Baada ya tamko la TEC, tunasubiri tamko la BAKWATA

Bakwata wakivaa kanzu na lemba lile nao wanajiona ni waarabu soo hawezi kuwa na tamko lolote zaidi yakushingizia waislam wanaonewa wivu na wakristu.
Mkuu kwenye suala maslahi ya taifa tunapaswa kusimama pamoja kama taifa badala ya kuangalia maslahi binafsi.
 
Baada ya TEC kuukataa mkataba wa DPW hadharani bila kumumunya maneno, sasa tunasubiri tamko la BAKWATA nao tusikie watasema nini. Ni matumaini yangu kwamba BAKWATA watafuata nyanyo za TEC kwa kuukataa mkataba wa DPW bila kupepesa macho.

Aidha, inawezekana BAKWATA wakaukubali mkataba na endapo watafanya hivyo basi watakuwa na sababu za msingi. Au wanaweza kuukubali na kutoa maoni kuhusu kuboreshwa vipengele vyenye utata, hasa vile vinavyohusu muda wa mkataba na vinavyobagaza mamlaka ya nchi (sovereignty).

Kimsingi ni vigumu kubashiri nini BAKWATA watasema lakini kwa kuwa bado hawajatoa tamko hadharani, ngoja tusubiri tuone watakuja na tamko zito au jepesi kiasi gani. Waswahili wanasema 'usiusemee moyo' au 'usiandikie mate wakati wino upo'. Kwa maana hiyo, hebu tuvute subira kidogo tusubiri kusikia BAKWATA watakuja na tamko la aina gani. Wakati ukifika wataanika kila kitu hadharani. Subra yavuta kheri.
1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
Hatuhitaji kufuata matamko ya TEC au BAKWATA bali hoja zenye mantiki za kuwafaidisha watanzania na waafrika kwa ujumla.
Hizi dini zetu hizi zina msingi wa kumnyonya na kumdhalilisha mwafrika.
Fikra mbaya na mbovu kuliko yote ni kwa mwafrika kutukuza manabii wa wageni na kudharau wa nyumbani.
 
Baada ya TEC kuukataa mkataba wa DPW hadharani bila kumumunya maneno, sasa tunasubiri tamko la BAKWATA nao tusikie watasema nini. Ni matumaini yangu kwamba BAKWATA watafuata nyanyo za TEC kwa kuukataa mkataba wa DPW bila kupepesa macho.

Aidha, inawezekana BAKWATA wakaukubali mkataba na endapo watafanya hivyo basi watakuwa na sababu za msingi. Au wanaweza kuukubali na kutoa maoni kuhusu kuboreshwa vipengele vyenye utata, hasa vile vinavyohusu muda wa mkataba na vinavyobagaza mamlaka ya nchi (sovereignty).

Kimsingi ni vigumu kubashiri nini BAKWATA watasema lakini kwa kuwa bado hawajatoa tamko hadharani, ngoja tusubiri tuone watakuja na tamko zito au jepesi kiasi gani. Waswahili wanasema 'usiusemee moyo' au 'usiandikie mate wakati wino upo'. Kwa maana hiyo, hebu tuvute subira kidogo tusubiri kusikia BAKWATA watakuja na tamko la aina gani. Wakati ukifika wataanika kila kitu hadharani. Subra yavuta kheri.
Hatutoi tamko tuko nyutro!!
 
Hao si wanawakilishwa na Sheikh Mwaipopo!!
 
Kumbuka moja ya ahadi za DPW nikujenga misikiti Sasa bakwata watasemaje?
Bakwata wanajielewa wala hawatadanganyika na ujengaji wa misikiti!! Ila wale wanaovaa "don't touch", yaani kanzu fupi, suruali fupi na muda wote wako kinyume na bakwata hao ndo wajomba zake DP World!!
 
Mkuu hili sio sula la kidini hata kidogo. Ndio maana hata TEC wametoa maoni yao kama raia wengine wa kawaida wanaoguswa na utapanyaji wa rasilimali za taifa.
Ajabu hawajatoa hata siku moja kuhusu mikataba mibovu ya madini dhidi ya waingereza, au mimi tu ndo sijasikia?
 
BAKWATA wakitoa tamko watakuwa hawajitambui.. maana haiwezekani wafanye mambo baada ya kuona wenzao wamefanya.
 
Kwanini mkuu? Kwani wao hawana haki ya kutoa tamko?
 
Back
Top Bottom