Baada ya taifa stars kutolewa kwenye mashindano ya afcon 2019, njoo hapa tuikosee na kuishauri taifa stars

Ladder 49

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
7,918
Reaction score
20,037
Wakuu Habari zenu?

Walikuwa wanasema sio vizuri kuwakatisha tamaa wachezaji kabla mashindano hayajaisha mnawaraumu.

Sasa tumetolewa nadhani ni ndio muda muhafaka wa kukosoa na kushauri.

Kwa upande wangu najiuliza hawa wachezaji wanafanyaga mazoezi ya aina gani?

Yaani kupiga pass 5 tu hawawezi lazima wapoteze mpira.nashauri kwenye mazoezi wawewanafanya mazoezi ya kupiga pass ,pass 10 goli.na sio kufunga kwanza.

Na kingine ni vizuri hao wachezaji wakawa wanacheza ma game ya mpira kama FIFA,... ilikujifunza mpira unachezaje mpira sio kupeleka mbele tu unabutua.ukifanya hivyo utakoga mvua za magoli.

Mpira lazima utengeneze nafasi ndio ufunge.

Labda iwe kwenye ligi yetu huku kila timu inacheza formation ya 4-5-1, hiyo formation hata watoto hawajui mpira mitaani wanacheza hivyo hivyo .dunia ya sasa imebadilika.

Sijajua kocha anafundisha mpira gani zaidi ya kutaka tu wachezaji wapeleke mpira mbele tu.

Wachezaji wafundishwe kukaba na kucheza mpira.

Tumetia aibu afcon 2019,mara ya mwisho tulitoka na point 1. Safari hii bila hata point 1.

Kocha afundishe wachezaji kucheza mpira na sio tu kuweka wachezaji uwanjani wanakimbia kimbia tu uwanjani.

Ni hayo tu machache wakuu,ongezea na wewe ya kwako Hapo chini.

 
Hii timu naishauri isikubali kutumika kisiasa. Vinginevyo mimi binafsi nitaendelea kuiombea iendelwe kupokea vipigo vya kuichakaza kabisa.

Michezo huleta ari na umoja wa kitaifa ila kwa hapa kwetu michezo inatumika kama jukwaa la kisiasa na kusifu ovyo ovyo propaganda za chama tawala
 
Wakuu Habari zenu?

Walikuwa wanasema sio vizuri kuwakatisha tamaa wachezaji kabla mashindano hayajaisha mnawaraumu...
Mimi binafsi kwa moyo mweupe bila unafik naipongezaza stars na bench lote la ufundi, Kocha na wasaidizi wake wamefanya kilakitu walichoweza ila matokeo tuliyopata si mabaya kwenye soka kulingana na nama tunavyo endesha soka letu.

Timu tulizocheza nazo zilikua bora kuliko sisi baadhi ya timu hazikuchezesha ata mchezaji mmoja anayecheza Afrika. Tunahitaji vijana watengenezwe na watafutiwe nafasi wakacheze nje ya nchi.

Huwezi shindana na wachezaji wanaocheza njeya bara la Afrika na hawa wakwetu wanaocheza ligi dhaifu za kwetu. Hatua ya kufuzu ili tosha kwa sasa tuanze kwa kujizoesha kufuzu marakwa mara uku tukiendelea kupeleka vijana nje baada ya muda tutakua washindani.

Magoli tuliyofungwa kwa kila mechi, Katika soka hayakua mengi . Vijana wamejitaidi sanasana. Pongezi kwao, Wote kuanzia mashabik, viongozi katika soka, na wachezaji tumejifunza kitu.
 
Kuanzia samatha mpaka wenzake hakuna kitu kabiisa.....

Waanze kukuza vipaji chap... Wawachukue under 17 wawaweke pamoja kwa miaka miwili... Nina hakika tunarudi teena viizuur kuule
 
Wakuu Habari zenu?

Walikuwa wanasema sio vizuri kuwakatisha tamaa wachezaji kabla mashindano hayajaisha mnawaraumu...
Siyo mbaya Sisi lengo letu tayari lilishatimia baada ya kufuzu tu, wala siwadai kocha wala wachezaji kilichotokea nilikitegemea hata angeenda nani tungepigika tu maana sisi hatuna wachezaji wa kushindana,labda Msuva na Samata kidogo.

 
Wakuu Habari zenu?

Walikuwa wanasema sio vizuri kuwakatisha tamaa wachezaji kabla mashindano hayajaisha mnawaraum...
Falsafa ya kubutua mpira uende mbele Sijui wamefundishwa na nani. Kwamba Wapinzani wakipokonywa mpira na nyinyi basi mnawarudishia tena ili waendelee kuuchezea nyie muwakabe. Kasumba mbaya sana hii aisee.

Kwanini isiwe Wapinzani wakipoteza mpira kwenu basi iwe ni zamu yenu kuuchezea ili wao ndio wawakabe? Yaani nyinyi mmeumbwa kukaba tu pale wapinzani wawapo na mpira? Nyie mtauchezea saa ngapi sasa na kutafuta magoli? Mnashindwa kukaa na mpira walau hata dakika tatu labda?

Mechi zote tumefungwa kihalali kabisa, hakuna hata mechi moja tulio posses mpira.
 
KOCHA RC WA DAR UNATEGEMEA KUNA NINI HAPO?
 
Hakuna hio timu labda kama unasema CCM stars
 
Mimi binafsi ningeishauli tuwekeze zaidi katika soka la vijana kwani ndio njia sahii kuwatoa vijana kwenda kwenye ligi kubwa ulaya kwasababu kwetu hapa tuanza kumjua mchezaji tayari amesha kuwa over 27 katika soka la ushindani tutaferi tuu
 
tatizo siasa ameanza kuingiza Wallace karia

nakumbuka enzi za jakaya pamoja na kumlipa mshaahara masio maximo lakini hakuwahi kuingiza usisiemu kwenye team
 

Hii timu siipend ovyo kabsa
 
Wakuu Habari zenu?

Walikuwa wanasema sio vizuri kuwakatisha tamaa wachezaji kabla mashindano hayajaisha mnawaraumu...

Hi timu ni mbaya sana maana imeamua kutugawa na kutumika kichama! Siwez kuwa pamoja na timu inayotimiza ilan achia akina polepole tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…