John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe na wenzake watatu, wameachiwa huru leo Machi 4, 2022, na Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo.
Hatua hiyo imekuja siku 226 tangu aanze kuwa rumande, hay ani maoni mbalimbali ya watu maarufu, wanasiasa na viongozi wa dini wametoa maoni:
Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe:
"Kipekee kabisa, nitumie nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza wale wote ambao - kwa maneno na vitendo; sirini na hadharani, wamefanikisha kutendeka kwa haki katika kesi ya Ndugu Freeman Mbowe. Haki imetendeka."
Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF
“Tulieleza, haikuwa na afya sana nchi hii kurejea katika zama za ukoloni, kila aliyetoa kauli aliishia gerezani. Kimepita kipindi kigumu, hatufufui makaburi. Tunampongeza DPP kwa kuchukua uamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa letu.”
Askofu Benson Bagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe, Kagera:
“Mbowe ametoka gerezani alimokaa miezi 8. Watu wanashangilia kuwa Mbowe yako huru. Mimi nasema hayuko huru bali yuko nje ya gereza, kwa sababu sheria iliyomshtaki na kumnyima dhamana bado haijafutwa.”
Askofu Emmaus Mwamakula:
“Leo nina furaha kwa sababu toka mwanzo wamewakamata, sisi viongozi wa dini tuliona hii kesi ilikuwa ya kisiasa na tulipaza sauti Mbowe aachiwe bila masharti yoyote. Katika hili hatukuweza kumung'unya maneno, ilikuwa ni safari ndefu.”
Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Benson Kigaila:
“Tuliwaambia tangu mwanzo, hawana kesi (mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Freeman Mbowe), wakasema wana kesi lakini leo wamethibitisha hawakuwa na kesi.”