_20180502_071500.jpg


Hii ni fainali ya tatu mfulizo Real Madrid inaingia huku ikiwa imeshachukua kombe kwenye fainali zote mbili za nyuma

Je, mpenzi wa soka unadhani Liverpool atafanikiwa kucheza fainali au Roma itapindua matokeo?
 
Hapo ni liver ndo anaingia fainali, then kombe linaenaelekea uingereza mapema kabisa, leo liverpool atashinda tena
 
Hapo ni liver ndo anaingia fainali, then kombe linaenaelekea uingereza mapema kabisa, leo liverpool atashinda tena
Mnajifariji au sio, Hivi nyie liver mngekutana na mmoja tu kati ya psg, juve au bayern hatua ya mtoano mngekuwa wapi sahizi zaidi ya kuwa wapenzi watazamaji.
 
Kwa Liver hii ninayoijua mimi labda mngesemea liver ya 2016 ila hii hii liver mnayoiona sasahivi aise,,, heeeee, mtajuta hyo siku,
 
Back
Top Bottom