Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa kadri ya kumbukumbu zangu na kwa kadri ya umri nilionao , RPC Kyando wa Songwe ndiye kiongozi wa Polisi katili zaidi kwa waliopo sasa nchini Tanzania , huyu si wa kuonekana sana kwenye vyombo vya habari kama RPC Murroto wa Dodoma ambaye hata akikamata chupa 2 za gongo anataka TV zote zimuonyeshe , lakini unyama waliotendewa viongozi wa upinzani wa Mkoa wa Songwe na Jeshi la Polisi chini ya huyu RPC na hasa viongozi wa Chadema , haujawahi kufanywa mahali popote duniani.
Ukatili wa RPC Kyando wa Songwe unakaribiana na ule wa Omari Mahita alipokuwa RPC wa Kilimanjaro miaka iliyopita , lakini matukio ya uhalifu wa kawaida yanashamiri huku yeye akipambana na Chadema tu , Mahusiano ya wananchi na Polisi ni sawa na sifuri sababu kuu ikiwa ni unyama wa polisi dhidi ya raia kwa mambo ya kisiasa.
Ni Muhimu sana Kiongozi huyu wa Polisi Songwe akang'olewa ili kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao.