Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Vipi kuhusu kumuvua ukurugenzi wa wanyamapori enzi zile Prof Alexander Songorwa, hujuma zake kwa waziri wake Balozi Kagasheki?
Jamaa wamekwisha sahau kabisa hasara aloileta Nyarandu ktk wizara ya maliasili na utalii.
Waache wafanye party ila wajue ukweli utaki kuwa ukweli milele.
 
Hakubaliani na jaribio la mauaji ya Lissu na kwamba serikali haijachukua hatua zozote mpaka sasa. Nafsi inamsuta kuwa mpambe wa serikali ya namna hiyo. Anataka kupigania katiba mpya ili nchi iwe na serikali ya watu kwa ajili ya watu.
 
Kwa mtazamo wangu, Ccm inapaswa kufurahi wanapoondoka watu wenye makandokando ya ufisadi. Hawa watu wameighalimu sana ccm, mambo sasa yanageuka, ndege wanaofanana wanaenda kuruka pamoja kwenye pori linalowafaa. Huko tunakoelekea rangi halisi ya chadema itaonekana. Naamini wengi ambao walikuwa na tuhuma mbali mbali za kukosa uaminifu wataondoka ccm. Na mwisho wa siku kazi ya chama tawala itakuwa nyepesi. Fact shall always prevail against all odds!!
 
Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.

Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.

Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.

Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.

Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.

FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.

Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Tutawaletea moja baada ya nyingine.
maccm hamna akili kabisa, sasa mnatuletea huku sisi tufanyeje ?? MNA polisi mahakama, magereza usalama wa Taifa JWTZ, alafu hayo makampuni bado yako kwenye register ya makampuni mpaka Leo kweli ???
 
Madhara ya c&p umeleta kwa magreat thinker unaulizwa maswali unashindwa jibu na kichwa maji chako...

Muwe mnauwezo wa kutathimin mnayoandika before hamjafikisha mbele ya watu.
 
Wiki iliyopita Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Hamisi Kigwangalla, akizungumza na wadau wa Wizara yake alisema kuwa baadhi ya mawaziri na wabunge wa awamu ya nne wangepaswa kuwa jela kwa ufisadi na ushiriki wao kwenye ujangili. Leo Nyalandu amekimbia. Ifuatayo ni historia ya kashfa moja ya Nyalandu.

Kampuni ya Kimarekani ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo inamiliki kampuni tanzu za uwindaji wa kitalii za Mwiba Holdings Ltd, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) ni miongoni mwa watuhumiwa wa ujangili
Uchunguzi unaonesha kumekuwapo matukio kadhaa ya wafanyakazi wa Mwiba kukamatwa wakiwa wameua wanyamapori na kukutwa na nyara za Serikali.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii vimesema mara zote kesi zinazoihusu kampuni hizo zimekwama kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni urafiki wao wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu.

Urafiki wa Nyalandu na wamiliki wa kampuni hizo ulikuwa mkubwa kiasi cha kumpatia moja ya helikopta zake aitumie kwenye mbio za kuwania urais, kabla ya kushindwa na kujielekeza kwenye ubunge.

Helikopta ya kampuni hiyo ndiyo aliyoitumia wakati wote wa kampeni zake za ubunge
Nyalandu alimwamuru Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori wa wakati huo, Paul Sarakikya, kutoa Leseni ya Rais kwa familia ya Tom Friedkin (mmiliki wa kampuni hizi) kuwinda wanyamapori 700 katika vitalu vinane na eneo la wazi la Makao. Leseni hizo zilitolewa bure bila kulipiwa hata senti.

Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kwenye orodha ya kuuawa ni tembo walio katika hatari ya kutoweka.

Pia Nyalandu alikiuka sheria kwa kupuuza ukomo wa idadi ya vitalu vitano kwa kampuni moja. TGTS imemilikishwa vitalu vinane pamoja na eneo la wazi; hali ambayo ni ukiukwaji wa kifungu cha 38(7) cha Sheria ya Wanyamapori.

Kampuni hiyo pia ilipewa vitalu na Nyalandu kinyemela, ilhali sheria ikiagiza kuwa kitalu kinapobaki wazi sharti kitangazwe kwanza na waombaji washindanishwe katika mfumo na utaratibu ulio wa haki na uwazi [Kanuni ya Uwindaji wa Kitalii 18(1).

Pamoja na kutoa Leseni ya Rais, Wamarekani hao walileta watoto wadogo, chini ya umri wa miaka 18 kuwinda; jambo ambalo ni kinyume cha kifungu cha 43(3) cha Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009.

FCF na kampuni tanzu imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama (Makao Ranch).

Kampuni ya Mwiba Holdings Ltd chini ya TGTS Ltd ambazo zinamilikiwa na Friedkin Conservation Fund (FCF) imekuwa ikiendesha shughuli za utalii kwenye eneo la Makao WMA tangu 2011 baada ya Mwiba Holdings Ltd kumilikishwa eneo jirani na WMA ya Makao kwa ajili ya shamba la mifugo na wanyama.

Hata baada ya kumalizika Mkataba wake na JUHIWAPOMA, kampuni ya Mwiba Holdings Ltd iling’ang’ania na kuendelea kukalia eneo la Makao WMA kwa mabavu na kinyume cha sheria.

Tutawaletea moja baada ya nyingine.

Badala ya kuleta Umbea humu mpelekeni Mahakamani wengi tunasubiria kesi zake huko.
 
Huu ni mwanzo tu, serikali ya JPM ndo inaelekea kutimiza 2yrs, watachohola wengi!
Wengine watajipga risasi,kujinyonga,kujitosa baharini ili Wafe kukwepa Kutumbuliwa!

Na yeye nani atamtumbua??Maana bado kile Kivuko Kibovu hatujapewa mahesabu yake
 
Wewe ni nani mbona hujitambulishi, au ni mtu usiyejulikana?
 
Asubuhi hii nakuja na swali kama linavyojieleza,Maamuzi ya Mh Nyalandu kidogo yameninyima usingizi,je Mh unaweza real kuwa mwanasiasa wa upinzani kama Lisu,Lema,Mbowe,Halima Mdee,Msigwa
???je unafikiri this is right time to do so??unaonaje maneno ya Mh Lowasa Jana kwamba umechelewa?? Alikuwa anamaanisha nini?
Kwa kuwa nina uwezo wa kufikiri mbali kidogo nimeona nimshauri Mh Nyalandu mambo yafuatayo,na ninaamini atayapa kipau mbele kwa kuwa anakoelekea nilishakaa huko na najua matokeo yake,
Je Mh Nyalandu unayajua maneno ya Rais Magufuli aliyotamka adharani kwamba atakayetupinga tutambomoa au tutamvunja? Kabla ya kuchukua maamuzi uliwaza kitu kama hicho?je upo tayari kulipa gharama ya kuwa mwanasiasa mpinzani nchi hii? Ninachoona kwa macho yangu na kuamini moyoni mwangu ni kwamba unampinga mwanyekiti wako wa zamani na alishatoa warning!!!
Mh Nyalandu kuna gharama kubwa sana unatakiwa ulipe kuanza sasa hivi za safari uliyoanza Jana,kwa mtazamo wangu hutaweza na Lowasa alijaribu kukueleza kwamba umechelewa,huu sio wakati muafaka wa kufanya unayotaka kuyafanya,is dangerous and your risking it all?
Wanasiasa wa upinzani wameshalipa gharama kubwa kila MTU kwa wakati wake
Wamepigwa na polisi wanaotakiwa kuwalinda,wametukanwa,wameuawa,wamezushiwa na kufanyiwa vitendo vibaya na serikali unayojiandaa kuipinga,
Nakushauri huu sio wakati muafaka kufanya unayotaka kufanya,ni hatari kubwa kwa kuwa unataka kumpinga MTU aliyesema Ukinipinga nakubomoa,
Hutaweza kupita walikopita wakina Lissu is too late brother,
Dr Slaa yupo zake kanada katulia na familia mastrees yote ya kijinga yameisha,
Hujazoea misukosuko wanayopitia wapinzani and is too late now,
Ondoka Tanzania haraka sana chukua familia yako nenda nchi yoyote au rudi zako marekani enjoy life my friend,
Jambo unalotaka kufanya ni hatari kwa maisha yako na itakugharimu heavy price,
Brother hakuna politics in African, is wasting time,achana na siasa utaumia hutamuweza Magufuli atakuumiza,
Naongelea uzoefu na Mimi binafsi nimelipa gharama kubwa za kuwa mpinzani na nimekuja kugundua ni hatari kubwa na nimeamua kukaa pembeni kwa sababu I will never change anything anyway,,,,
Usikatishe tamaa watu. Nyalandu yuko smart zaidi yako, anajua gharama na yuko tayari kwa lolote!
 
Mawazo uliyoandika ndiyo mawazo ya watanzania wengi wanaoumia “-lakini wanasema moyoni nitabomolewa! Hakuna ambacho kitadumu milele ila change lazima tubomolewe ili kuifikia mbingu!
 
Mnataka kutuaminisha kuwa mtu akiwa CCM anaweza kufanya makosa yoyote ya kiutendaji na akabaki salama? Pia kwa mapovu ambayo watu wanaanza kutokwa sasa ina maana Nyalandu angebakia CCM hapakuwepo shida angeheshimika kama mbunge na waziri mstaaafu wa mali asili siyo? Kwa nini haya yote hayakusemwa kipindi akiwa kwenye power as minister, akiwa CCM kama mbunge na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa?
Na je kwa tuhuma alizoelekezea na upinzani enzi akiwa waziri, akivuka boda na kuja upinzani tuhuma hizo huyeyuka na ghafla huwa shujaa??
 
sina hakika kama wapinzani wana pesa kiasi cha kununua watu toka ccm, Wao wenyewe hawana vitega uchumi vya kuwapatia pesa, Huyo nyarandu atakuwa kakimbia bifu ndani ya ccm hasa kitendo chake cha kuhamasisha matibabu ya lis
 
Rosemarie iko wazi kuwa utawala huu si rafiki kwa upinzani hata kidogo.

Hivyo nina mashaka sana kama Nyalandu ataweza kupata hata nusu ya kura kwenye matokeo ya kugombea ubunge kama atafanya hivyo kwa tiketi ya upinzani kwasababu si kwamba labda Tawala inakubalika saaana, la hasha bali kauli za Mkuu kwa watendaji wa ngazi za chini zikiashiria kutokukubali kupigwa chenga,, mpira uende mchezaji abaki ama mpira ubaki mchezaji uende,, undavaundava!!!

Pia ukizingatia upinzani ulivyolaini awamu hii umekosa mbinu kabisa ya kusonga mbele, wamekuwa waoga, wenye kulialia mitandaoni,,, rojorojo kama urojo la kipemba.

Sioni chaguzi zozote ndogo upinzani uka-shine awamu hii.

Nyalandu uamuzi ni mzuri kikatiba na kimsimamo ila timing ya maamuzi ndio tatizo kama unafikiri utaweza rudi bungeni kwa tiketi ya upinzani.
 
serikali ililala haikuwasikiliza kwa hiyo muda huu ndo wanazinduka baada ya kuondoka sijui haya mambo yamekaaje ccm haiwezi kuziona kashfa za wakina chenge,tubaijuka na ngeleja wakiondoka nao itaandikwa kama wewe ulichoandika.

nguvu ya kushughulika na kashfa za wizi ni ndogo mno hapa lazima tutambue kuwa wastaafu wakuu wapo huko ccm walihusika ktk wizi haiwezekani vidagaa viwe vinanguvu kubwa namna hii naamini bila hao wastaafu kwa nguvu aliyonayo magufuli wengi wangekuwa jela.

Hawawezi kuwashtaki maana wengi walifanya kwa kuwasaidia wastaafu wenye KINGA ndiyo sababu kuguswa siyo rahisi kivihvyo tunavyodhani.Nasubiria kesi ya Lazaro Nyalandu inayopelekwa mahakamani na UVCCM
 
Back
Top Bottom