Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.

Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.

Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.

Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.

Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.

FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.

Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Tutawaletea moja baada ya nyingine.
 
Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
 
Haya ni mawazo haijawahi kutokea,inamaana Nyalandu akiwa nje ya ccm hawezi kushughulikiwa kisheria pindi awapo na makosa? Hivi watu wengine huwa mnatumia nini kufikiri? Na nikwanini mwizi aachwe muda wote huo? Je serikali ilikuwa likizo?
 
Ccm ni wapushkuna na wanafiki wakubwa...
Ni kwa nini haya yaibuke leo?
Leo hata Jaffo ikitokea akihama ccm basi maccm ni lazima yamfanyie fitina!
Kama vipi basi ccm wekeni kashfa za viongozi wote walioko madarakani na waliostaafu.
 
Kama yote haya yanafahamika kwa nini hapelekwi mahakamani? Na siku zote mnakuwa wapi hamuyasemi mpaka mtu ahame Chama? Hii ni ishara hakuna mtu msafi CCM, wanaogopa kuhama kwa kuhofia kuanikwa. Nina amini siku Rais Magufuli akihama CCM, naye yatamkuta haya
 
Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.

Wanasiasa wa vyama vyote wameshajua kuwa waTanzania tuna ulemavu wa kufikiria na mihemko iko juu........ndio maana wametugeuza kama vikaragosi......

Wanajua kusoma alama za nyakati na kuzitumia vyema nyakati.......
 
Ccm ni wapushkuna na wanafiki wakubwa...
Ni kwa nini haya yaibuke leo?
Leo hata Jaffo ikitokea akihama ccm basi maccm ni lazima yamfanyie fitina!
Kama vipi basi ccm wekeni kashfa za viongozi wote walioko madarakani na waliostaafu.

Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa waliokuwa wakiibua shutuma za ufisadi wa Nyalandu ni upinzani....haswa masuala ya vitalu......
 
Hahaaaa.... Machagadema yameshaanza kazi ya kumsafisha Nyala...ndu
 
Mleta Mara huu ni ulimbukeni unaousema hapa tena ulemavu wa akili
Unaposema nyalandu kamkimbia kingwangala
Ivi kama MTU anakosa kuhama chama ndo kukimbia kosa sheria ya wapi hiyo inayomhukumu MTU aliye CCM tu akihama inamwacha acha ulimbukeni
Pili huyu jamaa alionesha kukerwa na CCM tangu lissu ashambuliwe alianza kwenda against na nyie CCM wenzake alichokifanya sasa alikipanga muda hapa ulikuwa timing tu
Mwrnzenu kasoma alama za nyakati
Huyu jamaa ni genius sana
Fuatilia ata shule za secondary alizopita utadhirisha hilo
Kibaha_ilboru
Hapa anacheza na akili zenu tu mambulula kama wewe

Kingwangala ata mwezi hajafika tangu kuteuliwa hiyo wizara Leo useme kakimbiwa
Ulikuwa umfuatilii mnyambala nyalandu tangu shambulio la lissu litokee kawa tofauti sana
 
Ujambazi huko utalii haujaanza Jana wala juzi ni muendelezo tuu Stanley Katabalo alipotea kwa kuzungumzia ukweli wa Loliondo Gate kwenye magazeti ya mfanyakazi na motomoto wakati huo..
 
Ninachokijua angeendelea kubaki angeneemeka zaid na inawezekana kesi ingeishia juu kwa juu lakin kajisacrifice kutoka akijua kabisa kua cha moto atakiona.....
Uzuri machungu ya upinzani ashayaona wanavoteswa
Na mtambue kua uuzaji wa vtalu n process agizo halitoki kwa waziri peke yake ad ofisi ya rais inahusika
Kwaio msitegemee lolote kuhusu hii kesi zaid sana watamsumbua sumbua tu
Kwani lowassa ameshtakiwa ad sasa!?
Mahakama ya mafisad imeshafumga wangap!?
 
Kumbu kumbu zangu zinaniambia kuwa waliokuwa wakiibua shutuma za ufisadi wa Nyalandu ni upinzani....haswa masuala ya vitalu......
Well, lakini kwa nini ccm walikuwa kimya?
Huyu aliyeleta huu uzi ni kada wa ccm!
 
Mkuu ukisema nyalandu kamkimbia kigwangala.
Utakuwa unakosea.

KWANI NYALANDU AMEKIMBIA NCHI?
SI YUPO HAPA HAPA?

Sasa kamkimbia vipi?
Naomba ufafanuzi tafadhali.
sio kweli jamaa kwa sas hayupo nchini
ingia [HASHTAG]#magekimambi[/HASHTAG]....... usome zaidi
 
nyalandu2.jpg
 
Back
Top Bottom