Ndugu zangu Watanzania,
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan jasiri muongoza na shujaa wa Afrika ,kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt Husseni Mwinyi wamerekodi kwa pamoja Filamu ya kipekee kabisa kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanzania na nje ya mipaka, filamu inayoelezea na kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana hapa Nchini ,ambavyo huwezi kuvipata mahala pengine popote pale Duniani.
Katika filamu hiyo imemshirikisha pia muigizaji Nguli na wa kimataifa kutoka nchini china Jin Dong . Hii Maana yake nini ndugu zanguni? Hii maana yake filamu hii ambayo imekuwa gumzo ulimwengu kwote itatizamwa na Na watu wasio pungua Billion 2 siku tu itakapozinduliwa.kwa sababu China Pekee Ina watu zaidi ya Billion moja na million kadhaa yaani watu wengi zaidi ya idadi yote ya bara la Afrika lenye nchi takribani 55. Lakini pia filamu hii itavuka mipaka hadi nchi ya india ambayo nayo ina watu zaidi ya Billion moja.
Hapo bado sijaweka kwa nchi zingine ambazo nazo zitakuwa zikifuatilia kwa karibu uzinduzi huo ,ambao unakwenda kuweka rekodi ya kidunia pengine na kuingia katika vitabu vya Historia. Kwa hakika Rais Samia ni kiongozi mbunifu, anafahamu nini anafanya na nini afanye kuteka macho na masikio ya Dunia,anafahamu namna ya kufanya shughuli na shughuli ikawa ni kama shughuli ya Dunia nzima utafikiri sherehe za uzinduzi wa kombe la DUNIA.
Maana yake anakwenda kuliteka soko la watalii kutoka Bara la Asia Ambalo ni bara lenye idadi kubwa ya watu hapa Duniani ukilinganisha na Bara lolote lile kati ya mabara yote saba yaliyopo hapa Duniani.maana yake watanzania tunakwenda kushuhudia mafuriko na kumiminika kwa Watalii kuja hapa Nchini utafikiri maji yatiririkayo kutoka katika bomba lililopasuka .Tanzania tunakwenda kuwa kitovu cha utalii na chaguo nambali moja la watalii hapa barani Afrika.
Rai yangu ni kwa Wafanyabiashara wa ndani kujiandaa na fursa hiyo inayoletwa na serikali ya Rais Samia ,kwa kuhakikisha kuwa mnawekeza katika hoteli kubwa za kitalii zenye hazi ya kimataifa. Makampuni ya watalii hapa nchini kujiandaa kuteka na kuchukua fursa za ujio wa watalii. Anzeni kujiandaa mapema maana kunakuja kutokea gharika la watalii watakaokuwa wanafurika na kumiminika kuja hapa Nchini.
View attachment 2952819View attachment 2952820