Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Hawa wazee wetu wanastahili pongezi za dhati kwa utumishi wao ndani ya chama na kuendelea kuaminiwa na chama.

Tuzidi kuwaunga mkono katika juhudi zao
Siku wakihama mtasikia ah wale walikuwa mafisadi😀
 
Kwa kweli wapewe tu pongezi. Maana wamekomaa ndani ya chama siku wakitoa tu mguu hapo hapo tutasikia kama haya ya Nyalandu. [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mwambieni 'Dada Mange' afute comments zake za kumtukana Nyalandu maana kushajiunga na Team Malofa
Halafu najaribu Ku connect dot nahisi ile iPhone X ya mange anayotamba kuwa kuna jamaa kamnunulia nahisi itakuwa ni huyu huyu nyalandu kanunua maana kuna alarm inanambia
 
Hoja yangu si kwamba Nyalandu ni msafi au hana makosa, ila ni wakati gani anaonekana mkosefu. Kwa nini makosa yao yanaibuka baada ya kuhama Chama? Kwa maana hiyo unaweza kusema kuwa kama una makosa, unakuwa salama zaidi ukiwa ndani ya CCM


hata hoja yangu hujaijibu, kwenye haki na ukweli lazima atetewe, wewe umeshindwa kuona kuwa hata humu jf pekee amesemwa kwa takriban miaka 7 kuwa ni mfuja mali?
 
Nasikiliza wimbo wa snura CHULA ANARUKARUKA CHURA[emoji445][emoji445][emoji443][emoji445][emoji444][emoji444][emoji444][emoji441][emoji441][emoji442][emoji442][emoji442]
 
Tutazaa naye tu huyo jangili hata akimbilie kwenye kitanda alicholalia fisadi mwenzake Tundu Lisu!
Aiseee chenge bado mpo nae mjue... wale wote wa escro pia mpo nao ... mjue..????
 
Hebu tuambie ni nani aliyeko CCM ni fisadi na mwizi?
LOWASA mlituambia ni mwizi, akahamia Chadema mkasema ni msafi kwa vile hajapelekwa Mahakamani. Hivyo hivyo Nyalandu mumelalamika uuzwaji wa vitalu kifisadi na twiga kupanda ndege na mhusika ni huyu huyu Nyalandu, sasa mnasema ni msafi kwa vile hajapelekwa mhakamani. Hizi ni akili za wapi?
 
Daaah kweli bana aisee all the connections are there huitaji akili ya kuambiwa kujua brother N anakimbia kitu kutoka huko alikokuepo!!!!
 


Naonan umeamua kuimba wimbo uleule wa kila siku. Shauri yako bwana. Hoja hujibiwa kwa hoja na sio nyimbo!
 
Kuhusu madai kuwa ameamua kutoka CCM baada ya kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, Nyalandu alisema hilo si kweli na hajawawahi kuhojiwa na kamati yoyote ya maadili, kuanzia wilaya, mkoa hadi Taifa.

Alisema hata zile tuhuma ambazo pia zimeanza kuibuliwa mitandaoni dhidi yake, si za kweli bali zinalenga tu kumchafua.

Alisema anashangaa tuhuma hizo kuibuliwa zaidi ya miaka miwili tangu aachie uwaziri na kueleza ni jinsi gani hahusiki.

Kuhusu utoroshaji wa twiga kwenda nje ya nchi, Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea kabla hajawa Waziri wa Maliasili na Utalii na kuwa katika kipindi chake hakuna kitalu chochote cha uwindaji kilichotolewa.

Alisema vitalu huwa vinatolewa kisheria na vina muda wake, hivyo alipoingia wizarani alikuta vimeshatolewa na mtangulizi wake, Ezekiel Maige na muda ulifika tena katika kipindi cha Profesa Jumanne Maghembe wakati yeye ameshamaliza kipindi chake.

Kuhusu kashfa ya Faru John iliyoundiwa kamati na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Nyalandu alisema hilo lilihusu Bodi ya Ngorongoro na uchunguzi ulifanyika na likaisha.

Nyalandu aliwataka wanaosambaza kashfa hizo waache kwa kuwa si za kweli.
 
rfiki na wanajf
aliyelet uzwazwa huu atambue kuwa mahakamani kutawaleta wengi,yupo katibu mkuu w wizara,yupo mwanasheria wa serikali naw awizara na hata DPP NAIONA KESI ITAKAYOFUMUA NA KUITOA CCM GAUNI WAZI
 
Mlkuwa wap cku zote hizo, mbona hamkuyaanika hadharani? Km kwel mmejidhatiti kuwa wawazi kwa wananchi wenu mbona hampo tayari kuweka mapungufu ya kiutendaji ya wizara husika au mnasubiri mpaka pale watakapozipuuzia sera za chama na kugeukia sera pinzan na huo ndio unakuwa mwanzo wa kuwakosoa kwa utendaji wao? Leo nyalandu mbaya kwa ccm kesho kinana akihama utasikia wanasema kinana hakuwa katibu mzuri.
Hahaha hii inchi bwana
 
Ccm bana akili zenu mnazijua wenyewe
Hivi wale Waarabu wapo pale miaka mingapi?? Na Nyalandu amekaa kwenye hiyo wizara miaka mingapi??
Kuna vitu Lumumba huwa mnajitia aibu wenyewe. Hivi kina Ngeleja, Chenge, pesa za mboga, na wale walio waita wenzao tumbili bado hawana kashfa mpaka wahame chama??
Hebu Lumumba tutajieni watu kumi wasafi ndani ya Ccm!!! Maana kuna samaki, kuna nyumba za serikali, kuna epa, kuna escrow, kuna watu wasio julikana na mengi tuuu.
Acheni Chadema iwape mambo
 


Vipi kuhusu Maige?

Au hadi hapo atakapohama CCM?
BTW Nyalandu alivyo mjanja ,ingekuwa kweli hayo usemayo ,angebaki huko huko asubiri " human face"
 
Mbona speed ya kumshambulia Lazaro imepotea baada ya kujibu tuhuma zote?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…