Baada ya TCRA kuzuia local channels, Chaneli za Kigeni zinazotumia Kiswahili zashika usukani. Kenya yatawala soko

Njia mbadala ni kurudi analog
 
Shida ya TBC ni kwamba program zake haziendani na diversity ya media industry ilivyo sasa, kwanza kabisa hawana uhuru wa kuoperate as independent media, hili silielezei kwa undani ila athari zake ni kwamba program za TBC zinakuwa unbalanced. Pili pengine bajeti au mtaji wa kujiendesha unasuasua sababu ubora wa vipindi kuanzia upigaji picha mpaka sound output ya TBC hauko vizuri, nadhani pia hata vitendea kazi hawana vya kisasa na vinavyotakiwa, mfano, jana tu asubuhi nimemshuhudia mtangazaji akiwasiliana na correspondent kutoka kisiwa cha Ukara akiwa kashika simu kwa mkono wake kaiweka loud speaker halafu kaisogeza mdomoni mbele ya camera, nilisikitika sana kwakweli. Yaani audio expert wa TBC hata kama hawana lapelle at least wangetumia hata bluetooth handsfree kit wangetap receiver yake kwenye sound system hakuna hata asingejua kuwa hamna lapelle inayoweza kuunganishwa na simu. Huu ni mfano mdogo tu natumai ipo siku haya yatatuliwa na TBC itarudi kuwa vibrant na itapata watazamaji wengi.
 
Kwani walifungiwa ili wazioneshe bure? Au walifungia kwa kuwa hawana sijui leseni ya matangazo ya mitandaoni? Kwa hiyo wakalipie wapate hizo leseni. Hapa serikali yenye kuwaka tamaa ya hela tayari imeshalenga mpunga. Sidhani kama lengo ni hilo la kutaka zioneshwe bure kama mnavyotaka kutuaminisha. Kama sielewi vizuri naomba kueleweshwa
 
Mbona unaconclude mkuu, ulikua na wazo lako ndo umeamua kulisema hivyo, kwahiyo ww unapenda kulipia stesheni za ndani au hupendi
 
Wanaposema channels za bure mimi hata sielewi, maana jana tu, kifurushi cha Star times kiliisha. Channels zote hizo wanazozitambia kuwa ni za bure, wameziondoa: ITV, CHANNEL 10, CLOUDS, STAR TV, TBC, WASAFI, nk. Ubure huo tunaoimbiwa kila siku uko wapi?
 
TBC haiwezi kufunguwa kwa sababu iko kisheria kama Tv ya Taifa. Kila nchi kama unakimbusi chako basi kisheria lazima Tv ya Taifa ioneshwe bure. Ndio maana unaona pamoja na kufungiwa channels zingine kwenye DSTV na Azam lakini TBC bado inaoneshwa tu.
 
Hahahaa sina hasira mkuu!! Hasira juu ya nini brother?wakati pekee nilipomkaribia kukasirika ni kipindi kile JF iliwekwa sero! Tofauti na hapo sijaona cha kunikasirisha mkuu,kuhusu KUROPOKA sijui! Mi nadhani nimeelezea fikra na maoni yangu tu! Unaruhusiwa kuyapa tafsiri unayoona ina fit matakwa yako mkuu,pamoja sana!
 
Mbona unaconclude mkuu, ulikua na wazo lako ndo umeamua kulisema hivyo, kwahiyo ww unapenda kulipia stesheni za ndani au hupendi
Nina conclude? Umesoma nilichoandika mpaka mwisho? Nimesema kama mimi ndo sielewi nieleweshwe. Sass nimeconclude hapo??

Haya sasa swali langu la msingi ni hili : Niambie we mwenyewe siku walipofungiwa TCRA walisema sababu ya hizo Tv stations kufungiwa. Ulisikia walisema sababu ni hiyo ya kutooneshwa bure??

Tuache kumezeshana kwa lengo la kuitetea serikali kwa itikadi zetu. Tuseme ukweli wenyewe.

Nasubiri majibu yako sio kwa kubishana bali kwa kueleweshana na watz wengine.
 
"Wanaposema chanel za bure" akina nani?? TCRA wenyewe ndo walivyosema kwamba ndo sababu ya kuzifungia? Sababu ya kufungiwa hamkuisikia wakati zinafungiwa?

Yaani unawasikiliza watu tu wanavuojaribu kutengeneza mazingira ya kuitetea serikali na unaifanya ndio sababu rasmi ya kufungiwa??

Sababu sio hayo maswala ya chanel za bure. Labda kama mi ndo nakosea nipewe copy ya speech ya TCRA wakati wanazifunvia hizi stations.
 
YAANI NI WAPUUZI KABISA, ETI TCRA !!!!! NONSENSE KABISA,.
 
Hii naipataje mkuu, manake mie nimebaki kutizama azam one, two, azam sport 2 na azam sport HD basi.
 
Ni ngumu kwangu kuangalia TBC 1 angalau dk 30 mfululizo inakinzana sana na utashi wa akili yangu!Lakini haina shida najifariji na K24.Kama wanaamini wataipaisha TBC1 ngoja tuone!
 
Clouds 360 bora ukisahau tu ni cha kikuda kile kipindi..
 
Mawazo yako tu, sio kila anayelalamika akifika kwake haangalii TBC, unajua kila mtu ana familia yake, mnakutana mtaani mnaponda kila kitu akifika kwake anaangalia fresh tuu
watakuwa wana roho ngumu sana ! unaangaliaje TBC Aiseee , halafu unaangalia kipindi gani , cha uchambuzi wa Le Mutuz kuhusu Meli ?
 
Tatizo mikataba yao wanaosaini ni ya kuwabeba startimes na wenzake na sio DSTV wala AZAM maana hata serikali itoe tamko kwamba DSTV na AZAM waonyeshe bure hizo channel bado hivi ving'amuzi vingine vinaweza kwenda kortini kuhoji leseni zao...kikubwa serikali inapoanzisha kitu iangalie na nchi jirani kwanini wao local channel zipo kwenye hivi ving'amuzi kama DSTV na wanapata manufaa gani kabla ya kuanza kutenganisha leseni za wanaorusha kwa kulipia na wasiolipia. MAANA HATA HAO STARTIMES WAMEANZA KUONYESHA BURE HIVI KARIBUNI VINGINEVYO WALIKUWA WANAKUACHIA WIKI 2 ALAFU BAADAE ZINAKATA ZOTE WANAKUACHIA TBC na TV1
 
Kwani hao Srattimes local channels ni za bure?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…