peter chula
Senior Member
- Jun 8, 2013
- 123
- 68
*BAADA YA SERIKALI KUANZA MAHOJIANO NA RAZALO NYARANDU KUHUSU KASHFA MBALIMBALI KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII RASMI ATIMKIA CHADEMA.*
Baada ya Serikali ya awamu ya Tano kuanza kushughulikia kashfa mbalimbali zilizofanywa na baadhi ya viongozi waliokua madarakani katika awamu zilizopita za uongozi tayari baadhi ya watu waliobanwa na Serikali kwa kashfa hizo wameanza kuhamia upinzani hususani CHADEMA ili kuandaa mazingira ya kuonekana wameonewa baada ya kufikishwa Mahakamani.
Duru za ndani ya Serikali zinadai kuwa toka Mh. John Pombe Magufuli amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Nyarandu amekua katika Wakati Mgumu akihojiwa kuhusu Mikataba Mbalimbali ya Kifisadi iliyisainiwa katika Kipindi ambacho amehudumu kama Waziri wa MALIASILI NA UTALII.
Baada ya kuhojiwa na Vyombo mbalimbali na kujiridhisha pasipo na shaka kuwa Mh. Nyarandu aliingia mikataba mibovu na baadhi ya Makampuni ya Kigeni kwa maslahi yake binafsi ikiwa ni Pamoja na uuzaji wa Vitalu vya Uwindaji Pamoja na kashfa nzito ya Kupandisha ndege Twiga wa Tanzania na kuuza raslimali mbalimbali za Taifa ndipo Serikali ilipochukua maamuzi ya Kumfikisha Mh. Nyarandu Mahakamani.
Katika Kufanikisha adhima hiyo Wiki kadhaa zilizopita Mh. Rais alimteua Mh. Hamis Kigwangala kuwa Waziri wa MALIASILI NA UTALII ambaye ameanza kwa kufuta leseni zote za Uwindaji zilizotolewa na Mh. Nyarandu kwa makampuni ya Kigeni kwa misingi ya Rushwa. Baada ya kuvunjwa kwa mikataba hiyo na kurudisha Serikalini baadhi ya Vitalu vya uwindaji Mh. Nyarandu amekua katika Wakati Mgumu kwani wawekezaji aliosaini nao mikataba wamembana wakitaka arejeshe mara moja pesa zao Pamoja na fidia kwani ameonekana aliwatapeli kwa kuwahakikishia kuendesha Shughuri zao Nchini katika njia za Unyonyaji.
Kwa hiyo kutokana na shinikizo alilonalo toka kwa Makampuni hayo ya Kigeni na Kwa namna serikali ilivyodhamilia kumfikisha Mahakamani kwa makosa ya Uhujumu uchumi ameamua kukimbilia Upinzani ili atakaposhitakiwa ionekan Upinzani Nchini Tanzania unaonewa.
Baadhi ya Makada wakongwe ndani ya Chadema waliotoa maoni yao wameonyesha kuchukizwa kwao na jinsi watu wenye kashfa za Ufisadi wanavyokimbilia kwenye chama chao.
Ninadhani sasa huu ni mtego, kama tutampokea chama chetu litakua chaka la kupokea Mafisadi alisikika akisema Kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya Chadema.
*_Je Chadema watampokea Nyarandu wakijua kuwa atafikishwa Mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za Ubadhilifu, kuitia Nchi hasara na kufanya ufisadi mkubwa?_*
Tuendelee kusubiri Kuona maamuzi ya Chadema kuhusu Nyarandu.