Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
Waache wafanye party ila wajue ukweli utaki kuwa ukweli milele.
 
Hakubaliani na jaribio la mauaji ya Lissu na kwamba serikali haijachukua hatua zozote mpaka sasa. Nafsi inamsuta kuwa mpambe wa serikali ya namna hiyo. Anataka kupigania katiba mpya ili nchi iwe na serikali ya watu kwa ajili ya watu.
 
Kwa mtazamo wangu, Ccm inapaswa kufurahi wanapoondoka watu wenye makandokando ya ufisadi. Hawa watu wameighalimu sana ccm, mambo sasa yanageuka, ndege wanaofanana wanaenda kuruka pamoja kwenye pori linalowafaa. Huko tunakoelekea rangi halisi ya chadema itaonekana. Naamini wengi ambao walikuwa na tuhuma mbali mbali za kukosa uaminifu wataondoka ccm. Na mwisho wa siku kazi ya chama tawala itakuwa nyepesi. Fact shall always prevail against all odds!!
 
maccm hamna akili kabisa, sasa mnatuletea huku sisi tufanyeje ?? MNA polisi mahakama, magereza usalama wa Taifa JWTZ, alafu hayo makampuni bado yako kwenye register ya makampuni mpaka Leo kweli ???
 
Madhara ya c&p umeleta kwa magreat thinker unaulizwa maswali unashindwa jibu na kichwa maji chako...

Muwe mnauwezo wa kutathimin mnayoandika before hamjafikisha mbele ya watu.
 

Badala ya kuleta Umbea humu mpelekeni Mahakamani wengi tunasubiria kesi zake huko.
 
Huu ni mwanzo tu, serikali ya JPM ndo inaelekea kutimiza 2yrs, watachohola wengi!
Wengine watajipga risasi,kujinyonga,kujitosa baharini ili Wafe kukwepa Kutumbuliwa!

Na yeye nani atamtumbua??Maana bado kile Kivuko Kibovu hatujapewa mahesabu yake
 
Wewe ni nani mbona hujitambulishi, au ni mtu usiyejulikana?
 
Usikatishe tamaa watu. Nyalandu yuko smart zaidi yako, anajua gharama na yuko tayari kwa lolote!
 
Mawazo uliyoandika ndiyo mawazo ya watanzania wengi wanaoumia “-lakini wanasema moyoni nitabomolewa! Hakuna ambacho kitadumu milele ila change lazima tubomolewe ili kuifikia mbingu!
 
Na je kwa tuhuma alizoelekezea na upinzani enzi akiwa waziri, akivuka boda na kuja upinzani tuhuma hizo huyeyuka na ghafla huwa shujaa??
 
sina hakika kama wapinzani wana pesa kiasi cha kununua watu toka ccm, Wao wenyewe hawana vitega uchumi vya kuwapatia pesa, Huyo nyarandu atakuwa kakimbia bifu ndani ya ccm hasa kitendo chake cha kuhamasisha matibabu ya lis
 
Rosemarie iko wazi kuwa utawala huu si rafiki kwa upinzani hata kidogo.

Hivyo nina mashaka sana kama Nyalandu ataweza kupata hata nusu ya kura kwenye matokeo ya kugombea ubunge kama atafanya hivyo kwa tiketi ya upinzani kwasababu si kwamba labda Tawala inakubalika saaana, la hasha bali kauli za Mkuu kwa watendaji wa ngazi za chini zikiashiria kutokukubali kupigwa chenga,, mpira uende mchezaji abaki ama mpira ubaki mchezaji uende,, undavaundava!!!

Pia ukizingatia upinzani ulivyolaini awamu hii umekosa mbinu kabisa ya kusonga mbele, wamekuwa waoga, wenye kulialia mitandaoni,,, rojorojo kama urojo la kipemba.

Sioni chaguzi zozote ndogo upinzani uka-shine awamu hii.

Nyalandu uamuzi ni mzuri kikatiba na kimsimamo ila timing ya maamuzi ndio tatizo kama unafikiri utaweza rudi bungeni kwa tiketi ya upinzani.
 

Hawawezi kuwashtaki maana wengi walifanya kwa kuwasaidia wastaafu wenye KINGA ndiyo sababu kuguswa siyo rahisi kivihvyo tunavyodhani.Nasubiria kesi ya Lazaro Nyalandu inayopelekwa mahakamani na UVCCM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…