Baada ya 'Royal Tour', Serikali sasa yaja na filamu nyingine iitwayo 'Amazing Tanzania'

Baada ya 'Royal Tour', Serikali sasa yaja na filamu nyingine iitwayo 'Amazing Tanzania'

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa Bungeni leo wakati akiwasilisha Hotuba ya kuhusu Makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi yake kwa mwaka 2024/25 amebainisha kuwa Serikali kutokana na mafanikio ya programu ya The Royal Tour, Serikali imetengeneza filamu nyingine yenye hadhi ya kimataifa ya kutanganza Utalii ijulikanayo kama 'Amazing Tanzania'.

Filamu hii kama ilivyokuwa kwa Roya Tour imerekodiwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi na mwigizaji nguli kutoka China aitwaye Jin Dong.

Filamu hii imeandaliwa kwa lengo la kuvutia watalii hususani soko la China na inatarajiwa kuzinduliwa Mei 2024.
Naombeni kazi ya kuwa Sterling Mkuu/Msaidizi kwenye hiyo filamu. Mimi nina kipaji cha kuigiza, kiasi cha kufikia Bongo Muvi wote kutonikaribia.
 
Huelewi kuwa filamu hiyo ina manufaa makubwa sana kiuchumi.kwasababu itavutia Watalii ambao watakuja na pesa za kigeni ambazo tunazitumia katika kuwekeza katika maeneo mengine .lakini pia pesa hizo za kigeni zitaisaidia kununua bidhaa nje ya nchi kama vile dawa za binadamu n.k.lakini pia itavutia wawekezaji mbalimbali
Hivi kwa akili yako finyu... Unategemea kupata watalii kutoka china!?...

Huo ni utaahira! Uliona wapi china Wana shobo na kutalii!?

Kiuhalisia sisi ndio watalii kwa china! Hawataki kujengea viwanda huku ili mkatalii china kila mwezi
 
Huelewi kuwa filamu hiyo ina manufaa makubwa sana kiuchumi.kwasababu itavutia Watalii ambao watakuja na pesa za kigeni ambazo tunazitumia katika kuwekeza katika maeneo mengine .lakini pia pesa hizo za kigeni zitaisaidia kununua bidhaa nje ya nchi kama vile dawa za binadamu n.k.lakini pia itavutia wawekezaji mbalimbali
Lucas mkuu unaelezea kama kwenye vile vitabu vya darasa la nne enzi zile miaka ya 80!
 
Back
Top Bottom