Baada ya shambulizi la Israel dhidi ya Iran kuzuiliwa na mifumo ya anga ya Iran inaoneka wafuasi wa taifa teule wa humu JF hawaamini ndo maana kila dakika wanaanzisha nyuzi za kujifariji.
Mara mifumo ya ulinzi ya Iran imeharibiwa ,mara viwanda vya makombora vimeharibiwa, mara warazimishe tuamini kuwa ndege za Israel ziliingia ndani ya anga la Iran wakati hata vyombo vya habari vya Israel vinaripot kuwa mashambulizi yanefanyika kutokea kwenye anga ya Iraq km 100 kutoka mpakani mwa Iran.
Lakini mpaka sasa hawajatuletea ushahidi wa hizo tumba wanazo ziandika humu. Na kuonesha wanavyo babaika wanatuwekea mpaka video za makombora ya Iran yakiipiga Israel na kudai ndo shambulizi la Israel dhidi ya Iran 😃😀.
Wote tumeshudia video za mifumo ya ulinzi ya Iran ikiyaangusha makombora sasa na nyinyi tuletee video ya makombora yakitua na kuharibu hivyo mnavyovisema.
Kwenye shambulizi la Iran October1 tuliona kwa macho yetu makombora yakipiga mpaka Marekani akarazimika kuleta mifumo yake baada ya kuona ya Israel ni takataka, sasa na nyinyi tuleteeni ushahidi acheni kuturazimisha tuamini mambo ya kusadikika.
Hata vyombo vya habari vya kimagharibi vinajaribu kulikuza shambulizi la Israel lakini kwenye comment watu wanavipa za uso.
View attachment 3136875